Nini sababu ya wabunge wa CCM kusema ndiyo na kupiga makofi kwa jambo litaloleta athari baadae?

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,131
2,000
Ndugu zangu,

Ningependa kujua sababu zinazowapelekea wabunge wa CCM kusema ndioooo hata kwa jambo ambalo wanajua wazi kuwa litakuwa na athari kubwa kwa taifa.

Mifano ni mingi sana ya mambo mbalimbali ambayo wabunge wa CCM wamewahi kuyapitisha kwa sauti kubwa za ndiooooo, na kupiga meza pwaa, pwaa, baada ya muda wakajikuta wameanza kulaumu kile walichokiamua na kuhisi hawakuwa miongoni mwa wale walihusika kupitisha jambo hilo. Wakati mwingine wafikia hatua ya kuhisi wakati jambo hilo linapitishwa CCM haikuwa madarakani bali chama kingine.

Kama ni kweli rafiki yangu mmoja amekuwa akiniambia kuwa wabunge wa CCM wakiwa bungeni wanapatwa na hali fulani hivi inayoteka ufahamu wao, wakitoka tu nje hali ya kawaida inawarudia. sijajua kama ni kweli au la.

Walipitisha kwa mbwembwe ununuzi wa ndege ya Rais wakati ule wa Rais Mkapa ndege ambayo ilinunuliwa kwa dhihaka kubwa kwa kuwaambia watanzania kama ni kula majani wananchi bora wale ila ndege ya Rais itanunuliwa tu, matokeo yake tuliletewa mtumba.

Wakapitisha kwa mbwembwe sheria za uchimbaji wa madini, tena kwa hati ya dharula. Wakapitisha sheria za kuchimba geni kwa hati ya dharua pia, Leo wamesahau kuwa ni wao waliopitisha sheria hizo, wameanza kulaumu wale wanaotaka sheria hizo zifanyiwe review kwanza.

ESCROW ndio hiyo ambayo kwa bahati mbaya JK alisema si pesa za Umma wakapiga tena meza pwaa, pwaa, pwaa. Leo wameanza tena kukubaliana na wale waliosimama kidete kutetea mali ya umma. Kaka yangu Kafulila aliitwa Tumbili wakapiga meza pwaa, pwaa,pwaa.

Hivi wabunge wa CCM kuna roho gani inawaingia wakiwa bungeni?
 

mwenda wazimu

JF-Expert Member
Feb 20, 2017
823
1,000
Tatizo ni kwamba waliingia bungeni kuganga njaa zao na sio kuisaidia nchi na ndo mana wakiwaona tu mabosi wao pale mbele wanawaza kusema ndio mana mlija unaweza katwa mda wowote ikisikika sauti yako inasema hapana,pili ni kujua kusoma na kuandika tu!!!!! ndo kinawaponza
 

charty

JF-Expert Member
Oct 28, 2013
7,414
2,000
Hawa wabunge tatizo lao kubwa ni NJAA YA PESA na NJAA YA KUWA NA MADARAKA! Mara nyingi wanakua wamepewa vifungu vya pesa kupitisha kitu fulani bungeni.Wengine pia wanaogopa kusema hapana kwa kuhofia kuwaudhi wakubwa zao, haswaa mwenyekiti.Ndio maana wanaona bora liende tu, ilimradi matumbo yao yashibe.Hakuna mzalendo hata mmoja.
 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,600
2,000
Wewe unahisi kuna kitu gani kinawaingia kiasi cha kushindwa kujali maslahi mapana ya taifa na kujali zaidi chama chao?
Zikaguliwe seat zao!! Inawezekana kuna vitu vyenye kujipenyeza vertically, kwa hiyo kila wanapokaa inaleta mind upsetting.
 

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,131
2,000
Zikaguliwe seat zao!! Inawezekana kuna vitu vyenye kujipenyeza vertically, kwa hiyo kila wanapokaa inaleta mind upsetting.


You might be right, because they are normal people when they are outside and somewhere else. Ila wakiwa ndani ya bunge hata kama huyo mtu ni mlokole wa kweli akishakuwa tu mbunge wa ccm anaweza kusema ndio kwa kitu ambacho ni hatari kwa nchi na wananchi wake.
 

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,474
2,000
Mambo ya "sijui tumerogwa na nani" ni visingizio tu, ujinga ndio tatizo kubwa!
 

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,131
2,000
Mambo ya "sijui tumerogwa na nani" ni visingizio tu, ujinga ndio tatizo kubwa!


Inawezekana kimelogwa maana Nyerere alisema ccm inanuka, pia matendo ya ccm kwa wananchi yanaweza kusababisha laana inayosababisha ufahamu wao kushindwa kufanya maamuzi sahihi wakati wa maamuzi pale bungeni
 

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,474
2,000
Inawezekana kimelogwa maana Nyerere alisema ccm inanuka, pia matendo ya ccm kwa wananchi yanaweza kusababisha laana inayosababisha ufahamu wao kushindwa kufanya maamuzi sahihi wakati wa maamuzi pale bungeni
Umenipa mwanzo mwingine wa kufikiri aisee, pana ukweli hapa maana yanayofanyika ni ngumu kuyaamini hata kwa binadamu mwenye IQ below 5!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom