Nini sababu ya Samuel Sitta kuchapwa viboko enzi za Mwalimu?

Dijovisonjn

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
467
250
Heri ya Mwaka mpya wadau wa JF!

wadau huwa kuna habari kuwa wakati waziri wa sasa wa Afrika Mashariki ndugu Samuel Sitta anasoma pale UDSM, mwalimu Nyerere aliwahi kuhamrisha achapwe viboko. Napenda kujua Mheshimiwa alikosa nini hadi akachapwa viboko na kwanini yeye tu alichapwa na sio wenzake aliokuwa nao?!
Nashukuru.

Wakati S Sitta akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu UDSM alikumbana na kadhia hiyo ya kuchapwa viboko na Mwl nyerere kama sharti la kurudishwa chuoni. Sitta alituhumiwa kuwa kinara wa mgomo huo.

Ilivyokuwa:

Wanafunzi waligoma na kuandamana kupinga kujiunga na jeshi la kujenga Taifa na kukatwa mishahara yao baada ya kumaliza jeshi.

Baada ya shinikizo hilo la wanafunzi Nyerere alikubali kupunguza mshahara wake wa Tsh 4000 bila kodi na kuagiza pia mishahara ya mawaziri ipunguzwe kwa asilimia 2. Miezi miwili baadae akatangaza azimio la Arusha kuyapa nguvu malalamiko ya wanafunzi hao.

Sitta na Mwabulambo (sasa ni marehemu) na wengine kadhaa waliojitoa muhanga kutetea kile walichokiita haki zao, walimshutumu Mwl Nyerere kwa maneno makali wakidai " Ni heri wakati wa ukoloni kuliko utawala wa Mwalimu.

Mwalimu Nyerere alikasirika na kuwafukuza wanafunzi wote 400 kwa kile alichokiita " kwenda kufunzwa adabu majumbani mwao".

Hasira zilipoisha mwalimu aliamua kuwarudisha wanafunzi 392 tu huku sitta na wenzie 7 wakiendelea kubaki nyumbani.

Mwalimu alipobembelezwa sana alikubali kwa sharti la kuwatandika viboko watukutu wawili (Sitta na Mwabulambo) yeye mwenyewe.

Hii ndiyo ilikuwa pona ya Sitta ambaye alirejea UDSM na kuendelea na masomo kwa miaka kadhaa hadi alipohitimu mwaka 1971.

Chanzo: Mwananchi, Juni 4, 2015.
 
mapinduzi daima

JF-Expert Member
Sep 30, 2013
1,582
2,000
Heri ya Mwaka mpya wadau wa JF!
wadau huwa kuna habari kuwa wakati waziri wa sasa wa Afrika Mashariki ndugu Samuel Sitta anasoma pale UDSM, mwalimu Nyerere aliwahi kuhamrisha achapwe viboko. Napenda kujua Mheshimiwa alikosa nini hadi akachapwa viboko na kwanini yeye tu alichapwa na sio wenzake aliokuwa nao?!
Nashukuru.

Muungwana Dijovisonjn ...Mh. Samwel Sita kipindi hicho alikuwa kiongozi wa wanafunzi pale UDSM, kukawa na mgomo juu ya sera na taratibu za uendeshaji wa chuo kwa wanafunzi. Wanafunzi/wanachuo wakawa wanapinga sana. Basi mgomo ulipopamba moto, YEYE kama Kiongozi akasimama na kusema..."Ni heri kuongozwa na Serikali ya Kikoloni kuliko Serikali ya Mwl. Nyerere iliyo ya kidkiteta na Ukandamizaji Mkubwa ....."

Daah, HAKIKA alichochea Mgomo zaidi...Mwl. JK Nyerere, akaamrisha akamatwe HARAKA na KUCHAPWA VIBOKO VYA KUTOSHA SANA. Yote hayo yalitekelezwa na mgomo ukazimwa kwa NGUVU YA MWL. Nyerere.

Lakini, baadaye Mh. alipomaliza chuo na kuingia Serikalini..Mwl alimpenda sana baada ya kutumwa na Mwl. kwenda Ulaya kununua Meli au magari ya Serikali kama sikosei.

Kufika kule...kama kawaida ya Wazungu...wakamweka chemba na kumwambia kuna mgao wako mkubwa...ili bei iwe juu na meli mbovu iletwe.

Jamaa akarudi bila kununua akamwambia Mwl JK kila kitu, Nyerere akasema u-kijana mwaminifu sana.....ila baadaye mzigo ulinunuliwa na hela ile ya ziada ikaingizwa Serikalini
 
Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,327
2,000
Aliyechapwa alikuwa Wilfred Mwambulambo tena mwaka mwingine kabisa, na kwa tukio jingine kabisa la kuwakoromea wamarekani jambo ambalo Nyerere hakutaka lifanyike waziwazi.
 
BWANANDUGU

Member
Jan 1, 2014
28
0
Heri ya Mwaka mpya wadau wa JF!
wadau huwa kuna habari kuwa wakati waziri wa sasa wa Afrika Mashariki ndugu Samuel Sitta anasoma pale UDSM, mwalimu Nyerere aliwahi kuhamrisha achapwe viboko. Napenda kujua Mheshimiwa alikosa nini hadi akachapwa viboko na kwanini yeye tu alichapwa na sio wenzake aliokuwa nao?!
Nashukuru.

Ni kwa sababu ya ukorofi,c unajua kuwa kiboko ni cha mtoto mkorofi?
 
Dijovisonjn

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
467
250
Nashukuru sana mkuu.
Muungwana Dijovisonjn ...Mh. Samwel Sita kipindi hicho alikuwa kiongozi wa wanafunzi pale UDSM, kukawa na mgomo juu ya sera na taratibu za uendeshaji wa chuo kwa wanafunzi. Wanafunzi/wanachuo wakawa wanapinga sana. Basi mgomo ulipopamba moto, YEYE kama Kiongozi akasimama na kusema..."Ni heri kuongozwa na Serikali ya Kikoloni kuliko Serikali ya Mwl. Nyerere iliyo ya kidkiteta na Ukandamizaji Mkubwa ....."

Daah, HAKIKA alichochea Mgomo zaidi...Mwl. JK Nyerere, akaamrisha akamatwe HARAKA na KUCHAPWA VIBOKO VYA KUTOSHA SANA. Yote hayo yalitekelezwa na mgomo ukazimwa kwa NGUVU YA MWL. Nyerere.

Lakini, baadaye Mh. alipomaliza chuo na kuingia Serikalini..Mwl alimpenda sana baada ya kutumwa na Mwl. kwenda Ulaya kununua Meli au magari ya Serikali kama sikosei.

Kufika kule...kama kawaida ya Wazungu...wakamweka chemba na kumwambia kuna mgao wako mkubwa...ili bei iwe juu na meli mbovu iletwe.

Jamaa akarudi bila kununua akamwambia Mwl JK kila kitu, Nyerere akasema u-kijana mwaminifu sana.....ila baadaye mzigo ulinunuliwa na hela ile ya ziada ikaingizwa Serikalini
 
Dijovisonjn

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
467
250
Issue ya Wilfred Mwambulambo ilikuwa katika mgomo wa kushinikiza uhuru wa Zimbabwe, ila mh. Sitta naye aliwahi kuchapwa!
Aliyechapwa alikuwa Wilfred Mwambulambo tena mwaka mwingine kabisa, na kwa tukio jingine kabisa la kuwakoromea wamarekani jambo ambalo Nyerere hakutaka lifanyike waziwazi.
 
platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
8,791
2,000
TBC wana clip yenye sauti za hao wanafunzi walipokuwa wakipigwa viboko.
Na si Sitta peke yake, kuna Balozi Ally Mchumo pia.
 
DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
1,170
2,000
Naombeni mnijuzi wakuu, Ilikuwaje mheshimiwa huyu anayeita viongozi wa dini wapuuzi, Akanyukwa bakora na Mwalimu Nyerere alipokuwa Chuo Kikuu - MLIMANI?
 
Baba Joseph17

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
8,502
2,000
Naombeni mnijuzi wakuu, Ilikuwaje mheshimiwa huyu anayeita viongozi wa dini wapuuzi, Akanyukwa bakora na Mwalimu Nyerere alipokuwa Chuo Kikuu - MLIMANI?

Aliongoza mgomo wa kutaka wale vyakula vya kizungu chuoni kwani walijiona wao hawawezi kula ugali nyama na wali maharage. Akakutana na JK Nyerere akamwita ikulu ili wakajadiliane na yeye akaenda kichwakichwa kilichompata huko mnakijua
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom