Nini sababu ya Nape kutaka suluhu na CHADEMA juu ya DOWANS?

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,883
Hatua ya Nape kutoa pendekezo la kukutana viongozi wa CCM na Chadema kujadili kuhusu kupinga malipo ya Dowans si kitu cha kukichukulia kiulaini, nyuma ya pazia kuna kitu kinachozungukwa na hivyo kutafuta weak point kukutana na Chadema ili kufunika jambo fulani.

Mengi yametokea huko Igunga na bado yanaendelea kutokea na hivyo kuleta maswali wengi yasiyojibika.

Je? CCM yataka kujisafisha?
Chadema wakubali kukutana nao?
Nini nyuma ya pazia la CCM?
 
CCM wajifie wenyewe wasije wakatusingizia CDM

Kinachonishangaza CCM wameshona midomo, hawaongelei, wala kusikitikia vifo vya kutatanisha vya makada wa Chadema, hiyo si dalili nzuri kwa umoja wa kitaifa, maana itikadi si vita au ugonvi, ndio maana baada ya kumwaga sera tunaachiwa wananchi kufanya maamuzi kwa kila moja kwa ridhaa ya moyo wake.
 
Damu za wana Igunga zimeanza kuwalilia kina Nape Nchemba na Wassira.
 
Hatua ya Nape kutoa pendekezo la kukutana viongozi wa CCM na Chadema kujadili kuhusu kupinga malipo ya Dowens si kitu cha kukichukulia kiulaini, nyuma ya pazia kuna kitu kinachozungukwa na hivyo kutafuta weak point kukutana na Chadema ili kufunika jambo fulani. Mengi yametokea huko Igunga na bado yanaendelea kutokea na hivyo kuleta maswali wengi yasiyojibika. Je? CCM yataka kujisafisha? Chadema wakubali kukutana nao? Nini nyuma ya pazia la CCM?

Bull crap, mbona wakati wanatafuta kampuni ya kuleta umeme hawakuomba kukutana na viongozi wa CDM? Iweje hatua ya malipo imefika ndiyo waone wanahitaji umoja nao?
Kwa vile huwa wanaona sifa kupitisha kila ujinga bungeni na kugonga meza acha waicheze ngoma hii peke yao; isitoshe hakuna anayejua nini msimamo wa CCM - kulipa au kutolipa.
 
Wanasiasa wote wa Kitanzania ni wanafiki. Wapo kwa maslahi binafsi.
 
Wanasiasa wote wa Kitanzania ni wanafiki. Wapo kwa maslahi binafsi.

Nipo kinyume na mtazamo wako, your comment looks too general, try to double check and over look, you can observe something else than what you outlined.
 
Hawa wehu wanaopitisha maamuzi Bungeni kishabiki leo wanaomba msaada dhidi ya maamuzi yao!!!!!!!!
UKILIKOROGA ULINYWE MWENYEWE.
 
Wangeanza kuwapatanisha Mwigulu na yule aliyemwibia Mke...

CCM na itikadi za funika funika, means to paper cracks on the wall, unaona kama kumepambwa picha kumbe ni mbinu za kuficha crack na siku hii funikafunika itakapofumuka kila mmoja atakimbia maana hakivumiliki kitu.
 
Hawa wehu wanaopitisha maamuzi Bungeni kishabiki leo wanaomba msaada dhidi ya maamuzi yao!!!!!!!!
UKILIKOROGA ULINYWE MWENYEWE.

Usiamini kama msaada, ila ni chambo cha kutaka wakutane na Chadema mezani kwani mambo mengi yawewia magumu hasa mauaji yaliyotokea Igunga yanawaumiza kichwa hadi kufikia kukaa kimya bila kutolea tamko. Ni aibu.
 
Chadema wanataka kufunga ndoa na ccm

Bila aibu wataanza kusifia hiyo ndoa umoja wa kitaifa

Watataka tusahau kuwa wao wanasema cuf na ccm wana ndoa

keep on watching
 
Wee Topical, ndo Nepi? AU umetumwa na Nepi. Hatudanganyiki ng'o. Na mtabumburuka mwaka huu, hata mkibadilisha ID elfu
 
Wee Topical, ndo Nepi? AU umetumwa na Nepi. Hatudanganyiki ng'o. Na mtabumburuka mwaka huu, hata mkibadilisha ID elfu

Hakuna ujanja nyie 2015 mtaingia serikalini kama ndoa..watch my word

Siku hiyo, ndoa mtaisifu wenyewe nakwambia..japo sasa hivi mnaitumia kuiua cuf.
 
Back
Top Bottom