Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Amani iwe nanyi wadau!
Leo naomba niandike mada ngumu kwa wengi Ila nyepesi kwa wachache wenye akili na jicho la tatu!!
Mada hii imetokana na Jarida la African Report kuandika Makala inayoelezea kwa Jinsi gani Rais Samia anaweza pata ugumu katika kushawishi Kujengwa kwa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo baada ya majadiliano ya kwanza yalioanza mwaka 2012/2013 kukwama mwaka 2019 hadi pale Rais Magufuli alivyoamua kuachana na hayo majadiliano (Kuachana na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo)
Kwenye Jarida hili wameelezea mambo machache yanayoweza kufanya China asiwe na interest tena na Bandari ya Bagamoyo ikiwemo suala la China kuanza kujenga Bandari ya Djibout, Uwekezaji Mkubwa kwenye Bandari ya Lamu ambao umeshaanza kutake effect Kama vitu vitakavyoweza kuwafanya wachina wasiwe na interest tena kwenye ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo jambo ambalo Kwa upande mwingine inamaanisha kuwa mradi utakuwa umefeli.
Makala hii imenifanya niwaze sana juu ya miradi mingi iliyochelewa kufanyika kwetu na ikafanyika kwenye nchi jirani na wakapata faida kiuchumi na kwenye ajira. Niligundua sio mradi huu tu, kuna mradi wa Kiwanda cha kuchakata Gesi ambacho nacho kilitakiwa mpaka sasa kiwe kimeshaanza kujengwa au kinakaribia kumalizika, Kuna mradi wa Barabara ya Maloli, kuna mradi wa treni ya umeme katikati ya jiji la Dar es Salaam na miradi mingine mingi ambayo ni kama ilicheleweshwa kwa siasa ama propaganda fulani au imekuja kuanza baadae baada ya miradi kama iyo kufanyika nchi nyingine hasa za majirani.
Leo hii Pia Tanzania tukiwa tunaanza mchakato wa kujenga kiwanda cha kuchakata gesi, kule juu Egypt( Misri) wanakamilisha kiwanda chao Kwa ajiri ya soko la Ulaya na nchi nyingine za Africa. Hili limetangazwa pia kwenye jarida la African Report!
Makala hii imenifanya pia niwaze Kama Je Tanzania tungekuwa wa kwanza kujenga Bandari kubwa ya kisasa kwa ukanda wetu huu kuzidi Djibouti na Kenya tungekuwa wapi kiuchumi leo hii? Soko la kusafirisha bidhaa si lingekuwa kwetu?? Ajira si zingekywa kwetu, mapato na kodi makubwa si yangekuwa kwetu?
Makala hii imenifanya pia niulize Kama na sie kiwanda chetu cha kuchakata Gesi kingekuwa kinaenda kuanza kazi kama cha Egypt na kingetangulia kile cha Msumbuji tungekuwa wapi leo hii kimaendeleo? Au uwekezaji kwenye utafiti wa Gesi ungeendelea je Leo tungekuwa wapi?
Maswali haya yamenifanya niwaze kuwa Kuna hujuma kubwa imepenyezwa na majirani zetu kwenye nchi yetu hasa kwenye siasa na kwenye ngazi ya maamuzi ambayo kazi yake kubwa ni ku sabotage mipango mizuri yetu ya maendeleo ili either ichelewe au ikwame na wenzetu wawe mbele zaidi yetu zaidi kimaendeleo.
Hadi Leo nashindwa kuelewa ni kwa nini majadiliano yalioanza mwaka 2012/13 ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo yalikwama hadi Kenya na Djibouti wameanza ujenzi wa mega project zao za Bandari.
Hadi Leo nashindwa kuelewa ni kwa jinsi gani uwekezaji wa gesi uliotakiwa uwe umefikia hatua Nzuri na kuanza kuleta matunda ulikwama hadi msumbiji na sasa Misri wamekamilisha miradi yao ya LNG na kuanza kuteka masoko.
Je, Tanzania ianze kujisafisha na Majasusi wanaohujumu maendeleo yake wanaotumia Siasa na Ngazi za Juu za Maamuzi kuhujumu maendeleo yake?
Naomba mnisaidie majibu wanabodi