Tatizo la masikio: Fahamu kuhusu sehemu za sikio, magonjwa, ushauri na tiba

Hata mimi nina hilo tatizo sikio langu la kushoto halisiki kabisa. Nilienda Regency nikafanyiwa kipimo cha CT Scan nikabainika sina tatizo kabisa ila walinishauri nitumie Ear machine ya kuweka sikion ili inisaidie kusikia.Nilishindwa bei yake kutokana na gharama ambapo Semi digital ni Laki 650 na 1.5M kwa advanced yake.

Ila kuna doctor alinishauri kwamba kama sikio langu la kulia linasikia vizuri heri niache kutumia kifaa cha kusikia sababu nikitumia kifaa kwa sikio moja kusikia kuna uwekazekano nikaathiri na sikio langu la kulia. Tokea hapo sijahangaika tena kuhusu sikio.

Nishajizoelea na hali yangu nashukuru Mungu.
 
Kante98,
umenikumbusha baba yangu (R.I.P) alikuwa na tatizo kama hilo na hilo lenye usikivu hafifu lilikufa kabisa akatumia hiyo mashine ,mwishoni ilifika point bila mashine hasikii kbs.
 
kama sikio lingine linasikia vizuri ni bora kuachana na machine.
Mi nilishauriwa mapema nkaacha kufuatilia kabisaa.
 
MziziMkavu,
Habar yako mzizi mkavu,

Mimi nimeamka leo asubuhi sikio langu moja la kulia limeziba alafu sisikii vizur,saut mtu akiongea unakua na mitetemo na muhungurumo mzito kiasi kwamba sielewi nini mtu anasema, na saut inakua kali sana.

Naomba unisaidie nini Tatizo sielewi hata dawa ya Kutumia
 
Jamani nami nasumbuliwa na tatizo hili la kutokusikia yaani naweza sikia lakini nisielewe kinachozungumzwa,pia uchafu hautoki masikioni kiasi kwamba yameziba hata maji hayapiti.Naombeni ushauri wenu wapendwa
 
UKIENDA PHARMACY KUNA DAWA YA MAJI INAITWA BORIC ACID UKIIDONDOSHEA SIKIONI HATA KAMA UCHAFU UMEGANDA UNAYEYUKA NA UNATOKA.
MIMI NILIKUA NINA TATIZO HILO LIKAISHA.
 
Asante kwa kutupa pole wale tusikiao kwa sikio moja. Sikuwa najua kwamba Binadamu husikia kwa masikio yote mawili na hivyo sikuwa na wasiwasi hadi pale nilipoanza shule ndio nikagundua matatizo niliyozaliwa nayo. Namshukuru Mungu kwa kunifikisha hapa nilipo leo ingawa kwa sasa uwezo wa kusikia unazidi kupungua.
Pole.
 
Jamani nami nasumbuliwa na tatizo hili la kutokusikia yaani naweza sikia lakini nisielewe kinachozungumzwa,pia uchafu hautoki masikioni kiasi kwamba yameziba hata maji hayapiti.Naombeni ushauri wenu wapendwa
Umejaribu hospitali?

Ipo dawa fulani nzuri sana ya maji unaweka drop moja tu kila siku usiku...nikiikumbuka nitatuma picha

Cha msingi usiingize chochote katika sikio
 
Back
Top Bottom