Tatizo la masikio: Fahamu kuhusu sehemu za sikio, magonjwa, ushauri na tiba

Kuna wakati wax hushindwa kutoka sikioni kama imezidi. Hali hiyo hufanya usikivu uwe hafifu. Muone Daktari atakuchunguza na kutambua chanzo baada ya kukupima sikio hilo kwa tochi maalum ya sikio.
 
Wakuu, huwa ninapata au kusikia sauti fulani masikioni mwangu si muda wote lakini, ila kwa sasa zimezidi. Kuna sauti naweza kusema kama filimbi lakini zenye mlio mdogo zinakuwa kama zinapuliza feeeeeee. Nafikiri wapo pia wanaofahamu hili kwani watu huwa wanasema ukisikia hivyo basi kuna watu wanakusema, ni common sana kusikia watu wakisema hivyo. sasa kinachonishangaza ni jinsi ambavyo zimezidi kwa hivi sasa hasa tangu mwaka jana nilipoamua kujikabidhi kwa Mungu na kuanza kuwa mtu wa maombi sana. (mimi ni mkristo). Kinachonishangaza ni pale ninapokuwa ninaomba au ninapojiandaa kusema ngoja sasa niombe, basi ghafla nasikia masikio yakianza kufanya hivyo na inaweza kuchukua dk kadhaa. Mara nyingine huwa mpaka nahisi kama masikio yanakuwa mazito. Je kuna mwenye uzoefu hii inaweza ikawa inasababishwa na nini?

Tinnitus - Wikipedia
 
Habarini wanajamnvi...

Ni kwamba mimi kwa muda wa takribani mwezi mmoja nimekuwa nikisumbuliwa na tatizo la kuziba kwa sikio kama limeingiliwa na maji wakati halijaingiliwa na maji au kitu chochote.

Pia kutokana na kuziba huko nimekuwa nikitumia "cotton buds" (pamba) kukwangua kwa ndani ili kama kuna uchafu(nta) utoke. Hata hivyo hakuna uchafu mwingi utokao na kuziba kunaendelea!

Sasa basi, sijui kama "cotton buds" ndio sababu ya maimivu hayo au laa. Kwamba, pamoja na kuziba kwa sikio(ingawa na sikia ila sio kwa kawaida), pia nimekuwa nikijisikia maumivu fulani ivi kwa ndani ya sikio.

Hivyo basi ninaomba msaada na ushauri wa kitabibu wanajamnvi...

Nawasilisha.
 
Kuna mtu nayemfahamu alishawahi kuwa hivi akaenda hospital akaekwa bomba uchafu ukavutwa ukaisha
Ila nasikia inauma...nakushauri uende hospital

Ila mafuta ya kuku inasemekana pia ni dawa
Asante sana
 
Habarini wanajamnvi...

Ni kwamba mimi kwa muda wa takribani mwezi mmoja nimekuwa nikisumbuliwa na tatizo la kuziba kwa sikio kama limeingiliwa na maji wakati halijaingiliwa na maji au kitu chochote.

Pia kutokana na kuziba huko nimekuwa nikitumia "cotton buds" (pamba) kukwangua kwa ndani ili kama kuna uchafu(nta) utoke. Hata hivyo hakuna uchafu mwingi utokao na kuziba kunaendelea!

Sasa basi, sijui kama "cotton buds" ndio sababu ya maimivu hayo au laa. Kwamba, pamoja na kuziba kwa sikio(ingawa na sikia ila sio kwa kawaida), pia nimekuwa nikijisikia maumivu fulani ivi kwa ndani ya sikio.

Hivyo basi ninaomba msaada na ushauri wa kitabibu wanajamnvi...

Nawasilisha.
Pole sana Huo ni uvimbe wa kipele unaopelekea uhisi kama sikio limeingia maji nahiyo imesababishwa na cotton buds tumia antybiotics itakusaidia.
 
Nenda hospital mapema sana! Inawezakuwa ni ugonjwa wa fungus ya sikio.
Acha kuchokonoa fika kwanza hospital.
 
Unaweza kuweka mafuta ya kula yasiyoganda kwenye kijiko cha chakula, kisha dondoshea tone moja au mawili ya mafuta ya taa kisha yakoroge kwa kidole yachanganyike na kisha weka sikioni, na uzibe na pamba safi.utapona.

Kwa maumivu yoyote ya sikio, hasa sikio linalotoa usaa ,dawa yake ni majani ya bangi.
Chukua majini ya bangi , ukipata mabichi ni vizuri. Yafikiche kwa vidole mpaka yawe kama yamepondwa, kisha yadondoshee maji , kisha dondoshea ndani ya sikio, ziba kwa pamba safi mpaka asubuhi.

Hili dawa iliniponyeshea watoto wangu mawili waliokuwa wakitokwa usaa sikioni.
 
Unaweza kuweka mafuta ya kula yasiyoganda kwenye kijiko cha chakula, kisha dondoshea tone moja au mawili ya mafuta ya taa kisha yakoroge kwa kidole yachanganyike na kisha weka sikioni, na uzibe na pamba safi.utapona .
Kwa maumivu yoyote ya sikio, hasa sikio linalotoa usaa ,dawa yake ni majani ya bangi.
Chukua majini ya bangi , ukipata mabichi ni vizuri. Yafikiche kwa vidole mpaka yawe kama yamepondwa, kisha yadondoshee maji , kisha dondoshea ndani ya sikio, ziba kwa pamba safi mpaka asubuhi.
Hili dawa iliniponyeshea watoto wangu mawili waliokuwa wakitokwa usaa sikioni.
Asante sana
 
sikio.jpg
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24 katika kukua kwangu nilipata tatizo la kutokwa na usaha katika masikio yote mawili. Nilipelekwa hospitalini bila mafankio mpaka nikaanza kutumia dawa za kienyeji ambazo binafsi sikupendelea kuzitumia ikabidi niachane nazo.

Ndugu zangu wana JF mpaka leo tatizo hili huwa linanisumbua sana kiasi huwa sisiki kwa haraka masikio huwa yanajaa usaha mzito na uchafu kila siku siku nyingine yanatoa usaha ule wa maji kuna muda mwingine huwa najaribu kuiskia lakini muda mwingi nahisi masikio ni mazito kabisa.

Sijawahi kwenda hospitali kubwa maana huku kwetu hospitali kubwa hazipo. Toka nianze kupatwa na tatizo hili yapata hata miaka 17 sasa lakini nashndwa kurudi hospitali za huku kwetu maana dawa ni zile zile hasa amoxyline na nimeshaenda mara nyingi bila mafanikio.

Wapendwa naombeni ushauri wenu niondokane na hili tatizo linanikosesha raha hasa pale nisiposikia kwa haraka na kutokwa na usaha.
 
Pole sana ushauri wangu wa kwanza jitahidi kutofautisha Facebook na Jamiiforum katika uandishi wako, unaweza ukawa na shida ya muhimu watu wakakupuuza.

Ushauri wa pili kama kwenu hakuna hospitali kubwa unashindwa vipi kupanda gari kufata huduma ya matibabu, una uhakika upo serious?

Kama una tatizo la kipato unashindwa kufika hospital anza kutumia Mafuta ya Habat soda wakati ukiendelea kutafuta pesa ya matibabu.

Kumbuka Kufika hospital ni lazima
 
Pole sana kwa matatizo, Fanya mawasiliano na uongozi wa jf uchangiwe pesa uende kwenye hospital kubwa kwa uchunguzi zaidi.
Ni sawa ila Mimi naishi kambini na kutoka huku kwenda mikoani ni process nyingi zinafanyika
 
Pole sana ushauri wangu wa kwanza jitahidi kutofautisha Facebook na Jamiiforum katika uandishi wako, unaweza ukawa na shida ya muhimu watu wakakupuuza.

Ushauri wa pili kama kwenu hakuna hospital kubwa unashindwa vipi kupanda gari kufata huduma ya matibabu, una uhakika upo serious?

Kama una tatizo la kipato unashindwa kufika hospital anza kutumia Mafuta ya Habat soda wakati ukiendelea kutafuta pesa ya matibabu.

Kumbuka Kufika hospital ni lazima
Asante kwa ushauri, ila hospital nilienda sana na niliwahi kuwaambia wanipeleke hospitali za mikoa lakini mchakato huo kila siku nilikuwa naambiwa njoo kesho mpaka leo.

Ukweli suala na kifedha siko vizuri maana mimi naishi kambini Nyarugusu na hakuna shughuli yeyote ninayofanya maana haturuhusiwi kufanya shughuli yeyote.
 
Nenda hospitali kubwa sasa kwanini umeng'ang'ania huko huko?
Hata na mimi napenda kwenda kwenye hospitali kubwa ila kipato changu hakiruhusu niliwahi kufuatilia kupewa transfer lakini mpaka leo sijapata
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom