Nini sababu Choo cha kulipia stendi ya Mbezi Mwisho kutoza 500 tofauti na 200 ilivyozoeleka?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,501
26,999
Mambo ya uchumi wa kati!

Kwa hapa Bongo, kwa uzoefu wangu mdogo. Maeneo mengi ya umma hutoza 200 kwa huduma hiyo pendwa, na 500 kwa kuoga.

Hii imekuwa tofauti katika stendi ya daladala Mbezi Mwisho, Dar es Salaam. Bei ni Tsh 500/- tu, nini sababu ya tofauti hii?

Je, ni bei elekezi au wajanja wamejiongeza kiupigaji?

NB: Lipa kodi kwa maendeleo ya Taifa lako.
 
Unapewa Risiti yenye kusoma hiyo bei

Ila kwa wenzetu wa huko kujisaidia kwa 500 ni sahihi mzunguko wa pesa ni mkubwa sana huko
 
Ile stand ya Mbezi wahudumu ndio wezi, kila wanapokuzidishia 200 ni ya kwao, wandewa tunajua pale ukijisaidia tunatoa 300 iwe kubwa au ndogo....akikuangalia tu usoni anajua huyu anajua hajaribu kukata zaidi ya 300....
 
Wewe Usitumie, ila ukibanwa na tumbo hata 1,000 utatoa

Iliwahi kunitokea hii kumbe eneo la taasisi ya utunzaji mazingira, ile nakojoa tu wadau kama sita hawa hapa nikajua tu nimeisha.... mbona ilinitoka 15000/- kuwapoza!

Kivukoni pale karibu na geti la kuingia Chuo cha Nyerere.
 
Mambo ya uchumi wa kati!

Kwa hapa Bongo, kwa uzoefu wangu mdogo. Maeneo mengi ya umma hutoza 200 kwa huduma hiyo pendwa, na 500 kwa kuoga.

Hii imekuwa tofauti katika stendi ya daladala Mbezi Mwisho, Dar es Salaam. Bei ni Tsh 500/- tu, nini sababu ya tofauti hii?

Je, ni bei elekezi au wajanja wamejiongeza kiupigaji?

NB: Lipa kodi kwa maendeleo ya Taifa lako.
Itakuwa uchumi wa kati huo
 
Tatizo sio gharama za malipo 500.. Tatizo ni uchafu..
Hivi kwann vyoo vya umma vinakuwa vichafu kulinganisha na inchi zilizoendelea?
Tunakwama wapi?
1..vyoo havina lock kwa ndani,,unajisaidia huku umezuia mlango,
2.. Baadhi ya vyoo vimejaa,,maji hayatembei kwa wakati..
3..kukuta magogo ya watu wengine yameziba kwenye choo..
4.. Vyoo haviflash bado tunatumia makopo kweli?
5..hakuna sehemu utahifadhi nguo zako wakati wa kujisaidia.

Vyoo vile vya kujisaidia haja Dogo ni balaa,,
1.. Kukuta mkojo umejaa kwenye sink ni kawaida..
2..masink ya kujisaidia haja ndogo machafu sana,,
Yamebadilika rangi na kuwa njano..
Tunakwama wapi?
Pesa zote mnatoza za nn? Kama kuhudumia vyoo hamuwezi?
 
Tatizo ni corona, iliongeza matumizi ya vitakasa mikono

Sijawahi kuona hii bei ya 500 sehemu nyingine yoyote ya umma, mlimani city ni buuure ila unaweza kuingia na soda yako fureshiii tu!
 
Back
Top Bottom