Nini plan B baada ya vifurushi vya internet kupanda bei?

Option nnayotumia mimi ku access internet kwa gharama nafuu ni google wifi.
Gharama yake ni 30 usd per month. Unapata access kwa line tatu. Hii ni kama 66000 tu kwa mwezi.
 
Kama upo Dar maeneo ya Kariakoo, Mjini posta, Msasani, Peninsular, Upanga, Kinondoni ya Morocco, Mikocheni, Masaki, O'bey, n.k Kuna fiber za kutosha kama zuku, Raha, Gofiber, n.k

Fibre ni internet ya waya, unavutiwa waya hadi sehemu ulipo nyumbani kwako, ni internet ya waya lakini kuna kifaa utapewa kinaitwa wireless router, hiki kifaa kitakuwezesha utumie internet kwa wifi ya simu au laptop ama vifaa vingine vyenye wifi.

Kwa mfano internet ya fibre ya zuku inapatikana kino, kariakoo, msasani, peninsular, upanga,n.k utalipia elf 70 kwa mwezi (kifurushi cha chini) au zaidi (kuna vifurushi vina speed kali sana hivi ni kama watumiaji ni wengi na vina speed kali sana) pia hapo hapo utakuwa umelipia na channel za zuku utazocheki kwa kingamuzi.


A.10 Mbps = 69,000,
B.20 Mbps = 99,000
C.40 Mbps = 129,000
D.100 Mbps = 249,000.

Tukumbuke Mbps (Megabits per second) sio na zile megabytes ambazo huwa tunadownload, zile huwa na herufi kubwa ya "MB", ukitaka kujua unaweza kudownload MB ngapi kwa sekunde, hapa kilinganishi ni kwamba 1 Mbps ni sawa na MB 0.125 kwa hio mfano kifurushi A cha 10 Mbps ukifanya hesabu unapata uwezo wa kudownliad MB 1.25 kwa sekunde moja, ukija kifurushi B ni MB 2.5 kwa sekunde, n.k japo speed hushuka pale mnapokuwa watumiaji wengi mnaanza kugawana speed.

Utaweza kutumia internet bila kikomo, speed ni nzuri hata kwa kifurushi cha chini cha elf 70 ambacho unaweza kudownload mb 1 (nasikia sikuhizi ni 2) kwa sekunde, ni speed nzuri hata videos utaangalia bila kukwama na hata kwenye kudownliad utaweza kudownload muvi hata ya GB 1 kwa takribani dakika 18 tu, kitu kizuri zaidi ni hakuna kikomo, hakuna mambo ya ukifikisha gb kadhaa speed inashuka. Makampuni mengi gharama za vifaa na kuletewa waya wa internet hadi kwako ni bure ikiwa utalipia bando la mwezi au miezi kadhaa.

Changamoto ni kwamba haipo kila sehemu Dar na pia inabidi uwe mazingira ya nyumbani au ofisini ili kutumia wifi ya kifaa chao.

Kwa waliopo nje ya maeneo hayo au mikoani TTCL nao wana fibre sema nasikia ni gharama.

Kiukweli ni pigo kubwa, saizi wasanii wasahau kupata views nyingi kama zamani huko youtube, Internet ilikuwa silaha yetu kwa kuinua wasanii ila kwa hali hii jumna bovu limewaangukia
mkuu na dodoma ni kampuni gani zina gharama nafuu ukitoa ttcl tunatumia habarinode wanatuuzia mbps 2 kwa TSH.
100500
 
kutokana na vifurushi kuwa affordable hata sjawahi kufikiria kuwachek hao watu lakini hivi sasa itabidi tu,lamda kama kuna mtu alishawahi kuwachek atuambie hapa
Huyi alieniunga ni wa Jamiiforums. Nakitumia hadi sasa hivi.

mpaka dakika anaunga. Tsh 23,000
Screenshot_20211107-070037.png
 
Option nnayotumia mimi ku access internet kwa gharama nafuu ni google wifi.
Gharama yake ni 30 usd per month. Unapata access kwa line tatu. Hii ni kama 66000 tu kwa mwezi.
Mkuu tunaomba ufafanuzi kuhusu ii device inafanyaje kazi, na gharama zipoje na uliagiza wapi na mitandao gani inasupport kwa apa Tanzania na speed yake ipoje cc Chief-Mkwawa
 
Back
Top Bottom