Nini Nimejifunza kutoka Ze Utamu na RM/RA Saga

Mwanafalsafa;
Mimi bado mgeni hapa na pengine nimekosea. Samahani kwa hilo. Kuna hoja nyingi za kisiasa ndanimwe!
 
Wakubwa si ndio watawala wenyewe? Wao ni kama "wafalme wa mbingu ya duniani..." so, sisi "watwana" tulie tu? Mpaka lini?

Kuna mtu aliandika humu: Tutaendelea kuwavumilia viongozi wabovu mpaka lini?

Jibu mnalo!
 
Mimi nadhani system ya Rais ndio iliyofanya kazi yake katika kutimiza wajibu wa kumlinda kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria zote za nchi. Hakuna mwanasiasa yeyota alietakiwa kuwakumbusha UWT kuifanya kazi hiyo ambayo hufanyika automatically.

Kitu ambacho tunatakiwa kushinikiza kifanyike ni ulindaji wa haki za raia wote kutokana na uchafuzi unaofanywa na baadhi ya media kama ilivyofanywa na hao zeutamu. Nijuavyo mimi, kama mtu akipeleka malalamiko yake (based on facts) kuhusu kudhalilishwa, kutukanwa na kadhalika, vyombo husika vingechukua hatua na kutokana na uwezo wake, vingeweza kufanikiwa kuizima hiyo zeutamu siku nyingi tu. Lakini ifahamike kuwa mshughulikiaji masuala ya usalama wa Rais na msimamiaji wa masuala ya usalama wa Raia ni tofauti kabisa na hata bajeti zao ni tofauti sana. Usishangae kusikia kuwa UWT wanatengewa pesa nyingi zaidi (pamoja na uchache wao) kuliko jeshi la Polisi linalotakiwa kulinda watu wote ikiwa ni pamoja na mimi na wewe na kufanya uchunguzi wa yote yanayotakiwa kuchunguzwa.

Anyway, hivyo ndivyo tulivyo. Nadhani ndio maana inasemekana hadharani kabisa kuwa kuna wenye nchi na wananchi.
 
Karibu kwenye uwanja wa kupigana na jiunge kwenye kundi la watu mwenye msimamo wa dhati kama wakina Dr. Slaa na wengine, Kimbia kabisa huko ulipo na jitokeze hadharani na jiungeni nao
 
Mwawado;

Ninachofahamu, next day baada ya kumdhalilisha mkuu wa kaya, haikupatikana tena. For sure I know Intelpol na vijana wa ICT Usalama wa Taifa waliplay role kubwa.

Maoni yako mengine nakubaliana nayo with a note kwamba: Je mambo hayatokei nchi hii mpaka tu watu wakubwa waguswe?

usidhani wanaweza chochote....hakuna sana sana wanategemea interpol.
 
Zeutamu:

1. Wengi walilalamika kuwa zeutamu inawadhalilisha na wakataka ifungwe - hakuna aliyerespond.

2. Wengi walilalamika kuwa zeutamu imevunja ndoa zao na mahusiano na wapenzi wao na wakataka ifungwe - hakuna aliyesikiliza

3. Baadhi wakaandika kuwa kuna watu wamejiua kwa ajili ya zeutamu na wengine wajijidhuru na hata kuathirika kisaikolojia hakuna aliyesikiliza . . . .

4. Na hatimaye Mkuu Wakaya akadhalilishwa . . . . Usalama wa taifa hakuna aliyekuwa na amani, vijana wote wakaingia kazini, Police Force wakaingia kazini, Intelpol wakaingia kazini na hatimaye zeutamu haipo tena. Yote hayo yalifanyika katika muda mfupi sana . . . . . . .

RM/RA Saga

1. Wananchi wameumia sana miaka mingi kwa ajili ya ufisadi . . . hakuna aliyewasikiliza

2. Wananchi wamekufa sana kwa ajili ya umasikini ambao wakati mwingine umesababishwa na ufisadi hakuna aliyeshtuka

3. Hatimaye List of Shame ikatajwa . . . . Matokeo yakaanza kuonekana

4. Hatimaye Mafisadi wakubwa wakaanza kutajwa . . . na sasa mengi yafichuka na yataendelea kufichuka na najua kutakuwa na matokeo.

Just wondering . . . Nchi hii mambo hayafanyiki hadi wakubwa na mafisadi waguswe.

Nimejifunza kuwa ili nchi hii mambo yaende sasa ni lazima kuwagusa wakubwa na mafisadi?

Kama si hivyo . . . Why things do not happen the way they should happen?

Mhhh interesting
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom