Nini Nia Ya Butiku Na Wenzake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini Nia Ya Butiku Na Wenzake?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sumaku, Dec 8, 2009.

 1. S

  Sumaku Member

  #1
  Dec 8, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ( Nimeunasa mjadala unaopamba moto kule kwanzajamii.com

  Mbashiri said:
  Mchomeko;
  Ni nini hasa nia ya Butiku na wenzake?
  Na Abdul Mbashiri wa Mbashiri
  KWA watu walioshikilia madaraka, tena kwa miaka mingi, wakayatumia kama walivyopenda, wakitamba na hata kuonea watu lakini wakayapoteza madaraka hayo ghafla na wasijue jinsi ya kuyapata tena, siyo jambo la ajabu wala la kushangaza kusikia na kuona watu hao wakitapatapa kwa kauli zisizo za msingi dhidi ya utawala ulioko madarakani sasa.
  Wakubwa hawa wanadai kuwa nchi inakwenda ovyo. Kwamba nchi imejaa rushwa (wenyewe wamepata neno jipya la ufisadi). Kwamba nchi imegawanyika vipande vipande. Kwamba inafaa kurudisha Azimio la Arusha. Kwamba nchi inaharibiwa na Mtandao. Kwamba Rais Jakaya Kikwete amezungukwa na “majizi”.
  Hakuna namna bora zaidi ya kuzielezea kauli hizi zinazotolewa na watu ambao wamepata kuwa viongozi, tena wakubwa Serikalini, ila kusema kuwa kauli hizi ni kauli za hatari kwa uhai na usalama wa nchi, na kwa kweli ni ushahidi halisi za watu wanaotahayari baada ya kupoteza madaraka hata kama wanaendelea kuyasaka kwa udi na uvumba kwa njia nyingine.
  Pamoja na uhatari wake, hizo ndizo baadhi ya kauli zilizotawala Mjadala wa Kongamano la Miaka 10 ya Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, lililofanyika majuzi mjini Dar Es Salaam kwa kuandaliwa na Mfuko wa Mwalimu Nyerere (Nyerere Foundation).
  Hakuna shaka, hata kidogo, kuwa kongamano hili lilikuwa zuri na muhimu kumuenzi Baba wa Taifa, kiongozi ambaye pamoja na kwamba utawala wake haukuwa kamilifu hasa katika maeneo kama ya uchumi na utawala bora, bado alikuwa na anabakia kuwa nguzo kuu la Taifa la Tanzania, na nyota iliyong’ara na inaendelea kung’ara katika Bara la Afrika.
  Mwalimu Nyerere anabakia kiongozi ambaye amelijenga Taifa Huru la Tanzania, atabakia kiongozi mfano wa uadilifu, hasa wa mali. Waliomharibia wakati wa utawala wake na pengine wanaoendelea kuharibu jina lake kwa kulitumia vibaya jina hilo ni hawa akina Joseph Butiku, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere - Nyerere Foundation na wenzake ndani na nje ya taasisi hiyo.
  Hakuna njia mbaya zaidi ya kumuezi Mwalimu Nyerere kama wanavyofanya akina Butiku kwa kutumia jina la Mwalimu kama kichaka cha kuficha tamaa na laghai zao kwa wananchi na kuendeleza maslahi, mahitaji na matakwa yao binafsi.
  Kuna mambo kadhaa yanayostahili kuwekwa wazi mapema ili kufuatilia vizuri makala hii na zile zitakazofuatia. La kwanza ni kujua shahaba kuu ya kuanzishwa kwa Nyerere Foundation. La pili kujiuliza ni kwa nini mashambulizi haya yanazushwa sasa hivi. La tatu ni kujiuliza mashambulizi hayo yanamlenga nani hasa - Serikali, nchi ama kiongozi wa vyote viwili na mwisho ni kujiuliza nini hasa nia ya akina Butiku na wenzake. Nini kinawasukuma kuwa katika mstari wa mbele kabisa kuushambulia uongozi wa sasa wa Tanzania.
  Tuanze na la kwanza. Nyerere Foundation inazo shabaha kadhaa, lakini kubwa kuliko zote ni kwamba huu ni Mfuko ulioanzishwa kwa nia kuu ya kuendeleza yale makuu ambayo aliyaanzisha, akayasimamia na kuyaenzi Mwalimu wakati wa uhai wake wote, ndani ama nje ya madaraka ya uongozi.
  Na moja kubwa katika hayo ni nia ya dhati, iliyoungwa mkono na vitendo vya dhahiri kabisa ni jitihada zake kubwa kujenga Taifa la Tanzania, kuleta Umoja wa Tanzania, na kuhakikisha kuwa nchi hii inaendelea kuwa na utulivu na amani katika eneo la dunia ambako mambo hayo mawili ni tunu kubwa.
  Ni dhahiri kuwa kauli za akina Butiku zinavunja kabisa msingi huu mkubwa wa Mwalimu, na hivyo nia ya watoa kauli hizo, haiwezi kuwa wanalenga kumuenzi Mwalimu, bali ni kutumia jina lake vibaya tu, na kama kichocheo cha kuendeleza chuki na ajenda zao binafsi.
  Mashambulizi haya ya wakubwa hawa yasiyoisha dhidi ya uongozi wa sasa hayalengi kujenga taifa lenye Umoja, bali yanajaribu kubomoa Umoja wa Taifa letu kwa kuwarubuni wananchi waamini kuwa uongozi wa sasa siyo makini na haustahili kuwa madarakani. Ni aina ya hatari ambayo tumeishuhudia ikiziingiza nchi nyingi za Afrika katika zahama kubwa.
  Kauli hizi za uchochezi za akina Butiku, ikitokea zikasababisha vurugu, uvunjwaji wa amani na upotevu wa maisha na mali katika nchi, ni dhahiri kuwa katika dunia ya sasa, Butiku na wenzake wanahusika na kuwajibishwa moja kwa moja, siyo tu na vyombo vya Tanzania tu, bali hata vile vya kimataifa.
  Mfano halisi ni jirani zetu wa Kenya ambako viongozi waliohusika na machafuko, mauaji na upoteza wa maisha na mali baada ya Uchaguzi Mkuu wa Desemba 2007, sasa wanahaha kujinasua katika ndoani ya Mahakama ya Kimataifa ya Uharifu (ICC) na mwendeshaji wa mashitaka ya Mahakama hiyo, Bwana Luis Moreno Ocampo.
  Akina Butiku wanasahau hata sifa kuu za uongozi. Moja ya sifa kubwa ya kiongozi mzuri ni kujua nini la kusema na wakati gani. Kiongozi hawezi kuwa mropokaji, tena hadharani, juu ya mambo ambayo yangeweze kusemwa kwa busara zaidi kwa kuyaelekeza kwa wanaohusika moja kwa moja bila kutumia jukwaa la kisiasa. Na basi ni vyema mtu kuropoka ukijiaminisha kuwa mtu safi ambaye hana madoa makubwa na ya dhahiri kabisa katika uongozi.
  Hoja ya pili na ya tatu hapo juu zinaweza kujibiwa kwa pamoja na kwa maelezo mafupi. Mashambulizi haya yanazuka sasa kwa sababu wenye kuyaendesha wanahisi kuwa baada ya kuwa wamejaribu na kushindwa huko nyuma, sasa ndiyo wakati mwafaka wakati nchi inajiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwakani.
  Na kwa kweli hii ndiyo nafsi yao ya mwisho kujaribu kuwashawishi wananchi kwa propaganda zao dhaifu na zisizo kweli. Wanaamini kuwa propaganda hizo zikifanikiwa wanaweza kujaribu tena kumpamba na kumwingiza mgombea wao katika kinyanganyiro cha uchaguzi mkuu wa mwakani.
  Tatu ni kwamba mashambulizi ya sasa, hata kama waendeshaji mashambulizi hayo wanajificha vipi, yanamlenga moja kwa moja kiongozi wa sasa wa Serikali na taifa la Tanzania, yaani Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Haya siyo aina ya mashambulizi yanayomlenga mtu mwingine yoyote wa chini ya Rais.
  Mwisho ni kwa nini akina Butiku wanamlenga Rais Kikwete? Nini nia ya akiba Butiku na wenzake? Nini kinasukuma wazee hawa kumshambulia kijana ambaye walimlea wenyewe katika uongozi, kwa miaka mingi.
  Kubwa la kwanza ni kwamba tokea mwanzo, kundi hili la wazee halikumtaka Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Rais wa Tanzania. Na wala halijapata kumkubali ama hata kumsamehe Kiongozi huyo kwa kuweza kuwashinda wakati wa mchakato wa kuwania uongozi mwaka 2005.
  Na ndiyo maana zinajegwa hoja zinazodiriki kuhoji hata ni kwa namna gani aliingia madarakani, wakisahau kuwa ni wananchi wenyewe wa Tanzania katika hatua mbali mbali waliomwingiza Rais Kikwete madarakani, tena kwa kumwuunga mkono kwa wingi wa kushangaza sana.
  Na siyo tu kwamba aliwashinda kuweza kuingia madarakani. Lakini pia wanahisi kuwa kuwapo kwake madarakani kunafunga milango ya maslahi na matakwa yao kuweza kutumikiwa vizuri na utawala wake. Kwa namna nyingine pia wana hofu kuwa udhaifu wao na uongozi na uchafu wa baadhi yao walipokuwa madarakani unaweza kuanikwa hadharani.
  Hivyo, wanatumia janja tu ya jukwaa la kumuenzi Mwalimu Nyerere kujitafutia umaarufu binafsi na kutaka waenziwe wao. Na wako tayari kulifanya hili kwa gharama zote zote ikiwa ni pamoja na kutumia siri za vikao
  Ni sababu hiyo ya msingi ambayo siku zote imewasukuma viongozi hao kuushambulia moja kwa moja uongozi wake. Wamekuwa wanashindwa kumshambulia yeye moja kwa moja kwa jina na cheto chake kwa sababu wanaogopa hasira ya wananchi, lakini baada ya mashambulizi ya Kongamano la majuzi ni dhahiri kuwa sasa wanajiandaa kuianza kazi hiyo kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. Na wala wananchi wasije kushangazwa na hili.
  (Makala hii itaendelea)
  CHANZO: http://www.kwanzajamii.com
   
 2. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  i think mwandishi wa habari hii is biased and shallow minded..! mbona hasemi hao akina butiku walisema nn kuhusu kikwete..? anasema tu oooh wanaropoka..? tafsiri ya kuropoko is relative.!!!

  tuambie walisema nn ili tujue kama kweli waliropoka au la!

  stop spoon feeding us!!
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Dec 8, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  KUKOSOA HAINA MAANA KUWA watu hao hawapendi utawala wa JK ama laah, ni mfumo mzuri wa kuambiana ukweli hata kama unauma kwa kiasi gani.
  najua Raisi kakereka na maneno ya kina Butiku, ila ukweli ndo huo.
  hebu tizama hawa ni washauri wa JK katika mikakati yakisiasa, MAKAMBA,TABWE HIZA, hawa siasa kwao ni kazi ni ajira, hawawezi kumueleza lolote la kweli JK , WANAKAZI MOJA TU NAYO NI KUJIKOMBA.
  mwandishi nae kafuata mkono huohuo wa kina makamba na Hiza.
   
 4. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nia yao ni moja tu.
  VIONGOZI WABOVU WASIONGOZE TANZANIA
   
 5. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Maoni yangu yataendelea!
   
 6. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BUTIKU,QUARES,SLIM,WARIOBA,MANGULA na MIMI tuna nia njema ya kuwaondoa viongozi majangili waliopo kwenye system walau walala hoi nao wapate cha kuwawezesha kwenda haja.
  "mkapa kajenga uwanja wa kisasa na kikwete kaleta kocha wa kisasa....lol."
   
 7. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  na wao wezi tu, kama walikula lakini wamemaliza ndio wanakumbuka sasa kuwa mwenzao hafai, wao wameifanyia nini nchi hii kipindi walipokuwa madarakana?
   
 8. B

  Bobby JF-Expert Member

  #8
  Dec 8, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Nadhani hii nzuri sana. Huyu mwandishi anyway huenda hapaswi hata kujadiliwa maana IQ yake inaonekana kuwa ndogo sana. Kama vile akachekiwe kwanza Mirembe ndio tumjadili. Anadai hawa wazee wanatapata, wangetapapa rais wako asingehaingaika kutafuta majibu ya kuyajibu.
   
 9. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ukitaka kujua nia yao jadili/tafakari walichosema,acha kuwajadili wao,jadili hoja walizotoa
   
 10. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #10
  Dec 8, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mi nashangaa sana viongozi wetu wakikosolewa wanavyopaniki......!

  Kiongozi akikosolewa basi watu wanajaa jazba, hii tabia mbaya sana ni ya kidikteta. Umeomba uongozi mwenyewe, ukapata; sasa pale wengine wanapokosoa mwenendo wa uongozi wako ni wajibu wako kurekebisha yale ya msingi sio kushabikia tu kuwa kila unalofanya ni zuri.

  Pili watu hawawezi kukaa kimya kisa uongozi ni wa fulani, hii nchi ni yetu sote. Raia wa Tanzania ana haki ya kujadili mambo yanayohusu Tanzania ili mradi havunji sheria.

  Nakumbuka Cicero aliwahi kusema 'Let a man practise a proffession which he best know'. Sasa ukiangalia baadhi ya viongozi wetu kuna profession wanayoijua vizuri, badala yake wameacha/wamestaafu hiyo then wameingia kwenye siasa (mfano Lt. Makamba, Capt. Chiligati, Capt. Mkuchika........etc) sasa ndio wanaongoza kwa kuleta kauli za kidikteta.
   
 11. B

  Bobby JF-Expert Member

  #11
  Dec 8, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Gud this is very low mbona? Nadhani itakuwa ni busara sana tukijadili kile walichokisema badala ya kuwajadili wao waliosema. Naona umeuingia huu mtego moja kwa moja kama rais wako anayestahili pole kubwa. Badala ya kujibu hoja anazungumzia makundi, makundi ndio nini? Hatuko kwenye kampeni hapa. Hawa wazee kama waliiba nadhani si agenda, agenda ni kwamba uongozi wa awamu ya nne ni hopeless na unatudhalilisha kama nchi. Sasa nini cha kufanya ili kuondoka na hili tatizo ambalo hata Makamba (kama akili yake ina akili ) atakubaliana na hii fact?
   
 12. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #12
  Dec 8, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Kwani wewe uko wapi usiyeona mapungufu kibao ya utawala wa Kikwete? Sasa ulitaka useme wewe ndio tukusikie au nafikiri umesahau hao unaowasema ni public figure kwa hiyo wanalosema watu watalisikia na kulipima,kama NEC wanashindwa kusema na Bunge linabezwa unafikiri ni kitu gani kinafuata kama si kutoa mwanya kwa watu kutafuta sehemu zingine za kusemea na ndio maana hata sisi tunachonga hapa JF au sio bana
   
 13. B

  Bobby JF-Expert Member

  #13
  Dec 8, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Moderators hivi haiwezekani kuitoa hii kitu? Ningetamani yule ambaye hajaisoma aokoe muda kwa kutoisoma. Huyu mwandishi ninatilia shaka sana uwezo wa ubongo wake. Kwa maoni yangu inadhalilisha hata Jamii Forums kwa ujumla haipaswi kujadiliwa hapa for sure.
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mie nadhani wote hawafai na tukija kwa akina Butiku, SAS na Qares wao wenyewe sio wasafi wanadai kuwakosoa akina Kikwete je mie naswali moja Qares atueleze yeye uongozini alifanya kitu gani cha uadilifu kiasi kwamba anaweza kusimama anyooshe vidole wengine??? Butiku vile vile??? Salim atuambie lile jumba alilojenga masaki, Unguja na viwanda anavyomiliki hela ameipata wapi??? Msituhadae kama mna hidden ajenda zenu bwana???

  Nyerere alikuwa na guts za kunyooshea mtu kidole kwakuwa alifahamu madhara yake ndio maana hakuja kwake Butiama wala kusomesha mtoto wake nchi za nje tumesoma nao humo humo kwa akina mkia nyuma primary school. But Salim watoto anasomesha nje wanafanya kazi nje na achilia mbali ana viwanda anamiliki, Butiku pia, Qares, Sasa tuambie nyie uadilifu wenu ukoje????

  Unaponyoosha kidole mtu vidole vinne vinakuaangalia wewe. Watuambie wao uadilifu wao ukoje????
   
 15. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #15
  Dec 8, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi wee mwandishi wa hii habari ni mtanzania kweli? familia yako, wazazi wako, wapo tanzania kweli? Na je unatazamia wajukuu zako pia waishi Tanzania pia?
  Kama yote ni kweli! naomba nikushauri jambo do not live for today....itakugharimu wewe, familia yako na ukoo wako na taifa kwa ujumla!
  Inasikitisha kuona kuna mtu haoni matatizo tuliyo nayo! na hata kama wanaona basi kwa sababu wao na wake zao na watoto wao hawaathiriki basi wanataka sote tuone kuwa hakuna matatizo...
  kisiasa,kiuchumi...tupo pabaya hilo halipingiki na haijalishi nani kasema awe mkuu wa mkoa wa zamani, rais wa zamani .....ukweli unabaki kuwa rais lazima ashauriwe na aambiwe ukweli na kama ni mzalendo apime na atekeleze kwa manufaa ya taifa na sio kwa manufaa ya MNF
  Ukweli usipindwe kwa kuwageuzia watu kibano kuwa eti kwa sababu hawakuchaguliwa si kweli! kama wangesema uongo kuhusu hali iliyopo kweli tungesema hawa wana njaa zao....walichokisema kipo na kinaonekana hata wasio na ndoto ya kuwa mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya wanakiona

  Mimi nadhani wewe unataka ku provoke tu watu maaana ndio kazi zenu nyie mashushushu

  Nanyi mtaifahamu hiyo kweli nayo kweli itawaweka huru
   
 16. D

  Don Cicci Member

  #16
  Dec 8, 2009
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  you are right my brother huyu katumwa
   
 17. B

  Bobby JF-Expert Member

  #17
  Dec 8, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  So kwa kuwa Salim, Butiku na wengine uliowataja walichemsha au kuiba tuache Kikwete, RA, Lowasa na wengine waendelee kuimaliza hii nchi? Na watakaofuata nao itabidi waibe kwa kuwa hawa wa sasa wameiba? Wakati tukisubiri malaika washuke kuja kuokoa jahazi. Is this home of great thinkers au nimepotea njia jamani?
   
 18. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #18
  Dec 8, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Your arguiment is irrelevant
   
 19. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #19
  Dec 8, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Je waliyoyasema si ya kweli? Those are the point worth discussing.
   
Loading...