ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,030
- 3,907
Filamu ni moja kati ya zana bora sana ya kuelimisha na kuburidisha
Nafahamu kwamba wako waigizaji na watayarishaji wa filamu za kibongo wengi na wengine walishakufaga na walifanya kazi nzuri sana.
Pamoja na ukweli huo lakini bado naona kuna tatizo kubwa katika soko la filamu la Bongo.
Baadhi ya matatizo ninayoyaona ni kama haya

- Kukosekana kwa great stories;Filamu nyingi za kibongo zinakuwa na story dhaifu zisizokuwa na msisimko na mbali na hapo zinakuwa hazina uelekeo sahihi
- Tatizo la pili ni tatizo la Fedha,Financing..Soko la filamu limevamiwa na PIMPs ambao wanalenga zaidi kutumia sanaa hii katika maswala ya anasa zaidi na kupata mabinti wazuri
- Tatizo la tatu ni udhaifu wa Basata.Basata imeshindwa kabisa kuweka uwanja mzuri unaowezesha soko la filamu kukua na kuwezesha ulinzi wa kazi za sanaa.Wanatumia Muda mwingi kufungia kazi za sanaa kuliko kufuatilia na kuhamasisha wasanii wafanye kazi bora na zenye viwango
- PAmoja na wingi wa Media hapa Tanzania bado hakuna Media ambayo imeweza kuwekeza katika soko la Filamu.Bado ni ivgumu kwa Filamu kupata Airtime kwenye TV za kibongo
- Elimu nayo ni tatizo kwani wengi wanaojishughulisha na sanaa hawana hata elimu ya kuwaida ya kuweza kutambua masuala ya kawaida kabisa kama vile seting ya ujambazi ambapo kwa kawaida jambazi havui viatu akivamia.