Nini ni nini kati ya Tembo, Ndovu, meno ya Tembo, Pembe za Tembo?

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534
Jamani wanalugha, nina maswali kadhaa kuhusu mnyama huyu;

1. Vile vitu viwili vinavyochomoza kichwani kwake vinaitwa Pembe za Ndovu au Meno ya Tembo?
Yaani zile ni pembe au meno?

Na kutokana na hilo swali hapo juu napata swali lingine,
2. Je, neno Ndovu ni mbadala wa neno Tembo au ni maneno yenye maana tofauti?

Maana nishawahi kuona mahala neno Ndovu likitumika kumaanisha zile pembe (au meno) za mnyama Tembo.

Nawasilisha.
 
kisheria Nijuavyo mimi Pembe hukaa Juu ya Masikio ya myama juu ya kichwa lakini meno hukaa ndani ya mdomo au pembeni ya mdomo mfano Ngiri na jamii zake huyo Tembo Boko nk.
 
Zile ni pembe sio meno.
Na kazi Yake ni kumsaidia kuchimba chini ili kupata maji vilevile humsaidia kubandua magome ya miti kwa ajili ya chakula.kazi ingine ni ulinzi na kujihami.
Meno tembo anayo mawili ndani ya mdomo wake yaani juu moja chini moja ila limeanzia mwanzo hadi mwisho kuzunguka na si moja moja kama binadamu.
jina la ndovu limetokana na nguvu ya tembo na ukubwa mfano kuna watu wababe wanaitwa katapila au bulldoza.tofauti ya pembe na jino pembe huwa na tobo katikati(hollow)wakati jino huwa halina tobo katikati (mass)labda liwe bovu
 
Mbona hujauliza kwanini pembe za ndovu na faru tu na si za mbuzi au swala?yaani kwann iwe inauzwa bei juu na inatafutwa kimagendo
 
Zile sio pembe ni neno.
Its a long elongated canine,
Its not horns
Though people think that they are horns
They work as hands helping in digging saline water on the river bank,getting barks of trees used as weapons,and during sleeping
 
Lahaja ya Kimakunduchi, kimtangata na hata ki lamu neno Tembo lina maana ya uke. Hivyo sio neno jema kulitamka hadharani.

Lahaja ya kiunguja ambayo ndio lahaja sanifu ya lugha adhimu ya kiswahili neno pembe ni sahihi ila tembo humaanisha kilevi. Na ndovu ndiye huyo mnyama unayemzungumzia mwenye jmbo kubwa mwituni.

Hivyo basi kwa usahihi ni vyema kusema pembe za ndovu na mnyama mwenyewe huitwa ndovu.
 
Mh,aisee niliposoma post nilistuka kweli duhh
Maana neno TEMBO huku kwetu ni...............,mhhh
Alaa kumbe mnyama?nimeelewa baada ya kuona neno Ndovu
 
Yale ni meno siyo pembe,yamechomokea mdomoni mdomo Wa tembo uko chini ya mkonga,ni sawa na meno ya ngiri ni meno marefu,ya ngiri yamejikunja kwa juu ya tembo yamenyoooka
 
Hivi Tembo ana pembe au meno? Mimi siwaelewi waandishi wetu maana wengine wanasema PEMBE ZA NDOVU wengine MENO YA TEMBO.Halafu ni wakati gani anakuwa TEMBO au NDOVU? Mbaya zaidi kizungu chake ni TUSKS na wala sio TEETH ama HORNS.

straight-tusked-elephants.png


cc mshana jr
 
Subiri akina Mayalla wake wakusaidie.
Hivi tembo ana pembe au meno? Mimi siwaelewi waandishi wetu maana wengine wanasema PEMBE ZA NDOVU wengine MENO YA TEMBO......Halafu ni wakati gani anakuwa TEMBO au NDOVU? Mbaya zaidi kizungu chake ni TUSKS na wala sio TEETH ama HORNS!!!

straight-tusked-elephants.png


cc mshana jr
 
Back
Top Bottom