mazaga one
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 2,463
- 3,932
Mimi ni kijana wa kiume ambaye nipo kwenye mahusiano na binti wa kabila X. Binti anaupendo kwa kweli na anajua kupenda haswa ila changamoto iliyopo wazazi wangu kila nikikaa nao wananionya sana kuhusu hilo kabila na inatokea mara nyingine mzazi wangu ananipigia kelele nyingi akinisihi niachane na huyo binti wa kabila X.
Je, ndugu zangu wa humu ndani kuna mtu ambaye ashawahi kupitia changamoto kama hii?
Je, nini nguvu ya wazazi kukataa kuoa au kuolewa kwenye kabila fulani?
Naombeni msaada wenu na maoni yenu kwani nipo njia panda na binti wa watu naona kabisa nampotezea muda na sijaweza kumwambia chochote mpaka sasa na ananipenda sana ila kila nikifikiria maneno ya mzazi wangu nakuwa nachanganyikiwa. Najitahidi kumpotezea lakini binti hachoki kuwa karibu yangu kunitafuta na kunijali.
Naombeni msaada wenu wakuu.
Nawasilisha.