Nini na siri ya vyama vingine vya siasa kuwa dhaifu sana huku vingine vikiwa imara sana?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,503
2,046
Naomba wajuvi wa mambo wanisaidie kuelewa kwani kila nikitafakari kwa kina sipata jibu linaloniridhisha.
Hivi tofauti kubwa sana ya vyama vya siasa iko kwenye Nini?

1.Wanachama na viongozi kwa maana ya hulka za wanaokiunda chama!?
2.Muundo wa chama kwa maana ya jinsi chama kilivyoundwa.!?
3.Uwezo binafsi wa kiakili na kiuongozi wa wanaokiunda chama husika!?
4. Jina na alama mbalimbali za chama.!?
5. Historia na muda ambao chama kimedumu.?
6. Uwezo wa kifedha na kiuchumi ambao chama kinao.?
7. Mazingira ya kisiasa ambayo taifa linapitia?

Lengo la mjadala huu ni kujaribu kutoa mwangaza wa kisiasa kwa viongozi wetu wa vyama ili wafanye maboresho kwenye vyama vyetu ili tuwe na vyama imara sana kwa maslahi ya taifa letu.
 
Ukiachilia mbali ilani ya hivyo vyama, lakini viongozi kuwa na misimamo isiyoyumba ni jambo la msingi sana, sio kusema kisa leo tuna Rais mwanamke basi wabadilishe approach yao, huu ni udhaifu, chama imara kinaundwa na viongozi imara wenye kuijua vision ya kile wanachokitaka na namna ya kuipigania ili kuipata bila kujali ikulu kuna jinsia gani.
 
Ulizoorodhesha hapo no sababu, lakini nyingine ni tabia ya vyama vingine kujikita ktk kuzungumzia masuala ya vyama vingine yasiyowahusu, huku vikisahau kujiimarisha kwa ajili ya kushinda uchaguzi.
 
Back
Top Bottom