Nini mtazamo wako kuhusu Clouds FM kuiga ubunifu wa E-FM?

Sultan Kipingo

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
236
175
E fm ni kituo cha radio ambacho hakina muda mrefu tangu kianzishwe lakini kimejipatia umaarufu mkubwa Jijini Dar es Salaam na Pwani kutokana na ubunifu ktk utoaji wa matangazo yao na swaga za watangazaji wake mahiri ktk vipindi vyao ambao baadhi yao wametoka clouds fm.

Pamoja na uchanga wa kituo hicho (E fm), kituo kingine ambacho ni kikubwa nchini ambacho kinasikika karibu nchi nzima kwa masafa ya fm na Duniani kote kupitia mtandao kimekuwa kikiiga ubunifu wa radio E fm na kufanya kama vile ni ubunifu wao.

Mifano ya vitu vilivyoigwa na clouds fm ambavyo awali vilifanywa na Efm ni pamoja na kufanya kipindi nje ya studio. Efm wana kitu kinaitwa Nje ndani naona Clouds fm nao wameiga hiyo kwa kufanya kipindi cha leo cha sports Xtra huko Tandale.

Mbali na hilo Efm waliwahi kuandaa tamasha la waendesha bodaboda na bajaji kule kijitonyama, lakn baada ya tangazo la E fm clouds kupitia radio ya choice fm waliibuka na tangazo lao lenye tarehe hiyohiyo kufanya tamasha la walaji chips huko mbagala.

Baada ya matamasha haya Efm kwa kutumia Jingo ya Wimbo wa Mwana FA "Ahsanteni kwa kuja" waliwashukuru wote waliofika kwenye tamasha lao pale kijitonyama jambo lisilo la kawaida kwa kutumia jingo hiyohiyo choice fm (clouds media) walitumia kuwashukuru waliohudhuria tamasha lao pia.

Clouds media kupitia radio zake walikuwa hawawathamini kabisa wasanii wa singeli lakn baada ya E fm kuufanya aina hiyo ya mziki kama ndo mziki rasmi wa kituo hicho, clouds media kupitia Choice wameanza kupiga singeli na wameenda mbali hadi kuwajumuisha wasanii hao wa singeli kwenye matamasha yao llikiwemo tamasha lao kubwa la fiesta.

Kingine Efm walikuwa na kitu kinaitwa kapu la sikukuu, ambapo wanapiga jingo ktk kipindi fulani halafu wasanii wanapiga simu wakipatia muda jingo ilipopigwa na kipindi husika na watangazaji basi wanajishindia hilo kapu Clouds nao wakaja na kitu kinacgofanana na hiki (sikumbuki jina lake) ila nakumbuka walikua wanataja namba ww unatakiwa useme hizo namba zilitajwa kipindi gani, muda gani na watangazaji walikuwa akina nani.

Mimi naona kwa uigaji huu, clouds inajipotezea umaarufu pia inapoteza wasikilizaji. Na hilo linajidhirisha hapa mjini ukitembea mitaani ni E fm sehemu nyingi ukilinganisha na siku za nyuma.

Sasa sijui Efm ikisambaa mikoani itakuaje. Efm walikuwa na kitu inaitwa Sakasaka, Shika ndinga na sasa hivi wameanzisha Efm Jogging Club Ninawasiwasi Clouds huenda wako mbioni kuiga.

Efm wana msemo wao "Huu mchezo hauhitaji hasira". Nilishangaa siku nikausikia huu msemo kwa Kipanya wa Power Breakfast.

Nini mtazamo wako juu ya hii kitu.?
 
Hiyo Ni kawaida kwa Wtz wengi akiwa peke yake anakimbiza anakuwa jeuri na dharau hataki kusikiliza maoni na kuwa mbunifu kutokana na taste za wateja wake.

Akitokea mpinzani hlf akaboresha Huduma basi huyo mtangulizi anakuwa mtumwa WA mpinzani wake ataiga kila kitu hata cha kipuuzi kwa sababu anakuwa amechsnganyikiwa na ajili haifanyi kazi vizuri.
 
Mbona clouds fm walishapoteza muelekeo zamani tu?
 
Hiyo Ni kawaida kwa Wtz wengi akiwa peke yake anakimbiza anakuwa jeuri na dharau hataki kusikiliza maoni na kuwa mbunifu kutokana na taste za wateja wake.

Akitokea mpinzani hlf akaboresha Huduma basi huyo mtangulizi anakuwa mtumwa WA mpinzani wake ataiga kila kitu hata cha kipuuzi kwa sababu anakuwa amechsnganyikiwa na ajili haifanyi kazi vizuri.
Mkuu kwa sasa Efm wapo juu huwezi kuwalinganisha na hao clouds
 
Clouds sjuh wamekuwaje. Sjuh kipi kilichowatokea. Nawaambia siku E-fm wakianza kusikika hata mikoa 8 tu Tanzania basi Clouds wajiandae kisawasawa. Ila E-fm wasipolewa sifa na wakaanza kusikika angalau mikoa 8 tu, clouds wanaenda kufifia kabsa.

E-fm wananifurahisha na huu msemo "Sisi tunaanza kukopi na kupesti inakuhusu".
 
Clouds ilikuwa zamani, saiv haina kitu ikibid iuze masafa au ibadirishe jina la kitu. Mwanzo waliwaonea sana timesfm, timesfm walipo anza kutangaxa mziki wa naijeria clouds wakadaki.. Efm na kisengeli na pale wakadakia il waonekane wao ndo wanausapot huo mziki. Ila kwa bahati mbaya wamechemka.
 
Tangu waanze kuhoji Mashoga kwenye kituo chao cha Clouds TV walizidi kuporomoka maradufu,na nyie E fm msije iga huo upuuzi.
Hilo la kuhoji mashoga ni sababu mojawapo ya kukosa wasikilizaji na watazamaji. Wengi hawajafurahishwa na kile kipindi na wao Clouds wanaona kama hawajakosea, kikubwa na cha kushangaza hawajaomba radhi kama TCRA ilivyowaagiza.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom