Nini Mtazamo wa Jamii kuhusu Magenge ya Kialifu kama "Panya Road"

Mahoma

Member
Jan 27, 2012
20
0
Hodi wana Jamvi na watanzania wenzangu,
Imelanilazimu kandika humu ili kutoa mtazamo wangu kuhusu yanatokea katika jamii yetu hasa kuhusiana na uhalifu na wahalifu panya road wakiwa ni sehemu tu wengi au ya makundi ya jinsi hiyo.

Nakiri kuwa sina uelewa mpana sana wa mambo ya kiinteligensia na pengine sihitaji hilo kutambua kuwa wahalifu hawa wanatoka katika familia zetu au jamii yetu.

Ni jambo la kusikitisha mno tunapofikiri aidha tuko sisi ama mali zetu ziko salama kwa kujiangalia kwa ubinafsi na kushindwa kuangalia kwa upana athari za kijamii,kiuchumi,na hata kiroho zitokanazo na hali hii.
Mara nyingi tumekuwa na matazamo kuwa usalama wetu uko mikononi mwa vyombo vya usalama.Ningependa kila mtu ajiulize je nani amewahi kwenda polisi kutoa taarifa kuwa mwanawe,ndugu yake au jairani yake anajihusisha na vitendo vya kihalifu? Ploisi anahusishwa tu tukio linapokuwa limetendeka na pengine hata hapewi ushirikiano wa kutosha.Hebu tujiulize maswali machache tukitumia panya road kama kundi wakilishi.

Maswali ya Kujiuliza
1.Hawa panya road ni watanzania wenzetu?

2.Wanatoka familia zipi(malezi yao yakil,makuzi yao,walipewa fursa za msingi kama elimu nk)?

3.Kwanini wamechagua mfumo huo wa maisha?

4.Jamii inawatambua na kuwachukuliaje(je tunawaona kama nguvu kazi iliyokosa kuelekezwa na kushirikishwa katika mambo ya msingi na hasa ya kiuchumi)?

5.Je tuna mpango wowote wa kuwasaidia hao walioathirika na kujijenga katika makundi kihalifu kwa kuweka mipango shirikishi ya kiuzalishaji mfano kilimo cha vikundi sehemu mbalimabli.

6.Je inawezekana hawa vijana kufundishwa na jeshi la kujenga taifa uzalishaji mali bila kupewa mbina na mafunzo ya kivita (kama tahadhari)?

7.Jamii inaweza kurejea wajibu wake wa kukosoa, kufundisha na kuadhibu kama ilivyokuw huko nyuma kwamba motto ni wa jamii hivyo akikosea anaweza kuadhiwa kihalali na jamii?

Mwisho, japo nina mengi kama ushauri, lakina niombe tu tuchangie hoja hii kwa mtazamo chanya wa kujenga nchi bora ambayo tunajivunia amani tuliyopewa na Mungu,na tunapaswa kuilinda kwa kumweshimu na kumhofu Mungu. Hakuna aliye salama kama tutaruhusu hali hii iendelee maana si kila mtu atakuwa na uwezo wa kuweka walinzi binafsi wa kunlinda yeye na mali zake,lazima jamii nzima tushirikiane.
 

Mayunga96

Member
Oct 11, 2013
73
0
hodi wana jamvi na watanzania wenzangu,
imelanilazimu kandika humu ili kutoa mtazamo wangu kuhusu yanatokea katika jamii yetu hasa kuhusiana na uhalifu na wahalifu panya road wakiwa ni sehemu tu wengi au ya makundi ya jinsi hiyo.

Nakiri kuwa sina uelewa mpana sana wa mambo ya kiinteligensia na pengine sihitaji hilo kutambua kuwa wahalifu hawa wanatoka katika familia zetu au jamii yetu.

Ni jambo la kusikitisha mno tunapofikiri aidha tuko sisi ama mali zetu ziko salama kwa kujiangalia kwa ubinafsi na kushindwa kuangalia kwa upana athari za kijamii,kiuchumi,na hata kiroho zitokanazo na hali hii.
Mara nyingi tumekuwa na matazamo kuwa usalama wetu uko mikononi mwa vyombo vya usalama.ningependa kila mtu ajiulize je nani amewahi kwenda polisi kutoa taarifa kuwa mwanawe,ndugu yake au jairani yake anajihusisha na vitendo vya kihalifu? Ploisi anahusishwa tu tukio linapokuwa limetendeka na pengine hata hapewi ushirikiano wa kutosha.hebu tujiulize maswali machache tukitumia panya road kama kundi wakilishi.

Maswali ya kujiuliza
1.hawa panya road ni watanzania wenzetu?

2.wanatoka familia zipi(malezi yao yakil,makuzi yao,walipewa fursa za msingi kama elimu nk)?

3.kwanini wamechagua mfumo huo wa maisha?

4.jamii inawatambua na kuwachukuliaje(je tunawaona kama nguvu kazi iliyokosa kuelekezwa na kushirikishwa katika mambo ya msingi na hasa ya kiuchumi)?

5.je tuna mpango wowote wa kuwasaidia hao walioathirika na kujijenga katika makundi kihalifu kwa kuweka mipango shirikishi ya kiuzalishaji mfano kilimo cha vikundi sehemu mbalimabli.

6.je inawezekana hawa vijana kufundishwa na jeshi la kujenga taifa uzalishaji mali bila kupewa mbina na mafunzo ya kivita (kama tahadhari)?

7.jamii inaweza kurejea wajibu wake wa kukosoa, kufundisha na kuadhibu kama ilivyokuw huko nyuma kwamba motto ni wa jamii hivyo akikosea anaweza kuadhiwa kihalali na jamii?

Mwisho, japo nina mengi kama ushauri, lakina niombe tu tuchangie hoja hii kwa mtazamo chanya wa kujenga nchi bora ambayo tunajivunia amani tuliyopewa na mungu,na tunapaswa kuilinda kwa kumweshimu na kumhofu mungu. Hakuna aliye salama kama tutaruhusu hali hii iendelee maana si kila mtu atakuwa na uwezo wa kuweka walinzi binafsi wa kunlinda yeye na mali zake,lazima jamii nzima tushirikiane.


mambo ya msingi kama haya watu huwa hawachangii yani daah!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom