Mdokezi2
Member
- Apr 4, 2014
- 70
- 5
Kwa kipindi chote ambacho nimekuwa nikifuatilia vikao vya BMK nimepata mashaka-tena makubwa-juu ya mapendekezo ya Zanzibar juu ya msimamo wao kuhusu muundo wa serikali. Wajumbe walio wengi wanawasilisha kwamba Zanzibar kupitia baraza la wawakilishi lilituma mapendekezo yao juu ya muundo wa serikali kuwa ni serikali tatu. Lakini katika vikao vinavyoendelea hapa Dodoma mawazo ya walio wengi kutoka zanzibar ni serikali mbili!!!! Kama kuna mwenye kujua zaidi tufahamishane hapa!!!