Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,797
- 71,215
Chama changu kilitumia nguvu nyingi kumtetea na kumnadi msanii Wema na wengine ikiaminika kuwa wanaweza kutumia fursa ya umaarufu wao katika sanaa kuvuta hisia kwa wengine wakati kama huu makamanda wanapo pambana huko field.
Lakini kwa muono wangu hakuna faida yeyote tuliyopata au tupatayo ukilinganisha na nguvu kubwa iliyotumika kumpokea, kumtetea na hata kumpa nafasi kama mtu wa msaada kwa chama.
Imagine matukio kama haya ya mawakala kupigwa mapanga na nondo na kuumizwa, mtu kama Wema angeposti katika ukurasa wake kuonyesha kusikitishwa nayo jamii ingepokeaje swala hilo? Hata vijana washabiki wake wangeguswa na kujenga taswira mpya ya kuelewa nini kinaendelea.
Sasa tokea kampeni za udiwani zimeanza hadi mabaya haya yanatokea yeye hana habari kabisa na hayamhusu. Lakini utetezi wa maonevu aliokuwa anafanyiwa ndio anaona chama kinamhusu, huu ni ujinga usio vumika kabisa. Nadhani kama chama kitengo cha uenezi tuwe na la kujifunza hapa.
Kama mtu haumizwi na ile damu ya wana Chadema inayomwagwa kwa maumivu makali basi hastahili kuitwa mwenzetu na akae mbali nasi au arudi alikotoka.