Nini Mchango wa Msanii Kama Wema Wakati wa Harakati kama za Leo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini Mchango wa Msanii Kama Wema Wakati wa Harakati kama za Leo?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Chakaza, Nov 26, 2017.

 1. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2017
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 25,488
  Likes Received: 26,386
  Trophy Points: 280
  Chama changu kilitumia nguvu nyingi kumtetea na kumnadi msanii Wema na wengine ikiaminika kuwa wanaweza kutumia fursa ya umaarufu wao katika sanaa kuvuta hisia kwa wengine wakati kama huu makamanda wanapo pambana huko field.
  Lakini kwa muono wangu hakuna faida yeyote tuliyopata au tupatayo ukilinganisha na nguvu kubwa iliyotumika kumpokea, kumtetea na hata kumpa nafasi kama mtu wa msaada kwa chama.
  Imagine matukio kama haya ya mawakala kupigwa mapanga na nondo na kuumizwa, mtu kama Wema angeposti katika ukurasa wake kuonyesha kusikitishwa nayo jamii ingepokeaje swala hilo? Hata vijana washabiki wake wangeguswa na kujenga taswira mpya ya kuelewa nini kinaendelea.
  Sasa tokea kampeni za udiwani zimeanza hadi mabaya haya yanatokea yeye hana habari kabisa na hayamhusu. Lakini utetezi wa maonevu aliokuwa anafanyiwa ndio anaona chama kinamhusu, huu ni ujinga usio vumika kabisa. Nadhani kama chama kitengo cha uenezi tuwe na la kujifunza hapa.
  Kama mtu haumizwi na ile damu ya wana Chadema inayomwagwa kwa maumivu makali basi hastahili kuitwa mwenzetu na akae mbali nasi au arudi alikotoka.
   
 2. Z

  Zygot JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2017
  Joined: Apr 14, 2016
  Messages: 335
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 80
  We unawaza hata waigizaji! Hawa ni wale wanaoigiza umaarufu, wanaigiza kuzungumza, wanaigiza ufahamu, kutembea, nk. hata siasa wanaigiza
   
 3. n

  ndayilagije JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2017
  Joined: Nov 7, 2016
  Messages: 5,898
  Likes Received: 5,997
  Trophy Points: 280
  Amepost mwenyekiti wa Simiyu CCM akiwa amelazwa mbona.
   
 4. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2017
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,701
  Likes Received: 9,812
  Trophy Points: 280
  Usichokijua ni kwamba huyo Wema tayari yupo mbioni kurejea CCM.
  Mlikua hamjui kwamba ni rahisi sana kumtongoza au kumgonga mwanamke aliyegombana na bwana ake? Mlipaswa kujipigia tu na kupita zenu kando, sasa nyie mtu mihasira yake mnampa mapokezi na kutangaza ndoa. Hasira Zikipoa lazima arudi kwa bwana ake tena huku akiomba msamaha na kutembea kwa magoti
   
 5. Moisemusajiografii

  Moisemusajiografii JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2017
  Joined: Nov 3, 2013
  Messages: 8,347
  Likes Received: 6,580
  Trophy Points: 280
  Muwe mnajifunza kuchangia hoja kwa hoja. Sasa hicho ulichoandika maana yake nini? Ndiyo maana huwa mnajibiwa kwa maneno makali halafu mnavimbisha mashavu. Grow uuuuuuuuuuuup!!!!!!
   
 6. tindo

  tindo JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2017
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 11,946
  Likes Received: 13,429
  Trophy Points: 280
  Mkuu Chakaza nikiwashambulia viongozi wa cdm hapa jukwaani kuhusu huo udhaifu wa kupokea wanaccm na kuwapa nafasi kubwa chamani naona kama baadhi ya makamanda hawanielewi. Sasa wangalau naona wewe mwenzangu umeanza kuchukua hatua. Tulipiga kelele sana kuhusu Shibuda tukajiapiza kwa kosa lile, nilidhani kama chama tulijifunza. Uchaguzi wa 2015 ndio tukafanya kosa la kipuuzi kuliko yote unayoyajua wewe kama chama. Huyu Wema saa hii ni kama kumuonea tu. Viongozi wa cdm wajitokeze watupe mchango wake na akiana Masha waliowapa nafasi ya kugombea ubunge wa EALA.
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Nov 26, 2017
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 13,577
  Likes Received: 6,712
  Trophy Points: 280
  ..msianze kulaumiana.

  ..tena wakati mnapitia wakati mgumu kama huu.
   
 8. tindo

  tindo JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2017
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 11,946
  Likes Received: 13,429
  Trophy Points: 280
  Mkuu Chakaza nikiwashambulia viongozi wa cdm hapa jukwaani kuhusu huo udhaifu wa kupokea wanaccm na kuwapa nafasi kubwa chamani naona kama baadhi ya makamanda hawanielewi. Sasa wangalau naona wewe mwenzangu umeanza kuchukua hatua. Tulipiga kelele sana kuhusu Shibuda tukajiapiza kwa kosa lile, nilidhani kama chama tulijifunza. Uchaguzi wa 2015 ndio tukafanya kosa la kipuuzi kuliko yote unayoyajua wewe kama chama. Huyu Wema saa hii ni kama kumuonea tu. Viongozi wa cdm wajitokeze watupe mchango wake na akiana Masha waliowapa nafasi ya kugombea ubunge wa EALA.
   
 9. tindo

  tindo JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2017
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 11,946
  Likes Received: 13,429
  Trophy Points: 280
  Mkuu wakati mgumu inaokutana nao cdm ni kama umesababishwa na viongozi. Angalia post yangu namba 9.
   
 10. Mwanzambaya

  Mwanzambaya JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2017
  Joined: Jul 27, 2016
  Messages: 875
  Likes Received: 834
  Trophy Points: 180
  Kweli kabisa mkuu,,,Hawa watu wengine sio wakuwapokea kwa mbwembwe kwenye chama,,hawana faida yoyote,,,na usije kushangaa ikikaribia uchaguzi mkuu ataomba nayeye eti apewe chance ya kugombea ubunge
   
 11. Crimea

  Crimea JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2017
  Joined: Mar 25, 2014
  Messages: 4,815
  Likes Received: 3,516
  Trophy Points: 280
  Chadema ya sasa ni kama changudoa!

  Mnatongozeka kirahisi mno!

  Mbaya zaidi unatongoza changudoa alafu unamkabidhi hadi ufunguo wa nyumba?
   
 12. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2017
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,455
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Kama mmeanza kupata ujasiri wa kohoji, chama kinaweza kurudi kwenye mstari come 2025.
   
 13. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #13
  Nov 26, 2017
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 25,488
  Likes Received: 26,386
  Trophy Points: 280
  Mkuu JokaKuu sio kulaumiana ni kuambiana ukweli. Na nadhani muhusika mwenyewe kwa vile anaweza kusoma hapa basi ni vema alitambue na kuchukua hatua. Inaumiza sana, chama sio kanisa au msikiti, kila kifanyacho lazima kiwe na faida kwake
   
 14. xav bero

  xav bero JF-Expert Member

  #14
  Nov 26, 2017
  Joined: Nov 24, 2016
  Messages: 4,885
  Likes Received: 6,316
  Trophy Points: 280
  Ukiwa msanii na kada wa chama cha ccm ukaondoka kwa nyodo utakuja kujuta baadae maana mbinu zote saf na chafu wanazijua,ss mnamtegemea wema atawapa impact gan ktk chama zaid ya uwema wake??
   
 15. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #15
  Nov 26, 2017
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 25,488
  Likes Received: 26,386
  Trophy Points: 280
  Umeingia kwenye mjadala usiokufaa. Hapa tunaangalia uwajibikaji wetu ndani ya Chadema hivyo mchango wako hauna faida hapa
   
 16. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2017
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 19,510
  Likes Received: 12,759
  Trophy Points: 280
  Siku mtakayojua kuwa Mbowe ndio tatizo ndani ya Chadema.....ndio siku ambayo Chadema itazaliwa upya.
   
 17. Crimea

  Crimea JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2017
  Joined: Mar 25, 2014
  Messages: 4,815
  Likes Received: 3,516
  Trophy Points: 280
  Mkuu.. Nikulize ulitakafakari kabla ya kushangilia ujio wa Wema?

  Nikulize tena faida ya Nyalandu umeitakafakari pia?
   
 18. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #18
  Nov 26, 2017
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,701
  Likes Received: 9,812
  Trophy Points: 280
  Mbowe anaweza kuwa ni kiongozi mzuri lakini si mwamikakati. Katika kipindi hiki ambacho hata CCM tuna changamoto kubwa kuliko wakati wowote ule inashangaza kuona chama kama Chadema ni kama hakipo vile. Kipindi cha Dr. Slaa CHADEMA ilikuwa na mvuto wa kipekee sana lakini CHADEMA ya hivi sasa inashangilia mtu kutoka CCM na kujiunga nao. Enzi zile mwana CCM angeweza kujiunga na isiwe habari kabisa na ndiyo maana mwana mikakati Dr. Slaa aliwashauri mumpokee Lowasa, ahojiwe kuhusu tuhuma zake lakini abaki kama mwanachama wa kawaida na asipewe nafasi ya Kugombea.
  Lakini Mheshimiwa Mbowe na mahesabu na maono ya kichaga akaona it's now or never. Akautupilia mbali ushauri wa Dr. Slaa na kumkubalia Lowasa kila alichokitaka ikiwemo nafasi mbali mbali kwa watu anaokwenda nao humo CHADEMA. Hata mke wake akazawadiwa ubunge wa viti maalum sema akaukataa. Kwa mseto huo bado mnataka mniambie kuna CHADEMA hapo? Acheni masikhara, njooni CCM tusaidiane kumpinga magufuli kutokea ndani .
   
 19. W

  Wakudadavuwa JF-Expert Member

  #19
  Nov 26, 2017
  Joined: Feb 17, 2016
  Messages: 9,946
  Likes Received: 8,475
  Trophy Points: 280
  Mbowe ni kada mtiifu wa CCM
   
 20. J

  JokaKuu Platinum Member

  #20
  Nov 26, 2017
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 13,577
  Likes Received: 6,712
  Trophy Points: 280
  ..mbona ccm walimtumia vizuri?

  ..nini kifanyike ili ujio wake uwe na faida kwa chama?

  ..tukubali kuwa cdm inapigwa mabao ktk level zote.

  ..sasa collectively watu inabidi warudi kwenye drawing board na kupanga mbinu na mikakati mipya.

  ..hakuna mwenye afadhali cdm sasa hivi.

  ..everybody sucks.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...