Nini maudhui hasa ndani ya Lady Jaydee Diary?

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,450
487
Wana Jamvi habari za asubuhi.
Leo katika jamvi letu hili nimeonelea tuongelee na kuchambua kwa undani maudhui yaliyoonekana katika kipindi kipya cha Lady Jaydee Diary hapo jana katika kituo cha channel 5. Mara nyingi kwa watu wanopenda kufuatilia documentaries zinazoelezea maisha ya watu mbali mbali, huwa aidha, mhusika mwenyewe au msimamizi wa kipindi hicho hujitahidi kuingia kwa undani wa kueleza mwanzo-mwisho wa mtu au kitu husika.
Katika kipindi cha mwanamuziki wetu huyo, binafsi baada ya kukiangalia kwa kina, kilichojidhihilisha ndani yake ni kutengeneza uonekano wake mbele ya kamera kuliko kueleza ni kitu gani amekifanya/kupitia ili jamii iweze kujifunza toka kwake na waweze kufika pale alipo au kufanikiwa kama yeye. Nina imani kwa yule aliyebahatika kukiona hicho hapo jana anaweza kusaidia kutoa mchango wake wa mawazo ili mara nyingine mhusika ajue ni mapungufu yepi yaliyojitokeza katika documentary yake.
Nawasilisha jamvini.
 
Yeye mwenyewe alisema anataka watu wamfahamu zaidi,hivyo endelea kukifuatiia kuangalia picha zake labda kuna kitu utajifunza toka kwake na kumuelewa zaidi.
 
Yeye mwenyewe alisema anataka watu wamfahamu zaidi,hivyo endelea kukifuatiia kuangalia picha zake labda kuna kitu utajifunza toka kwake na kumuelewa zaidi.

Wamfahamu vizr tena!?kwenye wimbo wake wa 'siku hazigandi',alisema,'kunijua sana undani siwapi tena nafasi'
....wasanii wabongo banaaaa
 
Wanajaribu kufanya reality show kama zile za kina kim kardasian.
Chid benz alijaribu kufanya chake ila kila siku alikua anaamka geto kwake na kupitia dukani kununua sigara, akitoka hapo anaenda studio anarekodi nyimbo moja anatoka studio anapita bar anakunywa viroba kadhaa, anatoka bar anaenda maskani anapiga story na washkaji zake anatoka hapo anaenda kufanya shopping ya t.shirt moja anarudi kwake na kipindi kinaisha.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Namuheshimu sana Judith Wambura Habash kwa bidii yake,amefanya vizuri kuwa na kipindi chake lakini hajaanza vizuri kwakweli. Nadhani maudhui ya kipindi ni mambo halisi lakini sehemu kubwa wanaigiza kuliko uhalisia,mfano pale alipokuwa anamuamsha Habash namna jamaa alivyokuwa anaamshwa na jinsi alivyokuwa anaitika ni full maigizo.

Nafikiri wajifunze zaidi namna ya kutengeneza vipindi halisi na ikibidi kwa kutega kamera sehemu husika bila kujulishwa (isiwe kwenye mambo private sana labda wapende).

Asiwe kama mtu aliyejiandaa kurekodiwa hasa akitaka kutuonyesha uhalisia mfano Habash alivyokuwa amevaa akiwa amelala kwa mazingira ya Dar hata kama unatumia A/C huwezi kulala na nguo namna ile (labda!)

Anyway,inawezekana anachofanya ndivyo anavyotaka lakini awe yeye zaidi na watu wa kamera wawe wanamvizia kwenye matukio ambayo hayajapangwa pia!
 
Hivi huyo bibi ana watoto wangapi? grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr wajukuu wangapi? umri wake vip?:shut-mouth:
 
kwa kifupi hakijanifutia kabisa camera inashake hadi nasikia kizungu zungu af sio reality kabisa
 
Back
Top Bottom