Miwatamu
JF-Expert Member
- Oct 2, 2012
- 1,450
- 487
Wana Jamvi habari za asubuhi.
Leo katika jamvi letu hili nimeonelea tuongelee na kuchambua kwa undani maudhui yaliyoonekana katika kipindi kipya cha Lady Jaydee Diary hapo jana katika kituo cha channel 5. Mara nyingi kwa watu wanopenda kufuatilia documentaries zinazoelezea maisha ya watu mbali mbali, huwa aidha, mhusika mwenyewe au msimamizi wa kipindi hicho hujitahidi kuingia kwa undani wa kueleza mwanzo-mwisho wa mtu au kitu husika.
Katika kipindi cha mwanamuziki wetu huyo, binafsi baada ya kukiangalia kwa kina, kilichojidhihilisha ndani yake ni kutengeneza uonekano wake mbele ya kamera kuliko kueleza ni kitu gani amekifanya/kupitia ili jamii iweze kujifunza toka kwake na waweze kufika pale alipo au kufanikiwa kama yeye. Nina imani kwa yule aliyebahatika kukiona hicho hapo jana anaweza kusaidia kutoa mchango wake wa mawazo ili mara nyingine mhusika ajue ni mapungufu yepi yaliyojitokeza katika documentary yake.
Nawasilisha jamvini.