Nini matumizi ya Mabondo ya Samaki Sangara?

Nimeupenda bure huu uzi,naomba kujua hiyo biashara ya mabondo inafanyikaje?mfano nikinunua samaki ya grade ya chini kabisa wa sh.milioni 1 naweza kupata faida kiasi gani kwa kadirio la chini?
Hapo kunasamaki na mabondo. Umesema samaki wa grade ya chini kabisa wa milion inamaana wale samake wawe na urefu wa under 50cm ambao watakuwa hawaendi kiwandani. Hao kimamlaka wanahesabika kama mboga ya taifa hawapo kwa ajiri ya kuchakatwa na kuuzwa nje.

Sasa katika hawa samaki itatokana na soko uñakowapeleka, ukusanyaji na uhifadhi pamoja na usafirishaji na gharama zake ndo tujue utapata kiasi gani. Kuhusu mabondo ya samaki hawa bondo lake hucheza kati ya gram 25 to gram 29 kwa kila bondo. Hapo nisamaki wa cm 46 to 49. Sasa mfano bei inayocheza mara nyingi ni tsh 100 kwa gram kwa mabondo ya samaki wa size hii. Hivyo sasa wewe tafuta yule samaki aliyetolewa bondo utamuuza sh ngapi kwa soko lako kisha njoo ununue hao samaki huku kerebe bukoba kwa sh 4000 to 5000 kwa kila samaki wa aina hiyo
 
Huwa yanatengeneza zile nyuzi za operesheni ambazo ni quality.Ukishafanyiwa opereheni na nyuzi hizo haina haja ya kurejea kuzitoa.
Hii inshu ishanipa wakati mgumu kama kweli yanatengeneza nyuzi ama lah. Bei ya mabondo inaanzia tsh 100 mpaka tsh 2000. Kwa gram. Inamaana kuna kilo ya mabondo inauzwa laki na kuna kilo ya mabondo inauzwa milion 2 nazote nikilo. Sasa najiuliza. Nikweli nyuzi za kushonea binadamu zinamadaraja mengi kiasi hicho. Kama lengo ni gafi. Kwanini thamani iangalie ukubwa nasi ubora wa kitu. Nikweli bondo jinsi linavyokuwa kubwa ndo linavyozidi kuwa bora
 
Hapo kunasamaki na mabondo. Umesema samaki wa grade ya chini kabisa wa milion inamaana wale samake wawe na urefu wa under 50cm ambao watakuwa hawaendi kiwandani. Hao kimamlaka wanahesabika kama mboga ya taifa hawapo kwa ajiri ya kuchakatwa na kuuzwa nje.

Sasa katika hawa samaki itatokana na soko uñakowapeleka, ukusanyaji na uhifadhi pamoja na usafirishaji na gharama zake ndo tujue utapata kiasi gani. Kuhusu mabondo ya samaki hawa bondo lake hucheza kati ya gram 25 to gram 29 kwa kila bondo. Hapo nisamaki wa cm 46 to 49. Sasa mfano bei inayocheza mara nyingi ni tsh 100 kwa gram kwa mabondo ya samaki wa size hii. Hivyo sasa wewe tafuta yule samaki aliyetolewa bondo utamuuza sh ngapi kwa soko lako kisha njoo ununue hao samaki huku kerebe bukoba kwa sh 4000 to 5000 kwa kila samaki wa aina hiyo
mkuu ahsante kwa majibu yako mazuri,mimi lengo langu hasa ni kufanya biashara ya MABONDO na sio samaki,ila samaki ni kama bonus tu.Naomba ufafanuzi upande wa biashara ya mabondo inafanyikaje ili angalau iwe na matokeo chanya?ahsante nasubiri majibu yako.
 
Ni chakula

Na pia wanazitumia kutengenezea nyuzi za kushonea miili ya wanadam

Ova
 
Bondo haliwezi kuliwa. Huwezi ukala kitu ambacho kinauzwa mpaka milion mbili kwa kilo kikiwa kama ghafi. Hapo hakijaripa ushuru, hakijasafirishwa na hakijaandaliwa kwa kuliwa. Sasa baada ya hayo yote mlaji wa mwisho anakilaga kikiwa na thamani gani. Labda kama milion 5 kwa sahani!!
 
mkuu ahsante kwa majibu yako mazuri,mimi lengo langu hasa ni kufanya biashara ya MABONDO na sio samaki,ila samaki ni kama bonus tu.Naomba ufafanuzi upande wa biashara ya mabondo inafanyikaje ili angalau iwe na matokeo chanya?ahsante nasubiri majibu yako.
Kuna watu wanayakusanya mabondo kama mabondo na kuyapeleka kwa wanunuzi wakubwa. Inamaana nawewe unataka uungane nawao kwa mtaji wa milioni moja. Katika miji mikubwa kama mwanza, msoma, bukoba huwa kuna wanunuzi wa mabondo wakubwa. Wewe unachokifanya unaenda kujua bei kutoka kwao kwa kila grade ya bondo kwa gram. Baada ya hapo nenda ufukwe wowote wenye vifaa vingi vya uvuvi ukiwa na mzani mdogo wa ki dictal. Anza biashara yako ya kununua mzigo ukitosha unapeleka kwa wakusanyaji wakubwa basi.

Nibiashara tu yaukusanyaji wa mzigo kwa kutumia mzani kama biashara zingine. Suara la faida kubwa ama ndogo itatokana na uelewa wa watu wanaokuletea mzigo pia yawezatokana na wingi wa wakusanyaji katika kushindana kibei.

Mfano huku niliko watu wanaona tu namba kwenye mzani na kuona wanapewa pesa hata hawajui kipi kilichopimwa yaani hata hawajui hesabu ilivyofanyika
 
hakika nataka niungane nao,vipi kuhusu vibali kwa mkusanyaji mdogo vinahitajika?
 
Back
Top Bottom