Nini masilahi ya Rais Donald Trump kuwataka washirika wa NATO kuongeza bajeti zaidi

Von Bismarck

JF-Expert Member
Jul 11, 2018
3,007
6,102
Rais Donald Trump amewataka washirika wa NATO kuongeza kiasi cha fedha mara mbili zaidi kwaajili ya kuongeza bajeti ya ulinzi ambayo kwa sasa wanachangia asilimia mbili tu,na yeye akiwataka kufikia mchango wa asilimia nne kutoka kwenye pato la mataifa hayo. Hata hivyo pamoja na kuhimiza ongezeko amezitaka nchi hizo kulipa ahadi zao za asilimia mbili mara moja.

Pamoja na rais Trump kuhimiza washirika hao wa NATO kuwa na ongezeko la bajeti ya ulinzi,lakini mataifa hayo yamesema hayawezi kutimiza ahadi zao ifikapo mwaka 2024.

Katika hatua nyingine Trump ameilaumu Ujerumani kwa madai kwamba inatumia kiasi kidogo, katika bajeti ya ulinzi wakati ambapo inatumia fedha nyingi katika ununuzi wa bidhaa za nishati, kutoka nchini Urusi,taifa ambalo walipa kodi wa Marekani wanachangia kodi zao kukabiliana na vitisho vyake.

Kansela wa Ujeruman Bi Angela Merkel,amejibu shutuma hizo za Trump na kudai idadi kubwa ya wanajeshi wake wapo katika vikosi vya NATO

Bi Merkel Anasema "sisi ni taifa la pili kuwa na kikosi kikubwa cha wanajeshi wetu,tunanatoa mchango mkubwa kijeshi kwa NATO na kushiriki kwa kiwango kikubwa kule Afghanistan,kulinda hata maslahi ya Marekani kwa sababu ya ushiriki wao Afghanstan,jambo ambalo ni mfano wa kuiunga mkono Marekani, kwa mjibu wa kifungu namba tano cha NATO'' Bi Merkel.

Hata hivyo katika mkutano wao wa pamoja na waandishi wa Habari na Bi Angela Merkel,Trump ameonekana kubadili msimamo wake na kuwa na kauli za kuiunga mkono Ujerumani.

"Tumekuwa na mkutano mzuri,tunajadili matumizi ya kijeshi,tunazungumza kuhusiana na biashara.Tuna uhusiano mzuri sana na Kansela na uhusiano mzuri na Ujerumani. Tunaamini kuwa tunafikia mafanikio makubwa sana,na biashara yetu itakua,na mambo mengine mengi yataongezeka.Lakini tunasubiria na kuona nini kinatokea miezi michache ijayo".

Mkutano wa Brussels unakuja ikiwa ni takribani wiki moja tu kabla ya Rais Trump kuwa na mkutano wa kwanza na rais wa Urusi Vladmir Putin mjini mjini Helsinki nchini Finland.
Source: bbc swahili
 
Utani Mazungumzo yatakavyo kuwa:
===
Trump : "Help Vladimir. Honestly I don't have a clue what I am doing !!"
Putin : "Imagine Turkey shoots down your jet over Syria and then you sell them an S-400 system."
Trump : "Huge !!"

Courtesy
-------
Brendan Colohan (RT.com comment section)
 
Hio ni US$ 140 billion kwa Ujerumani kila mwaka na tena fedha ya walipa kodi. Halafu masuala ya kuhoji matumizi ya mwingine na tena akijinunulia mahitaji yake ya msingi ni jambo haliingi akilini
 
Budget ya NATO kwa kiasi kikubwa inabebwa na Marekani.

Pamoja na kwamba faida za kiulinzi ziko zaidi sana kwa nchi za ulaya kuliko Marekani, hata hivyo ni Kwa miaka mingi sasa nchi wanachama hawatoi michango yao inavyopaswa kwa wakati na zaidi sana wanatuma wanajeshi pale wanapotakiwa wakati Marekani ikibeba jukumu la kutoa michango yake na vifaa. Nchi zenye uwezo kama Ujeremani zimejikita kwenye kuchangia maendeleo mengine na kukusanya wakimbizi,huku ulinzi wa Europa ukiachwa mikononi mwa Marekani. Hilo ndilo linalomkera Trump na kuamua kuwapa za uso waeuropa huku akiwasifia ujinga.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom