Nini maoni yako juu ya Kauli hii niliyoipenda japo ni Kijembe ya Waziri Dr. Mwakyembe?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,876
Leo alipokuwa mgeni rasmi wa mbio za Miguu huko Mkoani Kilimanjaro Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mwanahabari Mkongwe,Mwanasheria Mbobezi na aliyewahi pia kuwa Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dr. Harrison Mwakyembe alitoa ' Kali ' ya mwaka kwa kutoa ' Kijembe ' murua kabisa kwa Watanzania hasa baada ya Kukasirishwa kama siyo Kukerwa na Kitendo cha Tuzo zote za juu isipokuwa moja tu kuchukuliwa na Wageni kutoka nchini Kenya.

" Watanzania ni Watu wa ajabu sana na Mimi huwa siwaelewi yaani hapa katika mashindano haya ya Kukimbia Kili Marathon wamefanya vibaya na hawawezi kukimbia ila ngoja wafanye maandamano huko barabarani halafu Polisi wapige Mabomu uone watakavyochomoka mbio na ndani ya dakika moja ukimpigia kila Mtu Simu atakuambia ameshafika Kwake na mwingine atakuambia tayari ameshalala huku mwingine anaoga na wote wanakaa mbali. Sasa nawashangaa sana kwanini zile mbio zao za Kufyatuka wanazotuonyeshaga wakiwa wanafurumushwa na Polisi wasizihamishie hapa na kila mwaka Watanzania tukawa tunazoa tu hizi Tuzo? ".

Shikamoo Waziri Dr. Mwakyembe.

Nawasilisha.
 
Ha ha ha ha ha ha, mkuu GENTAMYCINE you have made my day! Nimecheka sana tena sana, kama ni kweli Mwakyembe kasema haya maneno basi naye kapinda kweli.
 
Sterehe ya ' Babaako ' hiyo. Nitukane tena tusi jingine tafadhali kwani katika matusi ambayo nimeanza kuyasikia tokea nikiwa mdogo ni hilo hivyo naomba unipe jipya na ambalo labda kidogo linaweza likaniingia na kunichoma kisawasawa tafadhali.
Pole
 
Ha ha ha ha ha ha, mkuu GENTAMYCINE you have made my day! Nimecheka sana tena sana, kama ni kweli Mwakyembe kasema haya maneno basi naye kapinda kweli.

Ili Chakula kuwe Kitamu hata kama kimeandaliwa na Mpishi mahiri basi si vibaya na Wewe ukaamua kukiboresha japo kidogo kwa kukiongezea thamani na kuweka ' chumvi ' ila ukishaanza tu Kula Chakula chako kiwe kitamu sana ikibidi hadi ujiume na Vidole.

Naona umefurahi na kucheka sana Mkuu. Endelea kuburudika!
 
Ndiyo maana Shunie hamtaki!!

Aliyekuambia Mimi nilikuwa serious na Shunie nani? Basi kwa taarifa yako tu ni kwamba hata kabla ya kuandika ule Uzi nilikutana nae katika uzi mwingine na nikamtania kwa kumwambia kuwa nataka kuwahamisha Watu mawazo na ' nakinukisha ' kwa kumwambia kuwa nampenda ili Jamvi lipambe moto na kweli lilipamba moto. Hata Yeye mwenyewe anaweza akakuthibitishia hili. Katika vitu ambavyo huwa sivipi kabisa vipaumbele humu JamiiForums ni ' Kutongoza ' Mademu na haitokuja kutokea hata siku moja ukaona ' namtongoza ' yoyote humu. Kumbe Wewe ' Bwege Nazi ' ulidhani ulichokiona katika uzi ule ni kweli? You're very ' Ludicrous ' Fella.
 
mwaka huu Tumepanga kukomesha ujinga Jf lazima tuwape middle finger mpaka mkome kupost upuuzi.

Hili ' mido finga ' Kwako Wewe ndiyo Tusi la Kumuumiza GENTAMYCINE? Kama umeishiwa matusi tafadhali sema nikukopeshe kwani naona kama vile unakuwa kama Mtu ambaye unatakiwa uwahishwe mapema sana Mirembe Hospital Dodoma wakakusaidie. Halafu kwa ' Kuniogopa ' zaidi umeamua uje na ID yako nyingine na siyo ile ambayo nimekupa ' dozi ' jana na leo hadi ukakimbia. Yaani ndiyo nakuona bonge la ' Bwege Nazi ' halafu nakucheka kwa dharau kubwa sana.
 
sio mzima uyo kichwa tangia walivyokimwagia tindikali mpaka waleo kiliteleza.

Si ulisema huu uzi wa Ki Qumer kama ulivyoandika mwenyewe pale juu katika post yako #1 sasa mbona tena na Wewe unauchangia kwa kumuongelea huyo huyo Waziri Mwakyembe? Nina hamu tena ya kusikia Tusi lako jingine hivyo nitafurahi kama utaijibu post yangu hii huku ukinisindikiza na Tusi tafadhali. Kuwa huru tu!
 
Waziri wa Mali Asili na Utalii...Dr.Kigwangala
Wazi wa Habari na Michezo...Dr.MwakiyembeWaziri wa Mambo ya
Ndani...Dr.Mwingulu
Wepi wengine wenye Shahada ya Dr ambao ni Mawaziri/Naibu waziri wawe Female au Male
 
huyu naye!! si nasikia alichezea kitaulo, India kikawashinda. sasa katugeukia na kutudhihaki. yeye yupo na walengaji sisi na walengwaji. lakini IPO siku tutawakabili kavu kavu kwa nguvu ya umoja
 
Aliyekuambia Mimi nilikuwa serious na Shunie nani? Basi kwa taarifa yako tu ni kwamba hata kabla ya kuandika ule Uzi nilikutana nae katika uzi mwingine na nikamtania kwa kumwambia kuwa nataka kuwahamisha Watu mawazo na ' nakinukisha ' kwa kumwambia kuwa nampenda ili Jamvi lipambe moto na kweli lilipamba moto. Hata Yeye mwenyewe anaweza akakuthibitishia hili. Katika vitu ambavyo huwa sivipi kabisa vipaumbele humu JamiiForums ni ' Kutongoza ' Mademu na haitokuja kutokea hata siku moja ukaona ' namtongoza ' yoyote humu. Kumbe Wewe ' Bwege Nazi ' ulidhani ulichokiona katika uzi ule ni kweli? You're very ' Ludicrous ' Fella.
Nilitaka nipime level ya akili yako,nashukuru Mungu nimeona level ya IQ yako kwenye sentensi yako ya mwisho!.....Goodnight man!
 
Back
Top Bottom