Nini majukumu ya CAG ikiwa mpaka apate scandal ndo afanye kazi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini majukumu ya CAG ikiwa mpaka apate scandal ndo afanye kazi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Mar 15, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hatari iliyoje kwa nchi kama Tanzania kujidhihirisha haina mpango kazi katika taasisi za serikali na hata mashirika ya umma.Tumekuwa mabingwa wa kuunda tume mbalimbali zisizo na mafanikio bali kukithirisha malumbano na kupoteza muda bila sababu za msingi.Uwajibikaji huu wa kizimamoto kwa serikali yetu utaisha lini na kurudisha nidhamu ya kazi ndani na nje ya taasisi za umma.Wakati mwingine ni vigumu kuamini kama kweli Watanzania tuna ratiba ya mpangilio wa shughuli zetu za kila siku.

  Taasisi mbalimbali ndani ya serikali zimekuwa ndicho chombo madhubuti cha kuhakikisha rushwa inakithiri na taifa kupoteza uhalisia wake mbele ya mataifa mengine.Leo hii utashangaa kusikia kuwa Wamarekani wameionya serikali ya Tanzania kwa kitendo chake cha kushindwa kuwafikisha watuhumiwa wa kesi za ufisadi mahakamani.Oh mara Uingereza imeiwajibisha kampuni iliyo iuziya rada serikali ya Tanzania kutokana na mazinigra ya rushwa.Ina maana sisi wenyewe hatujionei huruma mpaka mataifa makubwa yanatupigia kelele tena kwa kutushinikiza hawatatupa misaada kutokana na kuleana katika kufisidi nchi yetu.

  Serikali kwa kutumia sheria iliyopitishwa na bunge iliunda chombo cha ukaguzi na udhibiti wa mali za serikali na umma kwa ujumla.Kuundwa kwa chombo hiki tulijiaminisha kitafanya kazi yake barabara ikiwa ni pamoja na kupewa meno ya kuweza kuwasimamisha wahujumu wa mali hizo za umma mahakani,lakini cha ajabu siasa immekuwa siasa hata kwa mambo ya msingi.Leo CAG haijulikani ratiba ya mpango kazi wake ikoje,ikiwa mpaka apate mashinikizo ya wanasiasa ndo utasikia CAG amesema.Hatupendi kuamini schudule work ya CAG inamtaka kuafanya kazi za kizimamoto,na kama sheria ndiyo inamuongoza hivyo kuna haja ya kuiangalia upya sheria hiyo.

  Aibu tupu kwa serikali yetu kushindwa kufuatilia mashirika yaliyo ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali kwa kusimamia haki za msingi za watumishi wake.Hivi ni kweli hakuna utaratibu wa kukagua Taasisi za serikali kama vile hospital,mahakama polisi magereza na majshi yetu ya ulinzi na usalama.Nimependa kuzungumzia baadhi ya taasisi kwani ndizo zinaongoza kwa rushwa sana hapa nchini.Huwezi kusikia CAG ameyazungumzia mpaka itokee scandal ama imeibuliwa bungeni au wapinzani wameibebea bango.Hii ni hatari sana kwa maendeleo ya taifa letu.Mathalani Hospitali ya mkoa wa Shinyanga kunaufisadi mkubwa ambao hatuisikii serikali ikiuzungumzia wala kauli ya CAG juu ya ufisadi huo.Kuna watu ambao Watanzania wenzetu hawajalipwa mshahara kwa takribani miezi minne lakini serikali imekaa kimya.Hatujapata gharama ya rennovation kwa majengo yapo hospitali.Watu wanapewa tenda kwa mlango wa nyuma lakini serikali sikivu inayojali watu wake imekaa kimya.

  Barabara ya kuelekea wilaya mpya ya Kishapu aibu tupu,serikali imetenga mamilioni ya shilingi laikini leo hii barabara haipitiki.Tangu kufanyiwa matengenezo barabara hiyo haina miezi minne,lakini serikali imekaa kimya.Labda serikali yetu imekubwa na ugonjwa wa mshtuko,mpaka ishtuliwe ndiyo ikurupuke na maamuzi ya zimamoto yasiyo na tija kwa nchi yetu.Miradi hii ya maendeleo imkuwa haina tja ktaifa na wananchi wake,imekuwa sehemu ya miradi ya wakubwa wachache bila kujali madhara yatakayo ikumba nchi hii siku watu watakaposema sasa basi tumechoshwa na uwizi huu wa kimachomacho.

  Migogoro ya ardhi kila siku inachukua kasi kutokana na utendaji mbovu serikali,wahusika hachukuliwi hatua yeyote kama vile wanachokifanya kina faida kubwa kwa taifa hili.Mkoa huu wa Shinyanga unasikitisha kwa kukithiri kwa kesi za migogoro ya ardhi.Wajane wananyang'anywa hakuna wa kuwatetea,viwanja vya wazi vimetekekwa na wenye pesa lakini si mkurugenzi wala madiwani wanosemea wananchi.Yupo bwana mkubwa mmoja ofisi ya ardhi manispaa anawasumbua sana wananchi na wakubwa wote wanalifahamu hili lakini hawasemi kitu,inaonyesha huyu bwana ana mtandao mkubwa unao sababisha kukandamiza haki ya msingi ya raia wa nchi hii kumiliki ardhi.Ni muda mrfu sasa umepita toka tusikia ziara ya waziri wa ardhi nyumba na makazi mkoani hapa lakini mpaka sasa hajafika,tatizo nini.Sasa hivi mkuu wa koa naye ameingia kwnye mgogoro wa kiwanja na familia ya marehemu mmoja huko maeneo ya Kizumbi.Ikiwa vigogo ndiyo waporaji wakubwa wa mali za wananchi,wananchi wakimbilie wapi?

  Serikali mkoani hapa iliamuru kujengwa kwa stendi ambayo ilikuwa ikitumika maarufu kama stendi mpya,lakini stendi hiyo ilijengwa chini ya kiwango na hakuna hata mhusika mmoja aliyechukuliwa hatua.Kilicho kuja kufanyika ni changa la macho kwa kufunika kombe mwanaharam apite kwa kuhamisha stendi hiyo kwenda eneo ambalo mundo mbinu yake haijakamilika.Yote hii ni kuwaficha wale wote waliofisidi mali za hiyo ya umma iliyojengwa kwa kodi za watanzania.Ina maana CAG halioni hilo yeye na ofisi yake,mpaka lipigiwe kelele na wanasiasa?

  Polisi haki haitendeki,kila mmoja ni mbabe,wananchi wanabambikiwa kesi ilikuwageuza chanzo cha mapato.Wapo vijana ambao ni polisi wanalichafua jeshi letu kiasi cha kujenga chuki na wananchi na kusahau majukumu ya kazi zao.Haki inakandamizwa wananchi hawajui wapi pakukimbilia wapi tunakwenda!?Trafki wanaongoza kwa kura rushwa wazi wazi,mbaya zaidi wana vitabu feki vya notification kwa makosa ya barabarani lakini hakuna uchunguzi uliofanywa na serikali katika kudhibiti uhalifu wa askari wetu katika chombo hiki.Tuna amini kazi ya chombo hiki ni ulinzi wa amani na mali zetu,lakini kimegeuka cha kibiashara zaidi kuliko kutoa huduma.Leo hii ni watu wangapi wanaingia bure mahabusu lakini wanatoka kwa pesa,vinginevyo haki haitendeki.

  Wana JF tuliangalie hili kwa umakini na tuikosoe serikali bila kumung'unya maneno vinginevyo nchi yetu haitatawalika kwani wanyonge wameamka usingizini na wameshagundua hakia zao z msingi katika taifa hili ni zipi.
   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kumbe hufahamu kama vijana wa CAG wapo kazini kila siku wanaenda hadi nje kwenye balozi zetu
   
 3. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ndiyo wanakwenda mbona hatuoni impact ya safari zao?
   
Loading...