Nini madhara ya kuwa na damu nyingi?

Jodeo

JF-Expert Member
Mar 10, 2015
1,286
1,326
Habari Jf Dr?

Hivi majuzi nilipatwa na shida ikabidi nikimbizwe hospital haraka. Haraka nikapigwa drip bila hata vipimo. Wakati nipo kitandani ndipo utaratibu wa kuchukua damu kwa ajiri ya vipimo ukaanza. Hata hivyo hakuna damu iliyopatikana na kukawa na wasisi kwamba sina damu mwilini. Ikabidi watumie njia ya kunichoma kidole ili kuona kama kuna damu. Baada ya kupima wakaona Nina damu nyingi kuliko kawaida(HB).

Nikaskia wanasema hii nayo ni shida! Kipimo kilionesha HB 19! wakati kawaida inapaswa kuwa 15 kwa mwana mume.

Sasa naomba kujua ni nini madhara ya kuwa na damu (HB) nyingi kuliko kawaida?

Asante.

-Jodeo-
 
Back
Top Bottom