Nini madhara ya kuutangazia ulimwengu kuwa Tanzania ina mlipuko wa Zika kwa 15.6%?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Nafikiri wengi wanaonekana kulichukulia suala tangazo la Zika kwa ulimwengu kama jambo la kawaida. Tunakumbuka Miaka michache iliyopita baada ya madhara ya mlipuko wa dhahiri wa Zika kuikumba Brazil ilifika almanusura michuano ya olimpiki ipigwe marufuku,na hata kombe la dunia nchini humo liliathirika.

Natambua wengi wanafikiri uwepo wa Zika Tanzania utawanufaisha kisiasa au utawasaidia kupata umaarufu kisiasa ndio maana pengine wameibuka watu wanaotumia mwanya huu pengine kufurahia jambo hili.

Sipingi utafiti wa wataalamu wa afya tena ni taasisi ya serikali ila nimetaka kujua kutoka kwa wajuzi ni hatua gani hupitia ili kutangaza janga Fulani kwa nchi hasa la maradhi kwani matamko mengine huleta tafrani kubwa na kuathiri utalii,uwekezaji nk.

Nini madhara ya kuitangaza Tanzania kuwa imekumbwa na janga la Zika? ni taratibu gani hutumika kutangaza majanga? utafiti wa NIMR ulifadhiliwa na nani? kama ni serikali Je serikali ilipewa ripoti kabla ya kutangazwa kwa ulimwengu?
 
Kule brazil waliweka hadi picha.
Mbona hatujaona picha hata moja ya mtoto mwenye zika hapa Tanzania?

Zika mtoto anakuwa na mimacho makubwa na kichwa kiduchu/kikubwa.

Tunaomba picha za hapa Tanzania
Ni kweli mkuu, nini madhara ya kuutangazia ulimwengu kuwa Tanzania imekumbwa na mlipuko wa Zika?
 
Nafikiri wengi wanaonekana kulichukulia suala tangazo la Zika kwa ulimwengu kama jambo la kawaida. Tunakumbuka Miaka michache iliyopita baada ya madhara ya mlipuko wa dhahiri wa Zika kuikumba Brazil ilifika almanusura michuano ya olimpiki ipigwe marufuku,na hata kombe la dunia nchini humo liliathirika. Natambua wengi wanafikiri uwepo wa Zika Tanzania utawanufaisha kisiasa au utawasaidia kupata umaarufu kisiasa ndio maana pengine wameibuka watu wanaotumia mwanya huu pengine kufurahia jambo hili.Sipingi utafiti wa wataalamu wa afya tena ni taasisi ya serikali ila nimetaka kujua kutoka kwa wajuzi ni hatua gani hupitia ili kutangaza janga Fulani kwa nchi hasa la maradhi kwani matamko mengine huleta tafrani kubwa na kuathiri utalii,uwekezaji nk.

Nini madhara ya kuitangaza Tanzania kuwa imekumbwa na janga la Zika? ni taratibu gani hutumika kutangaza majanga? utafiti wa NIMR ulifadhiliwa na nani? kama ni serikali Je serikali ilipewa ripoti kabla ya kutangazwa kwa ulimwengu?

Kakurupuka tu huyo.
Mbavu sana mijitu mingine
 
Acha siasa wewe! Mmekunywa maji ya kijani hadi mmekuwa kama kasuku!! Pale alitangaza matokeo ya utafiti!!!! Hizo siasa zenu pelekeni kule mtaa wa buku saba!! Kama ugonjwa upo upo mbona marekani ilipoonyesha kupitia taasisi yake kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye ZIKA hamkuongea?
 
Kule brazil waliweka hadi picha.
Mbona hatujaona picha hata moja ya mtoto mwenye zika hapa Tanzania?

Zika mtoto anakuwa na mimacho makubwa na kichwa kiduchu/kikubwa.

Tunaomba picha za hapa Tanzania

Natumaini wewe mtoto wako au familia yako ndio itakuwa mrejesho usibishane na phd ya u doctor

wewe kabishane na wakina kigwagalla na wale wote walio disco na kununua majina.

HUNA ELIMU YA JUU

swissme
 
Dr M. Malecela alitangaza matokeo ya utafiti, na akaenda mbali kusema kuwa hatua za kubaini ukubwa wa tatizo hilo zichukuliwe (tahadhari). Ukienda hata katika website ya CDC utaona Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo watu wanatakiwa wachukue tahadhari kuna dalili zote za ZIKA (cautioned destination). Isn't yet epidemic.

KADA
 
Mimi naona faida tu:
1. Watu watachukua tahadhari kwa kutumia vyandarua na kuteketeza mazalia ya mbu na hivyo kupunguza magonjwa mengine kama malaria n.k.
2. Watu wataacha kujamiana hovyohovyo au watatumia kondomu na hivyo kupunguza magonjwa ya zinaa na ukimwi
3. Serikali itaokoa fedha nyingi zilizokuwa zinatumika kuagiza madawa na hasa fedha za kigeni
4. Kama ni kweli ugonjwa huo wa zika upo maambizo yatapungua maana watu watachukua tahadhari
5. Mashirika mbalimbali ya kimataifa yatatoa misaada mbalimbali ya wataalamu, utaalamu, vitendea kazi, madawa na fedha
6. Nchi itajijengea heshima kwa kuwa wakweli na wawazi
7. N.k.
 
Tumia kichwa kufikiri !!
Unauhakika na unacho kizusha?
Mkuu kinachoendelea ni kuwa watu wengi hawaelewi madhara ya kuutangazia ulimwengu kuwa Tanzania imekumbwa na mlipuko wa Zika nimeona pia wengine watafurahi zaidi pale nchi itakapokumbwa na matatizo ya kiuchumi, si kwamba wanampenda Dr.Mwele la hasha bali kwao wamepata hoja ya kisiasa dhidi ya nchi yao.
 
Ni kweli inaweza kupelekea jambo hilo ...na Serikali haina budi kupigana kwa hali na mali kuakikisha jumuhiya za Kimataifa hazipokei taarifa hizo kwa misingi ile ilie ilijitokeza Brazil..Zika iko kwenye jamii magonjwa hatarishi kama ebora sasa kwa kuacha haya aliyoa anzisha Dk Mwele yakasikika na kukubalika Kimataifa basi Tanzania itapita nyakati ngumu Kimataifa..na kuleta kero kwa Watanzania wanaosafiri nje ya Taifa kuwa na ukaguzi wa ziada kuthibitisha afya zao ili waweze kuruhusiwa kuingia Mataifa mengine.

Sijui DK Mwele aliingiliwa na nii kutoa taarifa bila kuzingatia japo sheria mpya ya takwimu na Utafiti...

Nimejaribu kuliangalia swala la Zika Tanzania na jinsi DK Mwele alivyo liachia lifikie Taifa
Binafsi tatizo sio finndigs tatizo ni uwakilishaji wa hizo findings...kwa weyeji wa kanda ya ziwa wana ufahamu wa aina baadhi ya watoto wanaozaliwa na kuonekana na mwonekano wa dalili za Zika.Kuna vijana baadhi tumekua nao miaka na miaka na kama wanavyosema wataalamu Zika iligundulika Tanzania miaka ya 1950.

Kosa la DK Mwele ni kushidwa kuangalia Historia ya Nchi dhidi ya ugonjwa huo ambao kwa Duniani yani mazingira mengine ugonjwa huo umekua marked kama ugonjwa hatari kwa binadamu.Yeye kachukua findings hizo na kuzalisha taaarifa kwa umma yai PUBLIC na hakuzingatia madhara ya kutangaza taarifa hizo Kimataifa na mapokea ya Mataifa mengine juu ya Taarifa hizo ambazo zitapelekea kuathiri uchumi wa Taifa..wakati kiukweli alichokitafiti kiko kwenye maisha ya Watanzania miaka na miaka.

Watanzania wanaishi na Mabusha na Matende huku wagonjwa wakipata matibabu bila tatizo.Hivi ikitokea jiji la New York Marekani ama London Uingereza watu wakaugua ugonjwa wa Mabusha na Matende nina hakika ugonjwa huo utakuwa ni wa Dunia kitaarifa na macho yote yatawekwa kila mahari kuakikisha vimerea vile mtu yoyote alie navyo havuki kuingia Marekani au Uingereza ..Je lakini Tanzania nasi tuemuke kuchukua taarifa zile zile za Marekani ama Uinngereza kama ni Taarifa za Watanzania kuona janga limetufikia na hivyo kupambana kufa na kupona na kuweka Kalantini na kuzuia Shughuri zingine za uchumi kisa kuna ugojwa wa Zika..Nooooo Hapana Big Noooooo.

Mmasai na Mkurya wanaruhusiwa kutembea na kisu ama Rungu jaribu wewe Mpogoro kutembea nacho kama defender aijakuchukua ...kwaii hilo ni kwa sababu ya historicak background...ina justify wao kuwa nazo..Uenda ni kweli tua case ya Zika lakini Kitanzania mapokea yake ni tofauti.

Kuna Mwalimu wangu A level alikua ananifundisha Hesabu ni mjapani siku moja akaugua Mafua [Flu]...hoooo bahati nilikua niko karibu nae kama Mwalimu na rafiki yake...akanipigia simu na kuniomba niwataarifu ubalozi wake kuwa anaumwa sana na wakati wowote akizidi sana basi wajiandae kumludisha nyumbani...Muda wote tunapita katika hatua hizo kwangu ni kicheko mnoooo ukiweka na akili ya Kisekondari nilikua nacheka mpaka machozi kwanimi kwa kuwa Kiafrika kuugua mafua na ukasema unaumwa tena kanda ya Ziwa eti ukaomba udhuru kuwa unaumwa sababu ya mafua wanaume watakucheka na utaonekana wa ajabu sana..Lakii kiukweli kwa wenzetu Mafua ni ugonjwa hatari sana kwao ni moja ya ugonjwa unaowekwa kwenye makudi hatarishi kuondoa uhai wa mtu..Lakini Kibongo tunasambaziana leo baada ya siku tatu,nyumba nzima itasahau kuwa ilikua na Mafua na uenda kidogo itasumbua kwa watoto wadogo na wale ambao kwao ikingia inatoka baada ya wiki nzima,yote iyo ni kwa sababu ya mifumo ya immune zetu na reaction dhidi ya Virus mbalimbali.

Sasa DK Mwale akuzingatia tafisri ya ugonjwa huo Kitanzania wakati amekaa kwenye Matende na Mabusha anajua magonjwa ya Kihistoria ya Tanzania leo hii alishindwa kujifunza juu ya huu wa Zika na kuja na Tafsiri sahihi kuwa kuna Vijana wengi tu wakitaznaia ambao ni victim wa ugonjwa huo miaka na miaka na huu wa kuibuka jana Brazil na kuweka Ramani Kimataifa kwa Tanzania ni rekodi nyingine Tofauti kabisa na ile ya Brazil japo uaweza kuwa ni aina ile ile ya ugonjwa lakini wenye madhara yenye mazingira na mapokea tofauti.

Uzalendo ulitakiwa Sana kwa kuzingatia Uhalisia na sio kuumiza Taifa kwa vigezo vile vi;le vya Taaaluma [Professionalism]
 
Nafikiri wengi wanaonekana kulichukulia suala tangazo la Zika kwa ulimwengu kama jambo la kawaida. Tunakumbuka Miaka michache iliyopita baada ya madhara ya mlipuko wa dhahiri wa Zika kuikumba Brazil ilifika almanusura michuano ya olimpiki ipigwe marufuku,na hata kombe la dunia nchini humo liliathirika.

Natambua wengi wanafikiri uwepo wa Zika Tanzania utawanufaisha kisiasa au utawasaidia kupata umaarufu kisiasa ndio maana pengine wameibuka watu wanaotumia mwanya huu pengine kufurahia jambo hili.

Sipingi utafiti wa wataalamu wa afya tena ni taasisi ya serikali ila nimetaka kujua kutoka kwa wajuzi ni hatua gani hupitia ili kutangaza janga Fulani kwa nchi hasa la maradhi kwani matamko mengine huleta tafrani kubwa na kuathiri utalii,uwekezaji nk.

Nini madhara ya kuitangaza Tanzania kuwa imekumbwa na janga la Zika? ni taratibu gani hutumika kutangaza majanga? utafiti wa NIMR ulifadhiliwa na nani? kama ni serikali Je serikali ilipewa ripoti kabla ya kutangazwa kwa ulimwengu?
Jamaa unapozi hoja kiukomavu sana. Unahoji huku ukielimisha. Nimekuelewa vzr sana hasa kwenye aya ya mwisho ya andiko lako. Kwamba hata kama ni sayansi lkn ni sayansi dhidi ya janga kubwa ambalo linahatua na taratibu zake siyo tu katika kulitafiti bali pia katika kutangaza uwepo wake. Hapo kwenye hatua na taratibu zake ktk kutangangaza ndipo tunapomkamatia Dr. Mwele. Thanks mingi sana
 
Dr M. Malecela alitangaza matokeo ya utafiti, na akaenda mbali kusema kuwa hatua za kubaini ukubwa wa tatizo hilo zichukuliwe (tahadhari). Ukienda hata katika website ya CDC utaona Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo watu wanatakiwa wachukue tahadhari kuna dalili zote za ZIKA (cautioned destination). Isn't yet epidemic.

KADA
Sawa sikatai sasa kwa sababu NIMR ni taasisi ya serikali kwanini asipeleke kwanza wizarani na Ikulu?
 
Nafikiri wengi wanaonekana kulichukulia suala tangazo la Zika kwa ulimwengu kama jambo la kawaida. Tunakumbuka Miaka michache iliyopita baada ya madhara ya mlipuko wa dhahiri wa Zika kuikumba Brazil ilifika almanusura michuano ya olimpiki ipigwe marufuku,na hata kombe la dunia nchini humo liliathirika.

Natambua wengi wanafikiri uwepo wa Zika Tanzania utawanufaisha kisiasa au utawasaidia kupata umaarufu kisiasa ndio maana pengine wameibuka watu wanaotumia mwanya huu pengine kufurahia jambo hili.

Sipingi utafiti wa wataalamu wa afya tena ni taasisi ya serikali ila nimetaka kujua kutoka kwa wajuzi ni hatua gani hupitia ili kutangaza janga Fulani kwa nchi hasa la maradhi kwani matamko mengine huleta tafrani kubwa na kuathiri utalii,uwekezaji nk.

Nini madhara ya kuitangaza Tanzania kuwa imekumbwa na janga la Zika? ni taratibu gani hutumika kutangaza majanga? utafiti wa NIMR ulifadhiliwa na nani? kama ni serikali Je serikali ilipewa ripoti kabla ya kutangazwa kwa ulimwengu?
Watu wanaleta siasa katika masuala ya Taifa
Hata kama kweli zika ipo,dada alitakiwa kupeleka ripoti yake serikalini,waziri ndio mwenye mamlaka ya kutangaza baa kama hilo.
Kupingana hadharani na mkubwa wa kazi ni kosa lingine la kiuwajibikaji
Juzi humu watu walikua wanalaumu waziri kupingana na polisi wake kuhusu taarifa ya watu waliookotwa kwenye viroba.
Magufuli endelea hivyo hivyo tutanyooka tu
 
DR.MWELE NI MBOBEZI WA UTAFITI WA MGONJWA JAMII YAENEZWAYO NA MBU./
•JE ANAWEZA TOA TAMKO BILA TAFITI?
•JE KAMA UPO,SI NI VYEMA KUUDHIBITI MAPEMA, KULIKO KUJIFARIJI HAKUNA,HAKUNA,HAKUNA...
•TUTAKAPOSEMA HAKUNA HAKUNA HAKUNA BAHATI MBAYA UKAWEPO WHO TO BLAME..?/
~>mtaalam anaona tatizo mapema at begin then anabezwa..

×××××××××××××
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom