Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Nafikiri wengi wanaonekana kulichukulia suala tangazo la Zika kwa ulimwengu kama jambo la kawaida. Tunakumbuka Miaka michache iliyopita baada ya madhara ya mlipuko wa dhahiri wa Zika kuikumba Brazil ilifika almanusura michuano ya olimpiki ipigwe marufuku,na hata kombe la dunia nchini humo liliathirika.
Natambua wengi wanafikiri uwepo wa Zika Tanzania utawanufaisha kisiasa au utawasaidia kupata umaarufu kisiasa ndio maana pengine wameibuka watu wanaotumia mwanya huu pengine kufurahia jambo hili.
Sipingi utafiti wa wataalamu wa afya tena ni taasisi ya serikali ila nimetaka kujua kutoka kwa wajuzi ni hatua gani hupitia ili kutangaza janga Fulani kwa nchi hasa la maradhi kwani matamko mengine huleta tafrani kubwa na kuathiri utalii,uwekezaji nk.
Nini madhara ya kuitangaza Tanzania kuwa imekumbwa na janga la Zika? ni taratibu gani hutumika kutangaza majanga? utafiti wa NIMR ulifadhiliwa na nani? kama ni serikali Je serikali ilipewa ripoti kabla ya kutangazwa kwa ulimwengu?