Nini madhara ya kuutangazia ulimwengu kuwa Tanzania ina mlipuko wa Zika kwa 15.6%?

Dr alikurupuka sana tena sana kutangaza kuwepo kwa Ugonjwa wakati alitakiwa atangaze kuwa anafanya utafiti na ni test ya vipimo vya Zika...kuhitimisha nchi ina Zika sio kitu kidogo na kingeweza kutugharimu sana kiuchumu kama hatua zisingechukuliwa.....
Mkuu zinanunuliwa ndege sita ili nchi hii iweze kuwa reachable kutoka kona yoyote ya dunia. Hao unaowapelekea ndege ili waje, wanakuja kutalii na kuwekeza, habari nyeti kama za zika zinahitaji umakini mkubwa kabla hazijasemwa hadharani.
 
Watu wanaleta siasa katika masuala ya Taifa
Hata kama kweli zika ipo,dada alitakiwa kupeleka ripoti yake serikalini,waziri ndio mwenye mamlaka ya kutangaza baa kama hilo.
Kupingana hadharani na mkubwa wa kazi ni kosa lingine la kiuwajibikaji
Juzi humu watu walikua wanalaumu waziri kupingana na polisi wake kuhusu taarifa ya watu waliookotwa kwenye viroba.
Magufuli endelea hivyo hivyo tutanyooka tu
Mkuu, asante sana kwa maelezo yako. Umeongelea insubordination yaani kutokutii mamlaka halali ya kiofisi.
 
Dr Mwele alikuwa akitangaza matokeo ya utafiti uliofanywa na watu wanne yeye km Kiongozi wa NIMR alikuwa na haki ya kutangaza.

Kumbuka ni utafiti na hakusema kuwa Tz kuna mlipuko wa zika.
WHO wamwsema Tz hakuna mlipuko wa zika haina tofauti na alicjosema Dr Mwele kwani amesema kwa sampling iliyochukuliwa na kupimwa imeonyesha kuna vimelea vya zika.
Tunapowaza madhara yatakayotokea kwa Tz kwamba yanaweza kuligharimu Taiga tunakosea kwani naamini usalama na afya ya watz ni ya muhimu kuliko kitu kingine.
Hata hivyo kumbukeni huu ni utafiti wenye mamia ya kurasa dhidi ya tamko la waziri lenye mistari mitano, tumia akili yako kuchagua kipi uamini.
Hata naibu waziri wa afya amesisitiza mkapate chanjo so mjiulize km hakuna vimelea vya zika Tz chanjo ya nini???
Swala la kutangaza utafiti ni tofauti na kutangaza kuwa kuna janga la zika, Dr Mwele hakutangaza janga Bali matokeo ya utafiti.
 
Athari za kiuchumi hutoziona Kwa kutangaza kuna zika, Bali utakuja kuona Kwa kutotangaza ili watu wajue namna ya kuepuka kuambukizwa Ama kujikinga. Na hiyo athari utaiona baada ya miaka 15 ijayo ama kumi Kwa kuwa na wananchi wengi dhaifu wenye mapungufu ya kiafya

Mkuu ahsante sana kwa elimu hii..
 
Mbona tumezoea uongo wao wanasema uchumi upo Imara wakati jamhuri imefilisika kama Ugiriki hata kuajiri walimu manesi na ma dr nimeshindwa na vi wonder vyake52000!!!
 
Nini madhara ya Tanzania kuwa ugonjwa wa zika na taasisi ya utafiti kutangaza kuwa kuna dalili lakini.wanasiasa kusema hakuna kiri kqmq hicho
 
Back
Top Bottom