Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Kwa baadhi ya nchi mfano Afrika kusini kupanda bei ya mkate na maziwa inaweza kugharimu hata kazi ya Raisi au lundo la watunga sera ili kumnusuru Raisi.
Umeme ni gharama mtambuka kwani huathiri majumbani,biashara na viwandani.Kupanda gharama za umeme au kukosekana kwa umeme Tanzania limekuwa ni kaa la moto kwa mawaziri wengi hata kama sababu ni za ukame.
Kwa utangulizi huo juu ni dhahiri serikali ya nchi yeyote hujihami dhidi ya bei na upatikanaji wa nishati ya umeme.Kwani baada ya EWURA kutangaza kupanda gharama za umeme John Mnyika waziri kivuli wa nishati na madili alikuja na tamko zito la kupinga huku akiomba Waziri wa Nishati na Madini Prof.Muhongo na Raisi Dr.Magufuli Watengue uamuzi wa EWURA huku akiahidi kuja na mswada binafsi dhidi ya uamuzi huo.
Ni kweli umeme ulishapandishwa gharama kinyemela toka mwezi disemba kabla hata ya kuidhinishwa? kwanini Tanesco walifanya bila kibali?
Nini madhara ya kupanda gharama za nishati kiuchumi,kisiasa na kijamii?
Nakaribisha hoja za wadau.