Nini madhara ya JK kuwawajibisha viongozi wabovu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini madhara ya JK kuwawajibisha viongozi wabovu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkulima wa Kuku, Mar 4, 2012.

 1. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Tangu aingie madarakani moja ya malalamiko makubwa ya wananchi kwa JK ni woga wa kuchukua maamuzi magumu dhidi ya viongozi anaowateua yeye. Mifano ni mingi: Chenge-mpaka madhara yalipojitokeza ndipo mwenyewe akaamua: Dr. Mwinyi, Mwamunyange kwenye mabomu ya Mbagala na G/mboto -mpaka leo tumepoteza watu wengi lakini wanadunda tu: Jairo, Malima, Ngeleja na rushwa za wazi kwa wabunge -hawa usiseme, mpaka leo maazimio ya bunge hayafanyiwi kazi: Richmond na Dowans saga: Meremeta saga; Dr. Mponda na Dr. Nkya pamoja na madaktari: na mengine mengi. Nini faida na hasara za kushindwa kwake kuchukua maamuzi magumu kichama, kiserikali, kijamii, kirafiki? Je, anawatendea haki watanzania kwa kushindwa kwake kufanya hivyo? Wananchi tunaweza kuchukua hatua gani kumwonyesha kuwa haturidhiki na mambo yake? Nawasilisha
   
 2. D

  Dopas JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2012
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jakaya Mrisho Kikwete hawezi kuwajibisha mtu kwa sababu YEYE mwenyewe mbovu.
  Ubovu wake: Anaongoza nchi kwa ushauri wa familia yake, 1st lady, riz1, na wengine
  Alianza uongozi kwa kuweka wasahiba wake, ambao wengi hawana uwezo, kuwafukuza ni vigumu...
  Anawakumbatia mafisadi wengi, hivyo ni vigumu kuwajibisha mafisadi, kuwawajibisha watu aliowateua hata kama ni wabovu, "eti huo ni upepo tu wa kisiasa, wewe bado kijana katika siasa... utauzoea tu..."
  what a sheet.!!!!
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Mar 4, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Akithubutu kumwajibisha mtu, tutasikia siri zake zote!
   
 4. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mwaga mboga nimwage ugali, akithubutu tu na wao wanamharibia
   
 5. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hii sio lazima iwe kitu kibaya, ubaya unakuja pale unapoisikiliza ushauri wa 1st lady kama Salma Kikwete. What do you expect?

  Huwa najiuliza, tunapiga kelele kwamba ana viongozi wabovu kila siku. huwa najiuliza, yeye mwenyewe anajua kwamba ana wasadizi wabovu? Probably, he do not know....
   
 6. m

  mharakati JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  wanamharibia kitu gani yuko term yake ya mwisho na anashika usukani mabadiliko ya katiba itakayomlinda yeye kama mstaafu? fikiri zaidi huyu ni mswahili tu na waswahili hawataki kuonekana wabaya muda wote..watalalamika chini chini au hata kukuendea kwa mganga lakini hawatataka kuchukua hatua yeyote wenyewe...kwa wale wnaosema amewekwa na kundi fulani mbona Mkapa aliwekwa na all powerfull Mwalimu ila akawa Rais anayejiamini na kuonyesha wazi wazi kujiongoza kuliko alivyokua anaongozwa na Mwalimu? huyu ni mswahili tu
   
Loading...