Nini Maana ya,,,

Ridhiki mafungu saba??

Kwanini si mafungu 3?4?20?etc.
Ndugu yangu, hayo ni mambo ya fasihi na simulizi katika lugha yetu tukufu ya kiswahili. Riziki Mafungu saba haimaanishi kuwa riziki kweli ni mafungu saba, hiyo hesabu ya saba inasimama badala ya wingi kwa kiingereza tunaweza sema several...!
 
Hebu msome huyu mshairi hapa chini, upate kuburudika...!

Riziki ni maksumu, kila mja fungu lake
Humshukia sehemu, Kinyume na wazo lake
Huo ndio ukarimu, Wamola kwa mja wake

Kila shina zao lake riziki anayo Mungu.

Riziki ni mahakumu, Wenzangu lifahamike
Aweza kosa hakimu, Topasi atajirike
Kuna walisha kaumu, Namshindwa tumbo lake

Kila shina zao lake riziki anayo Mungu.

Mola wetu ni karimu, Hakuna mfano wake
Kutowa kwamlazimu, Kila kiyumbe na chake
Ni wa nini ukhasamu, Nahuku msononeke

Kila shina zao lake riziki anayo Mungu.

Kaditamati tamamu, Shairi na lifupike
Tajiri sitabasamu, Fakiri msimcheke
Lenye mwanzo ufahamu, Halikosi mwisho wake

Kila shina zao lake riziki anayo Mungu.
 
Riziki ngegawa mja Makosa yangekuwapo
Angezitimiza haja Wakukosoa hayupo
Angeyatenda mauja Pa kukimbia hapapo

Kila shina zao lake riziki anayo Mungu.

Kushinda na zetu njaa Mtetezi asiwepo
Hilo ni kubwa balaa Ni moto wala si pepo
Tusingejenga tamaa Tamaa zisingewapo

Kila shina zao lake riziki anayo Mungu.

Wangeshiba mashujaa Wanyonge pasaliapo
Tungeshibia bakaa Makombo yasaliapo
Tungejifia kwa njaa Vundo la papo kwa papo

Kila shina zao lake riziki anayo Mungu.

Riziki ilipokaa Wajua Mola alipo
Razaki utamjua Riziki aigawapo
Huwezi neno kutoa Jalali hapo alipo

Kila shina zao lake riziki anayo Mungu.
 
Back
Top Bottom