Nini maana ya wakili kujiondoa kwenye kesi ya mteja wake?

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
651
853
Itafaa zaidi ikijibiwa na wenye taaluma ya sheria.

Katika kupitia gazeti la mwananchionline, nilikutana na habari inayosema..'Wakili Ajitoa Kumwakilisha Lema Kesi ya Uchochezi'.......Ningependa kupata mifano na ufafanuzi wa kina juu ya hali kama hii.

Nawasilisha.
 
Hamwakilishi tena (withdrawl) kwenye kesi hiyo kutokana na sababu mbalimbali.
Hivyo anatakiwa kuhandle documents zote na mlolongo wote wa kesi kwa wakili ambaye atakuwa akimwakilisha mahakamani.
 
Asante, ningependa kufahamu sababu hizo na mifano ya kina.

wakili anaweza kujitoa kwenye kesi anayomuwakilisha mteja wake endapo kutakua na sababu za msingi yeye kutokuendelea.

Mathalani wakili akigundua kuna "conflict of interest" katika hiyo kesi basi inampasa ajitoe ili haki itendeke. Ama ikitokea amekosa imani tena kwa mteja kwa mfano mteja kuwa muongo, n.k.

Katika kesi ya Mh. Lem Wakili aliyekua anamtetea alidai hataweza kuendelea kumtetea mteja wake kutokana na kushindwa kupata mwenendo wa shauri hilo licha ya kuomba mara tatu, ili aweze kukata rufani Mahakama Kuu.
 
Back
Top Bottom