Nini Maana Ya Viongozi Kutoa Pesa Mifukoni Kwa Ajili Ya Maendeleo?

Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,568
2,911
Members of JF tunazungumzia dhana ya ufisadi, ulaji rushwa ufujaji wa mali za umma. Lakini kuna jambo moja ambalo linanitia mashaka matumizi na mantiki au lengo madhubuti. Karibu viongozi walio wengi wanatuhumiwa kwa kupata kura kwa rushwa. Kwa walio madarakani wanajizatiti kwa kutoa vitita vya pesa na misaada I can call petty kwa walalahoi wa nchi na hivyo kuendela kutesa kila changuzi na kwa maana hiyo ufisadi na ulaji rushwa utakoma vipi?

Wabunge kadhaa wa majimbo wnashiriki katika maendeleo katika constituency zao kwa misaada ya kujenga shule, vituo vya afya, kujenga barabara wakitoa pesa zao cash mifukoni. Je mantiki hiyo ina lengo gani? Wananchi hawasikii harambee ikitangazwa au fund raising. Mfano hai ni Jimbo la MUSOMA vijijini. Kuna mabango 'MKONO KWA MKONO' kila junction ya barabara.

It means hakuna mtu atathubutu kuomba ubunge MUSOMA unless anatoa kitu kwa wananchi. Ulizeni na fanyeni tafiti What he has done. JE source ya pesa ni halali? Mana hapo ndiyo penye shida. Iweje mtu mmoja ajenge shule kadhaa na kukbidhi serikali iendeshe. Je utoaji wa aina hiyo unadumisha democrasia au unaua demokrasia. Katika jamii iliyotawaliwa na umaskini uliotokana na mifumo mibaya na uongozi mbaya je mtu aina hiyo utamhesabu kuwa mwadilifu? Je hiyo sio Mass Rushwa? Je Ni wangapi a kina Mkono? Rais katoa miilon kadhaa kwa mikoa je ni za serikali au binafsi. Nafikiri watu wanahitaji a good vision na strategy za kuondoa umaskini badala ya kuendelea na system ya baysitting.

JE tuna akina mkono wangapi out of 40 million Tanzanians? ili waendelee kugawa misaada free. Je kiongozi Bora wa Tanzania katika karne ya 21 ni yule mtoa mali yake kwa maendeleo hata kama njia alizopata mali hiyo wananchi hawaelewi. Je ni msingi gani tunajenga ya kuwapa wananchi ability wao wenyewe kujitegemea na kuondoa umaskini? Angeanzisha labda kampuni la kukopesha kwa low interest ili walalahoi wakope watafute na kjiajiri iwe katika uzalishaji au biashara ningemuona wa maana rather than kutumia pesa kununua kura. Je mtaji huo TUTAFIKA?
 
Mimi naona maana yao hasa ni kutupumbaza sisi wananchi kwamba wao ni watu wenye huruma sana kwa ajili ya kujaribu kusaidia maendeleo yetu. Lakini wakati mwingine kwakuwa wao wanajiita vigogo wakiwa na maana ya watu wenye pesa kufanya hivyo ni kuonyesha uwezo wao kuwa wao ni high class. Kuna maana nyingi sana lakini isitoshe hela zenyewe wanazotoa hazitoki mifukoni mwao bali ni hela ya serikali. Kwa lugha nyingine wanafanya kampeni kimya kimya. Yaani tunawapa pesa wazidi kutuziba macho yetu tujue wapo pamoja nasi kwa gharama yetu.
 
hii hoja imekaa vibaya.
kwa sababu kuna wale wanaotowa kitu kidogo kwa majimbo yao kwa nia ya kuchaguliwa tena uchaguzi unaofuata.

kuna na wale wanaotowa kwa moyo wa kutaka kusaidia majimbo yao kwa vile wameona hakuna jitihada zozote za serikali za kusaidia.

sasa kumjua yupi ni yupi ni ngumu mpaka pale serikali itapofanya kazi yake sawa sawa na ikawa hakuna sababu ya wabunge kusaidia kwa pesa zao za mfukoni. jambo ambalo haliwezi kutokea leo wa la kesho kwa vile serikali imelala na imelala usingizi mzito kweli kweli kama si kuzimia kabisa!
 
Thanks Guys for yr responses. Thats where we need critical thinking. Sometimes tuunde agenda za kujadili. Maada nzito na zenye kuleta mwamko wa kisiasa, kiuchumi na maendeleo. Pamoja na kazi nzuri inyofanywa na members hapa ya kudodosa news mablimbali still inbidi tuwe na agenda huru asila. bila kusubiri kwanza magazeti yaandike halafu kazi yetu ni kucoment. Well done all.
 
Suala hapa ni kuwawezesha wananchi na pia kumobilise wananchi waweze kufanya shughuli zitakazoweza kuwaletea maendeleo na kujikwamua toka katika lindi la umaskini. Hawa wanaotoa fedha zao wanatia kichefuchefu kwani hawa si viongozi bora wala nchi hii haiwezi kuendelea kwa vihela vyao uchwara, wanachofanya ni kutumia udhaifu na umasikini wa wananchi kujijengea mazingira bora wakati wa kutafuta uongozi - Hii nayo ni rushwa katika sura nyingine!
 
Uhamasishaji wa kutoa pesa mtu mmoja kwa ajilia aya maendelo ya umma. na amtu mwenyewe akiwa ni kiongozi wa kupigiwa kura inatia mashaka sana. Hapa wot I wanted to say ni kuwa Tanzania ya leo hasa walalahoi wamagubukwa na na viongozi wenye mali. kama huna mali unaonekana hufai tena. lakini hizo ni dalili tu. Kabla ya hapo viongozi walikuwa wanaoujua kuuchapa ulimi sawsawa. wakashindwa kuleta mabadiliko. Sasa hiyo imebadilika Viongozi wameamua kuchukua jukumu mikonni mwa binafsi. Implication yake ni kuwa Rushwa haitaisha! viongozi wataendelea kumbua utajiri wa nchi kwa njia zozote zile ili kuendelea kugawa ama kutoa misaada kwa maskini waliporwa utajiri wao. Sasa hii chain How will you break it? Leo nimesoma hapa Serengeti imeuzwa na vitega uchumi mbalimbali wakubwa wanagwana. watoto wao wanasomeshwa good Universities in the world wanarudi kuchukua nafasi za wazazi wao. wana vyeti hata kama ni vilaza. Je walala hoi when will you break out this chain? Waliosoma Mlimani rejea DS ya ngware!
 
je kuna mfano wa sehemu yoyote duniani ambapo wamelazimisha kuvunja chai hiyo?
kama ipo, je wewe uko tayari kufanya walichofanya?
if yes, tujiunge, if no then let us enjoy talking.
 
It true that whatever good name may be given wheather chai, kahawa mlungula, kisafisha macho, still the same is bad. na kwa bahati mbaya hufanyika kimyakimya na kwa usiri ingawa matokeo ndiyo yanatisha na yanonekana. Lakini kwa Tanzania naona it is an open. Haina maana kuiita rushwa tena. nafikiri kamuzi ya kiswahili sanifu watafute maana ingine. Iweje mtu agawe pesa holela na there is no one ku doubt. Kukaa kimya ni kukubali kushindwa. Hata mwalimu wakati wa kuomba uhuru aliwahi kuwaambia waingereza kuwa kama hawatasilikiza kilio cha watanganyika kuomba uhuru then tungewashitaki kwa Mungu. therefore Dont give up kemea na people should see it as not good.
 
:confused: Members of JF tunazungumzia dhana ya ufisadi, ulaji rushwa ufujaji wa mali za umma. Lakini kuna jambo moja ambalo linanitia mashaka matumizi na mantiki au lengo madhubuti. Karibu viongozi walio wengi wanatuhumiwa kwa kupata kura kwa rushwa. Kwa walio madarakani wanajizatiti kwa kutoa vitita vya pesa na misaada I can call petty kwa walalahoi wa nchi na hivyo kuendela kutesa kila changuzi na kwa maana hiyo ufisadi na ulaji rushwa utakoma vipi?
Wabunge kadhaa wa majimbo wnashiriki katika maendeleo katika constituency zao kwa misaada ya kujenga shule, vituo vya afya, kujenga barabara wakitoa pesa zao cash mifukoni. je mantiki hiyo ina lengo gani. Wananchi hawasikii harambee ikitangazwa au fund raising. Mfano hai ni Jimbo la MUSOMA vijijini. Kuna mabango 'MKONO KWA MKONO' kila junction ya barabara. It means hakuna mtu atathubutu kuomba ubunge MUSOMA unless anatoa kitu kwa wananchi. Ulizeni na fanyeni tafiti What he has done. JE source ya pesa ni halali? Mana hapo ndiyo penye shida. Iweje mtu mmoja ajenge shule kadhaa na kukbidhi serikali iendeshe. je utoaji wa aina hiyo unadumisha democrasia au unaua demokrasia. Katika jamii iliyotawaliwa na umaskini uliotokana na mifumo mibaya na uongozi mbaya je mtu aina hiyo utamhesabu kuwa mwadilifu? Je hiyo sio Mass Rushwa? je Ni wangapi a kina Mkono? Rais katoa miilon kadhaa kwa mikoa je ni za serikali au binafsi. Nafikiri watu wanahitaji a good vision na strategy za kuondoa umaskini badala ya kuendelea na system ya baysitting. JE tuna akina mkono wangapi out of 40 million Tanzanians? ili waendelee kugawa misaada free. Je kiongozi Bora wa Tanzania katika karne ya 21 ni yule mtoa mali yake kwa maendeleo hata kama njia alizopata mali hiyo wananchi hawaelewi. Je ni msingi gani tunajenga ya kuwapa wananchi ability wao wenyewe kujitegemea na kuondoa umaskini? Angeanzisha labda kampuni la kukopesha kwa low interest ili walalahoi wakope watafute na kjiajiri iwe katika uzalishaji au biashara ningemuona wa maana rather than kutumia pesa kununua kura. Je mtaji huo TUTAFIKA?

Kwako ndugu Maarifa:

Naona umekazania sana jinsi ya pesa zinavyotolewa. Lakini hilo lisiwe ni tatizo kubwa sana. Tatizo liwe uwezekano wa matumizi ya pesa hizo katika kuboresha maisha ya walengwa.

Kwa mtu kama mimi nineyeamini kuwa kitu chochote chenye thamani ni pesa, ningekutaka vilevile uulize kwanini elimu inatolewa bure Tanzania.

Kiongozi anayekupa ahadi ya kwenda shule bure na anayekupa pesa wanafanya kitu kinachofanyanana. Wanatoa kitu cha bure chenye thamani ambacho wakati mwingine hujakifanyia kazi.
 
Labda nimetumia falsafa iliyo na mizizi ya ya chini sana. Elimu haitolewi bure. katika kaui wengi husema elimu ni bure. Lakini ukifanya ucahmbuzi yakinifu sio kama ilivyo. watu wanalipa kodi, wananchi wanachangia kuanzia pesa za ujenzi hadi kununua vifaa vya shule. Labda enzi za mwalimu amabko kodi ilifutwa. Tatizo sio kuhamasisha watu kuleta maendeleo . Hiyo ndiyo wananchi wanahitaji. Kiongozi ni lazima awe na vision. Vison amabayo ni sustainable, inayowapa wananchi capability ya kuendelea kujenga their own life. All I am saying is double sided version the art of baystting of leaders na on the other hand the art of Hidden CORRUPTION.
 
Back
Top Bottom