S.N.Jilala
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 540
- 507
TAFAKURI.
Nini maana ya "Vetting", na kuna umuhimu upi wa kufanya "Vetting" Serikalini na kwenye Taasisi zetu zote?.
Vetting ni neno la Kiingereza, lakini sijui linaitwaje kwa Lugha yetu ya Kiswahili. Vetting ni mchakato unaofanyika hasa wa kufuatilia Historia ya mtu kabla ya kumwajili au kumpa zawadi ya heshima iwe kwenye Taasisi au serikalini. Watu wengi tunaamini kuwa watu ambao wanatakiwa kufanyiwa Vetting ni watu ambao wanataka kuajiliwa katika Idara nyeti tu hasa USALAMA WA TAIFA. Lakini, sehemu nyingi kama zinataka kuajili watu huwafanyia watu Vetting, japokuwa si ile Vetting ambayo anafanyiwa ambaye anataka kupatiwa nafasi kubwa.
Kwa kazi ya kawaida, mara nyingi Vetting yao ni kutumia CV ya mtu fulani na watu wanaokufahamu ukiacha ndugu zako yaani Referee. Hii ni Vetting fupi kabisa ambayo inasaidia angalau kujua A,B,C fupi kuhusu mtu ambaye mnatakiwa kumwajili. Kama huyo mtu anataka kuchukua nafasi kubwa sana kwenye Taasisi, iwe ya serikali au binafsi, anatakiwa kufanyiwa Vetting kubwa zaidi. Uchunguzi lazima uwe wa kina zaidi kuhusu mtu huyo.
Kwa mfano, hamuwezi kama Taifa kumuweka mtu kuwa Mkuu wa Majeshi kabla ya Taasisi husika hazijamfatilia kwa undani kabisa kuhusu Historia yake kiutendaji na kimaadili pamoja na vitu vingine ambavyo wataalamu wa vetting wanavijua.
Jambo hili la Vetting halijaanza leo, limeanza zamani sana. Hata enzi za Mababu zetu hili jambo lilikuwepo sana. Ili Jamii ikutawaze kuwa Chief kwa mfano, lazima uwe umeshaonyesha huko nyuma Uzalendo na Uaminifu mkubwa sana katika utendaji wako na umeonyesha mambo makubwa pia. Hapo zamani Jamii zetu zilikuwa zinazingatia mambo mengi sana, mojawapo ni kuwa na uwezo mkubwa wa kutumia "Nguvu za Giza" kuwazidi wote katika Jamii.
Vetting ilikuwepo zama na zama na Mababu zetu walikuwa wanafanya japo zinatofautiana na za sasa hasa katika njia, mbinu na kinachoangaliwa hasa. Mengine kwa mfano Uzalendo, Uwezo wa kutenda jambo husika na Maadili huwa ni mambo ya msingi sana tangu zamani. Na endapo Mtawala yoyote akagundua kuwa Msaidizi wake kwa mfano hana sifa zile ambazo alizitegemea, hakika wale wanaohusika na "Vetting" mara nyingi walikuwa wanapata wakati mgumu sana.
Nini faida ya "Vetting"
1. Kujirizisha kama huyo mtu mnayetaka kumwajili kama ana sifa ambazo amesema anazo.
2. Kuangalia mambo mengi sana ukiacha uwezo tu wa kufanya hiyo kazi; pia kuangalia kama ana maadili ya kutosha kukabidhiwa nafasi hiyo kubwa.
3. Kujirizisha zaidi na zaidi maana huyo mtu anaweza kuwa ni Jasusi na mkaliingiza Taifa lenu katika kashfa kubwa na kuhatarisha USALAMA WA TAIFA LENU.
4. Kujua uwezo ambao anao kama kweli alisitahili kuwa nao, hapa ni kufuatilia kama kweli anachokionyesha ni halali kabisa.
5. Kufuatilia kwa undani kama alishawahi kupatikana na makosa ya jinai kama kuuwa na mengine ili kujua kwa nini alifanya hivyo; n.k
Kwa hiyo basi, kama nilivyosema hapo juu, kama mtu anataka kuchukua nafasi kubwa zaidi Kiserikali au Taasisi binafsi, ni lazima afanyiwe Vetting. Tena Vetting ya undani ambayo ni Professional Vetting. Taasisi binafsi au Serikali inawajibika kufanya hivyo kwa sababu huyo mtu anaenda kukabidhiwa majukumu makubwa mojawapo ya majukumu ni ya SIRI KUBWA kuhusu Taifa au Taasisi. Ndiyo maana, Mataifa mengi wanapenda sana kuwapatia nafasi kubwa watu waliopitia maswala ya USALAMA WA TAIFA kwa sababu wanajua umuhimu wa kutunza siri. Au wanapatiwa watu ambao ni waaminifu sana na wamethibitika hivyo kulingana na walikopita baada ya Vetting kufanyika.
Rais wa Taifa lolote lile, mara nyingi huletewa majina ambayo yameshafanyiwa Vetting na Taasisi husika. Na endapo itathibitika kuwa wasaidizi aliwachagua hawana sifa ambazo alizitegemea, lazima asikitike sana na inabidi awe na wajibu wa kutatua changamoto hiyo. Na aliyethibitika hivyo, moja ya njia rahisi kabisa ni kuwajibika haraka sana iwezekanavyo ili angalau aonekane kuwa naye ameguswa na jambo hilo. Ndiyo maana tunaona mara nyingi viongozi wengi wakiwajibika Duniani kote.
Vetting ni jambo ambalo lina njia, mbinu, ujuzi na malengo yake. Nchi zilizoendelea ni rahisi sana kufanya Vetting kwa sababu Historia za watu kuhusu wao binafsi na kazi zao huko nyuma ziko wazi kabisa na zinaelewaka. Pia zipo kwenye mitandao. Huku kwetu, ni ngumu sana kufanya Vetting kwa sababu ya maisha tuliyonayo kwa ujumla. Kwa mfano, ni kawaida sana kuzaliwa na ukawa mtu mzima ukiwauliza wazazi wako pengine hawajui ulizaliwa lini na wao hawajui walizaliwa lini. Na hili lipo sana katika jamii za Wakulima na Wafugaji.
14/03/2017