Nini maana ya ukimya wa Vyombo vya Habari kujadili mwenendo wa Spika na Bunge lake?

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
Tunamshukuru Spika wa zamani Mhe. Pius Msekwa kwa kujaribu kuzungumzia kasoro na mwenendo wa bunge la Job japo alitumia akili kubwa zaidi kwa kuzungumzia wale wabunge wa viti maalum wa Chadema maarufu kwa jina la Covid -19 lakini lengo kubwa ni kutaka kuarifu umma kuwa maamuzi mengi ambayo amekuwa akiyafanya job likiwemo lile la kuacha kuwafuta ubunge wale waliokuwa wabunge wa Chadema waliofukuzwa kipindi za mwishoni mwa Bunge la 11(Lwakatare na wenzake)

Msingi wa hoja yagu ni kwamba tulitarajia kwa sasa hoja na malumbano makubwa katika nchi yetu hasa kwenye vyombo vya habari ni kuhusu mwenendo wa Bunge la spika Job hasa kutokana na sarakasi na matukio mbali mbali mfululizo ambayo yamekuwa yakijitokeza hivi karibuni.

Vyombo vya habari mnatuangusha saana aisee.... pamoja na madudu mliyoyafanya wakati wa uchaguzi badilikeni basi muuze. Hamuoni kuwa manapoteza mapato siku hizi!
 
Hatuna vyombo vya habari tuna wachumia tumbo tu wanaojali maslahi yao na si ya Nchi.
 
Unapokuwa na serikali ambayo sio ya waadilifu ikitokea ukawajadili jiandae kupotezwa. Hebu angalia uchaguzi ulikuwaje na watanzania wako kimya japo wanajua fika mchakato ulikuwaje. Na chombo chochote kitakachowajadili hao wakora kitapewa adhabu ya kukata na shoka, na wakati mwingine kuwakuta ya Azory.
 
Back
Top Bottom