Nini maana ya TANZANIA ni NCHI TAJIRI??

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
Kuna wakati huwa najiuliza maswali majibu yake huwa siyaelewi.Ukizunguka nchi nzima sio makasisi/mashehe/wanasiasa/waganga/wageni woote watakuambia nchi hii ni Tajiri sana kwa kigezo cha Rasilimali nyingi.Sio sisi tu Majigambo haya ya utajiri wa aina hii yapo karibu afrika yote. Mfano NIGERIA afrika inaongoza kwa mafuta lakini leo mafuta huko yananunuliwa kwa foreni kama tiketi za mechi ya SIMBA na Yanga.

Utajiri wa nchi Unapimwa kwa Mali zisizonufaisha wahusika au Uwezo wa wananchi wa nchi hiyo.

1:Uingereza Haina chochote lakini Ilitawala Dunia na kuwa na makoloni kila kona.

2:Japan Kila kona ni volcano udongo mbovu lakn ilitawala karibu asia yote ikiwepo china.

3:Marekani baada ya wazungu kukimbilia huko leo ndio anasujudiwa na Dunia nzima.

4:Singapole - kwa vitu tunavyojivunia haina karibu kila kitu lakn iko juu karibu kila kitu. Mfano Elimu tu Ni ya Kwanza Dunia nzima.
etc......
5: Israel - zaidi ya nusu ya nchi ni jangwa la NEGEV lakini Dunia nzima Wanafunga safari kwenda kujifunza kilimo/ufugaji/science/technology kwa ufupi wanailisha ulaya na sehemu kubwa ya dunia kwa mazao/mifugo na taaluma.

Haya maswali yamenishawishi kurudi nyuma na kutafuta TAFSIRI HALISI YA neno "TANZANIA NI NCHI TAJIRI". hata huyu raia tunaemuita tajiri Hana ujasiri wa kusimama kwenye media na kuelezea na kujibu maswali kuhusu uhalali wa utajiri wake.

Nini maana ya TANZANIA NI NCHI TAJIRI ili tujue ilipojificha siri ya kwa nini NCHI HII NI MASIKINI?

Najaribu kuwaza
 
Yap Tanzania ni nchi tajiri lakini tumeshindwa kutumia resources zetu kujikwamua ki-uchumi. Roman Empire ndiyo ilianza kutawala dunia na ilikusanya tax katika kila nchi waliyotawala kupeleka Rome. Hii ilifanya Roman Empire kuwa dola yenye nguvu sana.

Waingereza waliiga hii style na walianza kutawala Marekani, walikusanya tax ikarudi Uingereza. Walipoenda India waligunda pia chuma, chuma kutoka India ndiyo imejenga reli za uingereza akiwa mkoloni hakununua, hii imempa utajiri. Afrika hakuna anaejua amechukua almasi, dhahabu, shaba nk kwa kiasi gani.

Mpaka sasa Benki kuu ya Uingereza ina dhahabu nyingi sana, uchumi ukitetereka wanaiuza.

Wajerumani na waingereza wanaijua Tanzania kuliko tunavyoijua wenyewe, wanajua wapi watapata nini. Jiulize kwanini wazungu wanaokuja kuloea hawakai DSM wanakwenda Lushoto huko, Mbeyea, Kigoma ect.
 
Tajir kwa rasilimali ila ndo nchi ya amani ambayo raia wake hawana furaha kbs mlo mmoja kwa cku haki inaminywa.ila hii sio amani kwa maono yng ni amani ya uoga ndo imetawala
 
Haka ka style alikoanza nako magu akifanikiwa kufika nako mwisho tutapata jibu la utajiri wa nchi hii ulipo
 
Jiulize swali ni kwanini sarafu yetu iko chini mara 20 ya sarafu ya kenya....?

Tulipopata uhuru thamani zilikuwa sawa ni kipi kilichosababisha sarafu yetu ikose thamani mbele ya sarafu ya kenya wakati tumewazidi karibu kila kitu.
 
Jiulize swali ni kwanini sarafu yetu iko chini mara 20 ya sarafu ya kenya....?

Tulipopata uhuru thamani zilikuwa sawa ni kipi kilichosababisha sarafu yetu ikose thamani mbele ya sarafu ya kenya wakati tumewazidi karibu kila kitu.
Mfumo wetu wa ujamaa, Nyerere alivyokatalia wazungu mikataba ya kuchima madini walileta mgomo baridi kususa kununua kahawa, pamba, chai na katani. Uchumi wetu ulishuka sana.
 
Utajiri bora kuliko wote ni utajiri wa akili.

Kati ya Uswisi na Tanzania, ni nchi ipi iliyo na utajiri wa maliasili?
mkuu nafikili unaenda mahala sahihi.

Utajiri wa kweli ni kichwani. Nimemsikiliza kagame katika Lecture yake pale Havard University kipindi cha maswali na majibu. Anasema Resource Kubwa anayoitegemea sasa ni WATU WAKE sio hayo mavitu.

Ukiwa na watu ELITE, Wenye UPDATES, ALert nchi ndogo kama Rwanda inaweza kutawala Tanzania Tena huku tunawapigia na makofi kabisa. WATU KWANZA. KUna faida kubwa kuwa na Wananchi wenye high Conscious kuhusu wao wenyewe na mazingira yanayowazunguka kuliko kuwa na MAzingira TAJIRI yaliyozungukwa na watu WASIOJITAMBUA kifikra.

Huku ndiko tunapaswa kupaanzia alafu tumalizie kwenye viwanda/au dhahabu
 
Elimu ndio kila kitu kama huna elimu maisha ni magumu sembuse maendeleo
Tulitawaliwa kwa vile hatukuwa na elimu ya kutengeneza zana bora za kivita za kujihami na wakoloni , walituzidi kivita wakatutawala na bado wanatutawala kwa kutumia elimu yao

Elimu ni kikomboleo cha umaskini na si kingine kama unatafuta sababu ni kwanini sisi ni nchi tajiri lakini wananchi wake ni masikini basi ukae ukijua elimu ndio ufumbuzi wa kuondokana na umasikini
sera mbovu ya elimu ndio imetufikisha tulipo
 
Haka ka style alikoanza nako magu akifanikiwa kufika nako mwisho tutapata jibu la utajiri wa nchi hii ulipo

Style nzuri lakini tumeanza kuinvest kwenye vitu tukasahau WATU.
Mabadiliko ya kweli duniani yalianzia Ulaya Magharibi baada ya vita vya zaidi ya miaka 30. Ufumbuzi wa fikra ulaya magharibi "The Enlighnment/ The Age of reasoning ulifuatiwa na MApinduzi ya Viwanda, Mapinduzi ya Viwanda Hayakufuatiwa na MINDSET CHANGE, Ingawa sisi tunaweza kuanza vyote Simultaneously"

Mfano mdogo tu: Asilimia kubwa ya watanzania Tunaishi Vijijini, na Kama kuna sehemu ambapo Bora Aendelee mgeni (mchina/mwarabu/wa kuja) kuliko mwenyeji ni vijiji vyetu hapa nchini. Kama sio Uchawi itakuwa fitna, wiVu, hujuma,kusingiziwa hadi ufeli (fanya utafiti).

Nataka kujua serikali inafanya nini kwa Kundi hili kubwa la watu. Sisi tunaoonana huku hewani angalau tunafunguana bongo kidogokidogo.
 
Kuna wakati huwa najiuliza maswali majibu yake huwa siyaelewi.Ukizunguka nchi nzima sio makasisi/mashehe/wanasiasa/waganga/wageni woote watakuambia nchi hii ni Tajiri sana kwa kigezo cha Rasilimali nyingi.
...Zilizoko ardhini, ndio.

Sio sisi tu Majigambo haya ya utajiri wa aina hii yapo karibu afrika yote. Mfano NIGERIA afrika inaongoza kwa mafuta lakini leo mafuta huko yananunuliwa kwa foreni kama tiketi za mechi ya SIMBA na Yanga.
...Tatizo ni raslimali watu!

Utajiri wa nchi Unapimwa kwa Mali zisizonufaisha wahusika au Uwezo wa wananchi wa nchi hiyo.
...Vyote viwili, ila utajiri wa ardhini hauna maana kama utajiri wa raslimali watu haupo.

4:Singapole - kwa vitu tunavyojivunia haina karibu kila kitu lakn iko juu karibu kila kitu. Mfano Elimu tu Ni ya Kwanza Dunia nzima.
...Orodha hii hapa.

Haya maswali yamenishawishi kurudi nyuma na kutafuta TAFSIRI HALISI YA neno "TANZANIA NI NCHI TAJIRI" Nini maana ya TANZANIA NI NCHI TAJIRI ili tujue ilipojificha siri ya kwa nini NCHI HII NI MASIKINI? Najaribu kuwaza
...Moja ya sehemu ilipojificha "siri" hii ni kwenye hiyo orodha hapo juu.
 
...Zilizoko ardhini, ndio.


...Tatizo ni raslimali watu!


...Vyote viwili, ila utajiri wa ardhini hauna maana kama utajiri wa raslimali watu haupo.


...Orodha hii hapa.


...Moja ya sehemu ilipojificha "siri" hii ni kwenye hiyo orodha hapo juu.
Kwa maelezo yako kwa ufupi, BILA RASILIMALI WATU AU WATU WOTE KUELEMIKA SIO TU KUWA NA ACADEMIC QUALIFICATIONS BALI ABILITY TO UNLOCK OUR POTENTIALS VIJIJINI NA MIJINI. KAULI MBIU YA HAPA KAZI TU ITAISHIA KWENYE KINGO ZA SAKAFU.
 
Style nzuri lakini tumeanza kuinvest kwenye vitu tukasahau WATU. Mabadiliko ya kweli duniani yalianzia Ulaya Magharibi baada ya vita vya zaidi ya miaka 30. Ufumbuzi wa fikra ulaya magharibi "The Enlighnment/ The Age of reasoning ulifuatiwa na MApinduzi ya Viwanda, Mapinduzi ya Viwanda Hayakufuatiwa na MINDSET CHANGE, Ingawa sisi tunaweza kuanza vyote Simultaneously"
...Katika wakati tuliopo, hili suala linakuwa kama kitendawili cha kuku na yai. Ukweli ni kuwa, watu ni muhimu.

...Hata kabla ya maendeleo ya viwanda, kulikuwa na maendeleo ya kilimo, na kabla yake, maendeleo ya biashara. Tuna kazi kubwa!

Mfano mdogo tu: Asilimia kubwa ya watanzania Tunaishi Vijijini, na Kama kuna sehemu ambapo Bora Aendelee mgeni (mchina/mwarabu/wa kuja) kuliko mwenyeji ni vijiji vyetu hapa nchini. Kama sio Uchawi itakuwa fitna, wifu, hujuma,kusingiziwa hadi ufeli (fanya utafiti). Nataka kujua serikali inafanya nini kwa Kundi hili kubwa la watu. Sisi tunaoonana huku hewani angalau tunafunguana bongo kidogokidogo.
...Ukifanikiwa hata nusu kupambana na hayo madudu, maendeleo utayaona.
 
Kuzaliwa kwenye familia yenye baba bondia tena asie pigika sio kigezo cha watoto nao kua ivo unaweza kuta watoto ndo wajinga mno wanashindwa mtumia baba yao kujifunza ngumi kwaiyo hata tanzania sio tajiri sema ina vitu vinaweza tupa utajiri
 
Back
Top Bottom