Nini maana ya sheria? Ni matamshi ya kiongozi au hutungwa na bunge na kuridhiwa na rais? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini maana ya sheria? Ni matamshi ya kiongozi au hutungwa na bunge na kuridhiwa na rais?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jatropha, Mar 31, 2011.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Wanaboard wenzangu naomba kuuliza nini maana ya sheria?

  Je sheria inakuwa sheria pale mtu/kiongozi anapodai kusimamia sheria au sheria hutungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuridhiwa na Rais kwa mujibu wa Katiba yetu?.

  Je inatosha kwa sisi wananchi kudaka matamshi ya viongozi fulani kuwa maagizo yao haya na yale wanayatoa kwa mujibu wa sheria au kuna haja kubwa ya sisi wananchi kutafuta, kusoma, kujifunza na kujua sheria mbali mbali zinazopitishwa na Bunge ili tuweze kujua haki zetu, kuwabaini viongozi wababaishaji na kuondokana na hali ya kuambukizwa umbumbumbu wa sheria za viongozi wanaojifanya magwiji wa kufuata sheria?

  Nauliza hivyo kutokana na sakata hivi karibuni ambapo Waziri wa Ujenzi Mhe John Magufulia alipigwa stop kuendesha bomoa bomoa kwa nyumba anazodai zimejengwa katika hifadhi ya barabara na Waziri Mkuu Pinda na Rais Kikwete.

  Baada ya STOP hiyo, Wengi wetu tumejitokeza kumuunga mkono Mhe John Magufuli kwa madai kuwa anasimamia sheria, lakini sote tumeshindwa kutaja alikuwa anasimamia sheria ipi au vifungu gani vya sheria?.

  Hii inashiria kuwa wote wanaomuunga mkono Magufuli waliamini kauli na matamshi yake ya kufuata sheria kwa 100%. Kutokana na wao kuendelea kulalama huku wakishindwa kuthibitisha madai yao kuwa Magufuli alikuwa akisimamia vifungu gani vya sheria au sheria zipi inathibitisha wote wanaomuunga mkono Magufuli ni mambumbumbu wa sheria.

  Kibaya zaidi kama msemo wa wachina ulivyo "No Research No Rght to Speak" kitendo cha wanaomuunga mkono Magufuli kushindwa kufanya resaearch ya kutupatia uthibitisho wa vifungu vya sheria au sheria wanazodai Magufuli alikuwa anazisimamia hawana haki kuzungumzia masuala ya hifadhi ya barabara kwa kuwa ni mambumbumbu katika eneo hilo. Badala ake wamekuwa wakitegemea matamshi ya Magufuli kusubstantiate madai yao.

  Naomba mwenye mawazo tofauti asiweke kauli za Magufuli kusimamia sheria bila ya kuquote vifungu na sheria anazodai Magufuli anazisimamia.


  KIFUPI ALICHOFANYA MHE JOHN POMBE MAGUFULI NI KUNAJISI KIU KUBWA YA WATANZANIA YA KUPATA VIONGOZI WENYE UJASIRI WA KUSIMAMIA SHERIA BILA YA WOGA, PALE ALIPOKOSA UADILIFU NA UAMINIFU KWA SHERIA ANAZODAI KUZISIMAMIA.

  HIVYO UJASIRI WA KUSIMAMIA SHERIA BILA WOGA NI LAZIMA UAMBATANE NA UADILIFU NA UAMINIFU WA HALI YA JUU KWA SHERIA HUSIKA, KINYUME CHAKE NI MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA AMBAO NI AINA MPYA YA UFISADI HAPA NCHINI.
   
Loading...