Nini maana ya nguvu ya umma katika nchi ya kidemokrasia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini maana ya nguvu ya umma katika nchi ya kidemokrasia?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Nov 10, 2011.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nguvu ya UMMA ni falsafa inayotumiwa na CHADEMA nchini. Nini maana ya yake katika nchi ambayo ni ya kidemokrasia. Nchi ambayo mihimili mikuu ni Dola (Executive) , Mahakama (Judiciary) na Bunge (Legislature).
  Dola -ni Mtawala/Serikali;
  Mahakama-Tafsiri ya Sheria;
  Bunge-Kutunga sheria, kuwakilisa wanachi, Kupitisha bajeti za serikali n.k

  CHADEMA na nguvu ya Umma wana maana gani?

  Naleta kwenu wanajamii
   
 2. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Nguvu ya umma manake mamlaka yote yanatoka kwa umma, hivyo mihimili yote hiyo inaposhindwa kufanya kazi kwa maslahi ya umma, basi umma ndio unachukua jukumu la kuiwajibisha katika muda wowote itakapoonekana inafaa.
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  sijui huelewi nini????
  Inamaanisha kila kitu kuwa chini ya wananchi,
  Si kama saizi kila kitu kipo chini ya MAFISADI!
   
 4. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Demokrasia ni dhana, yaweza kutazamwa tofauti na mwanaCDM na mwana CCM. Hiyo mihimili kama watu wanaona haitendi haki wataikana na kuanzisha haki yao waonayo kuwa sahihi; ndiyo msingi wa "PEOPLE'S Power"-Yaani Nguvu Ya Umma. Kama unafikiri TZ ni nchi yenye demokrasia tele, siku zote wengine watafikiri tofauti kwa sababu unayofaidi tokana na mihimili yako hiyo, wao kwao ni maafa.
   
 5. RUMANYIKA

  RUMANYIKA JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 315
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna aina ngapi ya kamera za kupigia picha?
   
 6. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sina hakika kama unaamini kabisa kuwa Tz ni ya kidemokrasia kwa sababu tu ya mihimili uliyotaja. Lakini twende hivyohivyo tukuelimishe; Nitakupa mfano mmoja tu...Marekani ni taifa la kidemokrasia, lkn kwa mda tumeona ile movement ya occupy wall street. Sasa unaweza kuiitaje ile?... Ni upinzani wa umma dhidi ya mifumo fulani iliyopo.
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  matamshi kama demokrasia na rule of law ni
   
 8. s

  seniorita JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Demokrasia is a relative term....and its meaning is relational too----depends on whose point of view. Nguvu ya umma says everything...it is what the majority think is good for the majority...mihili unayosema are set to serve umma and not to own umma
   
 9. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa wenzetu hapa, nguvu ya umma ni vitisho vya kuvunja amani, sheria na kuminya uhuru wa mihimili ya dola kufanya kazi zake bila woga ala upendeleo. Tumeyaona arusha juzi.
   
 10. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  Sina uhakika kama Tanzania ni nchi ya kidemokrasia!
   
 11. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Maana ya nguvu ya umma ni kwamba mamlaka yote iliyo nayo Serikali yanatoka kwa wananchi na siyo kwa watawala. Mfano mzuri kwa nchi zenye demokrasia ya kweli, Mayor wa Arusha baada tuu ya yale maandamano yale ya January dhidi yake angekuwa ameachia ngazi kwa kutambua kuwa mamlaka ya juu yaani wananchi wamemkataa.
   
 12. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  katiba iko kabla ya vyama vingi, na inasema mamlaka yote itatoka kwa wananchi.
  hapo huelewi nini?
   
Loading...