Nini maana ya neno diwani?

dexterous

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
2,038
3,124
Masalkheri?

Kwa walio wahi kusoma shairi/mashairi nafikiri neno diwani sio geni, Ningependa kufahamu maana na asili ya hilo neno kama litumikavyo kwenye shairi.
 
Nijuavyo Mimi diwani ni jina la jumla la mashairi furani mfano mashairi kama mahaba, wasakatonge, wasodhambi, jiko gani .. ingeweza kuitwa Diwani ya wasakatonge.
 
Tamko Diwani ni tamko lenye asili ya Kiarabu na lina maana zaidi ya moja, na hizi ni miongoni mwazo.

1. Diwani ni sehemu ambayo huandikwa mambo ya kiserikali.

2. Diwani ni kiongozi katika dola.

3. Diwani ni daftari liliokisanya majina ya Wanajeshi ma mfano wake.

4. Diwani ni kitabu kilichokusanya mashairi mengi ya mtu mmoja au ya washairi kadhaa.
 
Ewaaaaa hiyo ya mwisho ndo ilikuwa inanisumbuaga
 
Back
Top Bottom