Nini maana ya miradi kuzinduliwa na mwenge wa uhuru?

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,938
Habari!

Tumeona mara nyingi katika televisheni au kwa macho moja kwa moja miradi ya kati na midogo ikifunguliwa kwa mbio za mwenge wa uhuru.

Miradi hii inayofunguliwa kwa mwenge wa uhuru inakuwa na nini cha ziada kuzidi ile ambayo haijafunguliwa na mwenge wa uhuru?

Na kama hakuna utofauti mkubwa kwanini serikali isitafakari njia nyingine ya kuzindua miradi hii ambayo haitachukua gharama kubwa.

Au uzinduzi wa miradi katika mbio za mwenge ni zao mbadala tu?
 
~~>>>Ni mbinu mojawapo ya "Ufisadi"..... Hakuna lingine la maana.
 
Habari!

Tumeona mara nyingi katika televisheni au kwa macho moja kwa moja miradi ya kati na midogo ikifunguliwa kwa mbio za mwenge wa uhuru.

Miradi hii inayofunguliwa kwa mwenge wa uhuru inakuwa na nini cha ziada kuzidi ile ambayo haijafunguliwa na mwenge wa uhuru?

Na kama hakuna utofauti mkubwa kwanini serikali isitafakari njia nyingine ya kuzindua miradi hii ambayo haitachukua gharama kubwa.

Au uzinduzi wa miradi katika mbio za mwenge ni zao mbadala tu?
Mkuu: hata mambo si msahafu; ni utaratibu tu kila nchi hujiwekea. Huu ni utamaduni wore tumerithi kwa Waasisi wetu. Ulaya ukiwa watu huja sehemu uliyouliwa wanasema maua na mishumaa na postcards kwa mwaka mzima. Wao wanafanya sisi hatufanyi. Na sisi hivyo hivyo: mwenge.
 
Ni muda muafaka kwa Mwenge kuwekwa kabatini.....uwe makumbusho kwa vizazi vijavyo!! Ama la ukimbizwe mara 1 kwa miaka 5 inatosha!!!
 
Back
Top Bottom