Nini maana ya methali hii?

Jitihada haiondoi kudra au (Jitihada haishindi kudra).

Maana yake jambo alilopanga Mungu binadamu hawezi kulipangua.

Jitihada ni harakati za Mungu na kudra ni mipango ya Mungu.

Mfano kama kuna jambo unahangaika nalo ili lifanikiwe hayo mahangaiko yako ndiyo jitihada baada ya kuhangaika jambo hilo likaleta matokeo tofauti na jitihada (mahangaiko) yako basi hapo watu wanaweza kusema kwamba; jitihada haishindi kudra, yaani Mungu ndiye amepanga jambo hilo liende kinyume na jitihada zako.

Kinyume cha jitihada ya mtu ni kudra ya Mungu.
 
Jitihada hazishindi kudra>Bidii au juhudi katika jambo lolote unalofanya haziwezi kuzaa matunda kuzidi vile ulivyoandikiwa na Mungu (kudura/kudra/qadr)
 
Back
Top Bottom