Nini maana ya masoko makubwa na kutapakaa kwa Wamachinga?

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,803
8,794
Mimi ni mkazi wa Dar na Dodoma. Moja ni jiji la kimataifa la biashara na jiji lingine makao.makuu ya nchini. Haya majiji ni machafu sana yametapaa vibanda mpaka barabara zimekosa uhalisia wake.

Nipo Dar lakini juzi na jana nikawa namalizia shughuli zangu niliyoyaona ukweli ni kituko. Mfano Kariakoo hivi sasa kupitia katika mitaa yake ni shughuli kila kona ni vibanda vya wamachinga wamevamia mpaka njia ya mabasi ya mwendokasi. Hapa najiuliza hawa machinga walijengewa soko lao nani analitumia?

Kwanini wasipelekwe huko wakagawia vimbweta ili serikali iweze kukusanya kodi kiurahisi? Nikapita mwenye barabara nzuri sana ila tayari wameshaanza kuweka vibanda vyao pembezoni mwa barabara hapa napata shauku ya kuhoji akili za watendaji wetu. Wamekimbilia kujenga uwanja wa mpira baada ya kujenga soko kwa ajili ya machinga.

Ukipiga hesabu za harakaharaka soko lingewapa faida kubwa kuliko uwanja wanaojenga. Dodoma wanasoko kubwa sana tena la kisasa lakini hakuna wamachinga matokeo yake wanajazana barabarani na kuzuia njia. Kwanini wasigawe bure sehemu ili kuweza kukusanya kodi kiurahisi. Dar imechafuliwa na haya mavibanda ya wamachinga lbs. Mji hauna hadhi tena.
 
Uzi wa namna hii uliletwa Nahisi week iliyopita..

Kwa ufupi ni kero kubwa, Na hua wanalazimisha kuonewa huruma na ukisema hivi unaonekana huna ubinadamu.
 
NaSik wakifukuzwa utasikia ndug wa machame serikal haitetei wanyonge Sasa wafanye nn yaan nyie mbn vigeu geu Sana kwanini.
 
NaSik wakifukuzwa utasikia ndug wa machame serikal haitetei wanyonge Sasa wafanye nn yaan nyie mbn vigeu geu Sana kwannn
Kutengenezwe mfumo sio wafukuzwe. Sijui umeelewa mada ama umekuja tu. Hili soko la Machinga ni hasa kwa ajili ya wachuuzi je linatumika kwa kufuata uhalisia wake?!
 
Back
Top Bottom