Nini maana ya likes kwenye post za misiba na huzuni?

four eyes

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
904
1,399
Habari wadau,

Kwa muda sasa nimekuwa nikiona post mbalimbali za misiba na huzuni mbalimbali Facebook, instagram na humu jamii zikipewa likes.

Kwa uelewa wangu like inatolewa pale mtu anapopenda kilichopostiwa au kufurahishwa na kilichopostiwa, je ina maana wanaolike post za misiba wamependa muhusika kufiwa au kupata balaa flan alilopost?

Sambamba na hilo kuna wale wanaopost SMS ambazo wanazielekeza either kwa mungu au watu ambao wameshafariki napo huwa pananichanganya je aliyekufa anarudi kusoma post mitandaoni? Je Mungu nae huwa anaperuzi mitandaoni?

Labda wajuzi wa mambo mnisaidie kuelewa hayo mambo kama nilivyouliza 1 likes katika post za misiba na huzuni 2 post zinazoelekezwa kwa wafu au Mungu mfano "umenitendea makubwa eeh bwana", au "umenifanya ning'are eeh bwana"je huyo bwana anaperuzi mitandao? Au ingekuwa vyema hayo yakasemwa katika dua na maombi binafsi?
 
Habari wadau,kwa Muda Sasa nimekuwa nikiona post mbalimbali za misiba na huzuni mbalimbali Facebook,instagram na humu jamii zikipewa likes.

Kwa uelewa wangu like inatolewa pale mtu anapopenda kilichopostiwa au kufurahishwa na kilichopostiwa,je Ina maana wanaolike post za misiba wamependa muhusika kufiwa au kupata balaa flan alilopost?

Sambamba na Hilo Kuna wale wanaopost msg ambazo wanazielekeza either kwa mungu au watu ambao wameshafariki napo huwa pananichanganya je aliyekufa anarudi kusoma post mitandaoni?je mungu nae huwa anaperuz mitandaoni?

Labda wajuzi wa mambo mnisaidie kuelewa hayo mambo kama nilivyouliza 1 likes ktk post za misiba na huzuni 2 post zinazoelekezwa kwa wafu au mungu mfano "umenitendea makubwa eeh bwana",au "umenifanya ning'are eeh bwana"je huyo bwana anaperuz mitandao?au ingekuwa vyema hayo yakasemwa ktk dua na maombi binafsi?
Utajua mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lengo la like kimsingi kwa uelewa wangu ni kuvutiwa au kependezwa na jambo au tukio lolote kwenye mitandao ya kijamii.

Hivyo basi kwa uelewa mdogo wa wengi au kwa kukariri manaake kwa mfano wengi wanajua au wana uelewa kwamba kila kitakachokuwa posted kwenye mitandao ya kijamii jambo la kwanza ni ku~like haijalishi maudhui ya kile kilichokuwa posted.

Hivyo basi kwa kukariri hivyo ndipo makosa yanapofanyika kwamba hata kwenye habari za misiba au kuhuzunisha utakuta likes nyingi sana kitu ambacho nadhani sio vizuri.

Kwenye posts za misiba nadhani ni jambo jema kutoa comments kama umeguswa na kuishia hapo na sio ku~like.
 
Jf Founders Ndo Watusaidie, Lkn Tukisema Tutumie Tafsiri Ya Like Km Kigezo Cdhani Km Itakua Sahihi, Kwan Hata Wanao Like Sio Wote Huwa Wanapenda Kilicho Postiwa, Wengine Wanasupport Post Au Comment, Wengine Wakiwa Na Maana Tupo Pamoja Au Kuwa Wameona. Co Kla Mtu Atapata Nafasi Ya Kucomment Kila Kitu Kwenye Social Media. Nadhani Tusijikite Sn Kwenye Maana Kwan Ktk Comp World Itatupa Taabu Maana Programers Hawawez Kuweka Kila Icons Tunazozitaka Cc. Wataangalia Ambayo Ni Common Af Users Nao Wanaweza Angalia Namna Ya Kuitumia. Mtu Akitabasamu Co Km Anafuraha, Inategemea Na Mazngira Wengine Ni Ishara Kuwa Amekasirika. Watu Wanapenda Shortcut Hataki Kupoteza Muda Thatzy Ana Like. Ss Labda Wahusika Waliangalie Hilo Watuwekee Shortcut Ya Huzuni Mf. X Badala Ya Tick.
 
Uliwahi tokea mjadala kule India FB founder alipotembelea na mojawapo mjadala ulikuwa ni huo wa kulike post za huzuni, Alitoa majibu na alifafanua maana ya Like ina maana nyingi mojawapo ni
Kama Asante kwa taarifa, Nimepata taarifa, Tupo pamoja, N.K

Na mjadala huo ndio ukazaa emoji za Huzuni, Upendo, Hasira, Vizuri na Penda. Hizi reaction utazijibu kutokana na aina ya post.
 
Ila hata mimi hizi likes kwenye post za majanga zinanipa wakati mgumu kujua maana yake japo na mimi ni moja kati ya wanao like
 
Lengo la like kimsingi kwa uelewa wangu ni kuvutiwa au kependezwa na jambo au tukio lolote kwenye mitandao ya kijamii.

Hivyo basi kwa uelewa mdogo wa wengi au kwa kukariri manaake kwa mfano wengi wanajua au wana uelewa kwamba kila kitakachokuwa posted kwenye mitandao ya kijamii jambo la kwanza ni ku~like haijalishi maudhui ya kile kilichokuwa posted.

Hivyo basi kwa kukariri hivyo ndipo makosa yanapofanyika kwamba hata kwenye habari za misiba au kuhuzunisha utakuta likes nyingi sana kitu ambacho nadhani sio vizuri.

Kwenye posts za misiba nadhani ni jambo jema kutoa comments kama umeguswa na kuishia hapo na sio ku~like.
Uko Sawa sana bro
 
Back
Top Bottom