Miwatamu
JF-Expert Member
- Oct 2, 2012
- 1,450
- 487
Watanzania woooote kwa sasa tupo katika kipindi cha mpito cha kuandika Katiba mpya itakayotokana na maoni tunayoyachangia hivi sasa. Katika michango inayoendelea, wamejitokeza watu ambao wameeleza mapendekezo mengi mapya ambayo hayakuwahi kuwepo katika katiba ya sasa! Na hii ndiyo maana halisi ya mapendekezo mapya.
Wakati hayo yakiendelea, baadhi ya wananchi wametoa mapendekezo yao ya kutaka kuvunjwa kwa muungano au ufanyiwe marekebisho. Kitu cha ajabu, wakati bado mapendekezo yanaendelea kukusanywa, tayari kuna viongozi serikalini wamesimama na kutamka bayana kuwa hao wote wenye ndoto ya kutaka muungano ufanyiwe mabadiliko wanaota ndoto ya mchana. Kamwe haitatokea.........!!
Sasa nauliza, kama tayari viongozi wetu wanayo majibu ya nini kitakachoandikwa ndani ya katiba mpya kwa nini wapoteze muda kuzunguka nchi huku wakikausha mate ya wakesha hoi bure?
Tulijadili na hili...............