Nini maana ya Kutakasisha pesa na lengo huwa ni nini?

Hili neno huwa nalisikia sikia nimejaribu kufatilia ila sipati maana halisi na mtu anayetakasisha pesa anakuwa anafaidika na nini?

Uzi
Unaiba pesa /unafanya dili haramu kupata pesa ,kisha hiyo pesa iliyopatikana unafungulia biashara halali
 
Unaiba pesa /unafanya dili haramu kupata pesa ,kisha hiyo pesa iliyopatikana unafungulia biashara halali

Hizi mbona tunafanya kila siku makazini huku kumbe na sisi tumo, anyway nimekuelewa asante
 
Mkuu, wengi wa wa Tanzania wakiwemo wanasheria hawaijui sheria ya utakatishaji pesa

Wanachofanya baadhi ya askari wa usalama barabarani ni kuchukua hongo/rushwa na sio utakatishaji hata kama atatumia pesa hizo kununua pikipiki au gari ya kutembelea

Kuna hatua kadhaa lazima zitimie ili tuhuma(kosa) analokamatwa/shtakiwa nalo mtu liingie kwenye utakatishaji. Na kiuhalisia kwa Tanzania hapa ni wachache wanaweza kuingia moja kwa moja kwenye mashtaka hayo

Ndio maana sasa hivi kuna watu wengi sana wametoka magerezani walipokua wanashikiliwa kusubiria kesi zilizokua zinaitwa UTAKATISHAJI PESA(MONEY LAUNDERING )

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka chini ya Mkurugenzi wake wa sasa Bwana Sylvester Mwakitalu imeona kua watu wengi walikua wanabambikiwa shitaka la UTAKATISHAJI PESA ili tu kuwanyima haki yao ya kufuatilia kesi zao wakiwa nje kwa dhamana. Kwa maana nyingine sheria ilikua inatumika kuwaadhibu watu kabda hawajatiwa hatiani na Mahakama

Makosa yaliyopo Tanzania ni pamoja na ukwepaji kodi, matumizi mabaya ya ofisi, kughushi, kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu, wizi nk na katu sio utakatishaji kama ilivyokua inatafsiriwa na waendesha mashtaka enzi za DPP Biswaro Mganga

Mzee baba naona una kitu cha pekee kwenye hili, naona kama una maelezo zaidi ya definition, ningependa utulishe bongo zetu, nadhani utatuSaidia zaidi tulio define Money laundering, hasa hasa kwa trend iliyotokea miaka ya urais wa hayati Dk.Magufuli ndio iliyonifanya kuuliza hii kitu.
 
Hili neno huwa nalisikia sikia nimejaribu kufatilia ila sipati maana halisi na mtu anayetakasisha pesa anakuwa anafaidika na nini?

Uzi
... in brief ni kutumia hela iliyopatikana kiharamu (mihadarati, rushwa, ujambazi, etc) kufanya shughuli halali ili machoni pa umma na vyombo vya dola ionekane imepatikana kihalali wakati sivyo.
 
mfano rahis wa mpka mtu anakamatwa kwa kes ya utakatishaj pesa ua iko hiv umepga pesa sehm kwakua kipato chako hakiendan na pesa hiyo na ikumbukwe serkal inamonta kila akaunt ya mtanzania kwenye mabenk ndio mana leo hii akaunt yako iksoma gafla ml 200 hutaweza kuitoa bila maelezo ya kutosha sasa weng ua wanafanya iv unakuta ana ki biashara let say duka la nguo na anaakaunt benk hizo pesa zake za magumash zko nyumban njia ya kuztakatisha atajfanya mauzo ya dukan kila sku yanaenda benk kwa kufanya miamala labda kila jion anapeleka mlion 1 mpaka 3 na n kila sku apo ndio kutakatsha kumbe mauzo hayafki hata lak 3 lakn anachanga na zile pesa zngne na kwenda ku benk mpaka unakuja kushkwa n pale hesabu znapogoma kubalanc unapoenda wanapokuja watu kama wa tra kukufanyia tathmin ya kulpa kod apo ndipo unapowekwa kwenye blak list na kuanza kuchunguzwa
 
Back
Top Bottom