Nini maana ya kupewa barua ya kujieleza na charge sheet

Musoma Yetu

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
2,626
2,000
Mimi si mtaalamu wa sheria, ila naona utumishi wanachanganya watu. Mfano, unakuta mtumishi hayupo kazini bila taarifa kwa muda wa siku kadhaa, na ukaja ukapewa barua ya utoro kazini, charge sheet na ukaeleza kuwa nilikuwa naumwa na bado naumwa kabla ya zile siku kumi na nne. Baada ya hapo, ukapewa onyo, na ukapewa masharti kuwa sasa omba ruhusa kamili. Nikaandika ruhusa, ila sikupewa wakati details za hospitali zinaonyesha kuwa naumwa. ghafla, nikakatiwa mshahara wkti bado naumwa. Huu ni mwezi wa nane sasa bado naumwa. je, hapo mimi ni mtoro au si mtoro? Maana mi najua kosa la utoro liliisha baada ya charge sheet na kueleza tatizo ni nini.
Hili la kukatiwa mshahara ni sheria ipi inasema ninyimwe
 

Musoma Yetu

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
2,626
2,000
maana, kisheria zijafukuzwa kazi, kwa kuwa nilitoa sababu za msingi, hivyo kulingana na barua za onyo, ina maana waliridhika na majibu yangu. Je, kuna utaratibu wowote kisheria kuzuia mshahara wa mtu, au wameamua kukata mshahara as business as usual
 

NDAMANDOO

JF-Expert Member
May 10, 2012
252
250
Mimi si mtaalamu wa sheria, ila naona utumishi wanachanganya watu. Mfano, unakuta mtumishi hayupo kazini bila taarifa kwa muda wa siku kadhaa, na ukaja ukapewa barua ya utoro kazini, charge sheet na ukaeleza kuwa nilikuwa naumwa na bado naumwa kabla ya zile siku kumi na nne. Baada ya hapo, ukapewa onyo, na ukapewa masharti kuwa sasa omba ruhusa kamili. Nikaandika ruhusa, ila sikupewa wakati details za hospitali zinaonyesha kuwa naumwa. ghafla, nikakatiwa mshahara wkti bado naumwa. Huu ni mwezi wa nane sasa bado naumwa. je, hapo mimi ni mtoro au si mtoro? Maana mi najua kosa la utoro liliisha baada ya charge sheet na kueleza tatizo ni nini.
Hili la kukatiwa mshahara ni sheria ipi inasema ninyimwe
Mkuu pitia vizuri sheria za kazi zimetoa tafasiri nzuri maana ya utoro na masharti ya likizo ya ugonjwa sheria ipo wazi tu. na kama ulikataaliwa ruhusa ulifanya jitihada gani zingine au je uliripoti kwenye chama chochote cha wafanyakazi? na je ripoti ya hospitali ilikupa ED?
 

Musoma Yetu

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
2,626
2,000
Mkuu ID zote ninazo, na nilipeleka malalamiko yangu TALGWU, wakaandika barua, lakini miungu watu wa halmashauri wamegoma kuwa mi mtoro. Nataka nifungue kesi CMA
 

Musoma Yetu

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
2,626
2,000
Pia kama wao wanasema mi mtoro, je nini lilikuwa lengo la barua ya onyo, na wakanipa barua nyingine kuwa jaza sasa ruhusa rasmi ya kuondoka. Nikajaza na nikaondoka. Kwa nini waendelee kusema mi mtoro
 

Deus J. Kahangwa

Verified Member
Jan 7, 2013
184
225
Kwa ufahamu wangu, kulingana na sheria ya ajira na mahusiano kazini no. 6/2004 na kanuni zake GN 42/2007:

1. Mchakato wa nidhamu una sura kuu mbili: informal na formal.
2. Katika informal stage, unaonywa kwa mdomo, na baadaye kwa maandishi kama mdomo hautatosha.
3. Katika formal stage, inayoanza baada ya kuona maonyo ya mdomo na maandishi havisaidii, unapewa hati ya mashtaka (charge sheet/show cause letter). Hati hii huanzisha mchakato wa kumfukuza mtu kazi, endapo atashindwa kutoa utetezi unaokidhi mahitaji.

Kwa hiyo, kiutaratibu, barua ya onyo haipaswi kuambatana na charge sheet. Kama kuna HR Officer kafanya hivyo, amechanganya mambo. Anapaswa kushauriwa vema.

Lakini pia kuhusu utoro, naona kama hujaeleza vizuri kilichotokea sequentially. Ni kama uliomba ruhusa baada ya kuhesabiwa kwamba ni mtoro. Kama ni hivyo, uongea vizuri na mabosi wako.
 

Musoma Yetu

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
2,626
2,000
Kaka nilipewa charge sheet, na nikaeleza vya kutosha sababu za kutokuwa kazini. wakaridhika nazo, na baadae wakanipa barua ya onyo ikinielekeza kufuata masharti ya nini nifanye ili niende kutibiwa. masharti hayo ni pamoja na kujaza fomu maalumu ya kutoka nje ya kituo cha kazi, na inasainiwa na mkuu wa idara. masharti yote nikatimiza. sasa hili la utoro tena linatoka wapi
 

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
3,944
2,000
Mkuu nasubiri ushauri wako, tayari jana nimefungua kesi CMA ya kudai mishahara yangu, je nitaipata??
Mkuu hebu nisaidie nami, kuna kesi ambayo iko hivi, kuna mdogo mdogo wangu wa kike ni mwalimu, alipata taarifa kuwa kuna mwanafunzi Yuko mimba nayeye kama mwalimu akapeleka taarifa kwa mkuu, mkuu akaamua mtoto huyo apmwe bila kutumia wataalamu, mkuu alichukua kpimo na kuwaambia walimu wa masomo ya sayansi wapine , sasa kesi imekuja mkuu inaonekana hana kosa eti alishnikizwa na walimu na baada ya hapo mdogo wangu amekutwa na hatia ya kumpima mtoto ujauzito, hivyo amepewa barua ya kujieleza huku mkuu wakimwacha huru, je mini kifayike hapa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom