Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,636
- 29,511
Wadau Kwema??
Muda mfupi uliopita, aliekua Mkuu wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro ameapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli kua Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi (IGP). Nimeona ameongea maneno yaliyokua yameandikwa kwenye karatasi aliyoshika huku Mkono mwengine ameshika kitabu (nadhani ni Biblia).
Nawaza tu ikiwa hata IGP aliepita ambae ameondolewa kwenye nafasi hiyo Bwana Ernest Mangu nae aliapa/aliapishwa hivyo hivyo, aliekua waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhingo nae aliapa/aliapishwa pia, Hata Wabunge nao hua wanaapa/wanaapishwa mara tu Bunge linapoanza baada ya uchaguzi au kuteuliwa, Viongozi mbalimbali wengi tu hua wanaapa/wanaapishwa kabla ya kuanza utendaji wao lakini mwisho wa siku tunakuja kuambiwa wame- under perform.
Maswali yangu ni kua,
1) Nini maana hasa ya hiki kinachoitwa "Kiapo"??
2) Na kwanini Kinashirikisha Vitabu vya dini/Mungu??
3) Je ni kila mtu ana hofu ya Mungu?? Yaani watu wanaapa ili waogope kua wakienda kinyume na Kiapo basi Mungu atawaadhibu??
4) Je Muapaji hua anaapa mwenyewe kivyake au hua anaapishwa na yule alieko mbele yake?
5) Kama anaapishwa, na huku ameshika kitabu cha dini moja, na yule muapishaji wake ni mfuasi wa dini ingine tofauti na ya muapaji, nini uhalali wa hiki kiapo??
6) Je Kiapo kiko kisheria?? Kwamba sababu wanasaini basi ukienda kinyume na kiapo waweza kshitakiwa? Kama jibu ni ndio tuna mifano hai??
7) Nani au watendaji gani wanaotakiwa kuapa/kuapishwa?? Hawa wanakua wenye sifa zipi hasa??
8) Watendaji wengine wasioapa/apishwa wana faida au hasara gani kulingana na hawa wanaoapa/apishwa?? Yaani tusipoapisha kuna faida/hasara gani??
9) Haiwezekani wale wanaoapa/apishwa wakabadili utaratibu na kufuata ule wa wale wasioapishwa?? Yaani tuwe hatuapishani we uwe Waziri, Mbunge, Jaji, etc ukichaguliwa tu unaanza kupiga kazi??
10) Au haiwezekani wale wasioapa/apishwa wakabadili utaratibu na kufuata ule wa wale wanaoapishwa?? Yaani tuwe tunaapa/apishana kila mahali, hata mhasibu umepiga intavyuu kampuni fulani ukapita fresh basi unaapishwa kwanza
Haya ndio maswali nayojiuliza kila nikiona Mtu anaapa/anaapishwa, naombeni wakuu mnisaidie vizuri kunielewesha angalau nikiona tukio kama hili next time basi nisiwe na maswali mengi sana kichwani.
Karibuni