Nini maana ya kauli hii "NIMEKUBALIA LAKINI TUMIENI BUSARA" tunayoambiwa kaisema Rais?

everybody

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
337
103
Nimelitafakari sana hili suala la posho za wabunge, na mwishowe nikaona kama vile JK na Ikulu yake wanatuchezea akili watanzania. Hivi kama mtu amekuomba kitu, halafu ukamwambia nakukubalia ila tumia busara, je inamaanisha kwamba umemkatalia? Kwa tafsiri yangu hapa ni kwamba JK aliwakubalia wabunge walipwe hizo posho, ila alitaka kutumia maneno ambayo mwisho wa siku kama wananchi wata 'react' kama walivyofanya apate upenyo wa kutokea. Kauli ya JK kwamba anakubali ila wabunge watumie busara, kama kweli ndivyo alivyosema, naona kama ni ya kuudhi na ambayo haina mwelekeo na sidhani kama ilistahili kutoka kwa kiongozi wa nchi.

Kiongozi wa nchi anatakiwa awe ni mtu mwenye kutoa msimamo bila kubabaisha, na maneno yake yawe yenye kueleweka, kwani kama mkuu wa nchi, na amiri jeshi mkuu, ulimi wake ukiteleza kidogo anaweza kutuingiza katika hatari ambayo hatukuitegemea. Natamani sana kama lile dokezo lililotoka kwa JK kwenda kwa Pinda, kuhusu hizo posho lingewekwa hadharani na hapo ndo tungejua JK ni mtu wa aina gani.

Inasikitisha sana. Wote kuanzia hao wabunge wanaotaka kujiongezea posho ili waweze kulipa madeni yao waliyoyaingia kwa ajili ya kufanikisha hanasa zao, na huyu Rais wetu sijui wanatutakia nini sisi Watanzania!
 
Hii kauli ilikuwa ni mtego dhidi ya waziri mkuu, na kwa hakika hapa Rais hakuonyesha msimamo wa moja kwa moja kama amekataa ongezeko, kwa upande mwingine Waziri mkuu aliyetakiwa kutumia Busara, Busara yake ndiyo hiyo aliyoitumia kufanya maamuzi kwa kutumia upenyo ule ule ambao sasa Rais anataka kukwepa.
Kwa hili la Posho, mtazamo wangu ni kwamba Rais na Waziri mkuu wanacheza na akili za watanzania. tusubiri tuone maana inasemekana wabunge wa CCM wameamua kuikomoa serikali kwa kusitisha posho.
 
Maana yake ni "Mimi ni kiongozi legelege siwezi kufanya uamuzi mugumu, hivyo ninawa mikono kama Pilato!"

Pilato (JK) alijua kwamba Yesu (watanzania) hana hatia lakini aliwaogopa Mayahudi (Wabunge).
 
It simply means that the guy is not decisive. Anapenda kufurahisha kila kundi hivyo anaiframe issue in such a way kwamba kama kutakuwa na fallout asiwepo. Yaani abakie kuwa clean
 
Hii ilikuwa kauli ya kumtia kitanzi Pinda , na yeye kwa uzuzu wake akaibebea hivyo hivyo mpaka bungeni kwa bashasha akaipakuwa kumbe pilau limejaa mchanga. KWELI AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZA KWAKO.
 
Hii ilikuwa kauli ya kumtia kitanzi Pinda , na yeye kwa uzuzu wake akaibebea hivyo hivyo mpaka bungeni kwa bashasha akaipakuwa kumbe pilau limejaa mchanga. KWELI AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZA KWAKO.
Kwani rais anapokubali issues kama hii hukubali kwa mdomo tu? Hakuna kutia saini? Wanaojua naomba ufafanuzi!
 
mi nadhani tafsiri sahihi hapa ilikuwa ni kwamba,ni kweli posho zinahitaji kuongezwa lakini tuvute subira kwa kuwa kwa sasa uchumi wa nchi na dunia nzima unayumba.sidhani kama ni sahihi sana kumlaumu rais kwa kukataa kusaini nyongeza ya posho.
 
Mkubali tu kuwa mna rahisi play boy, muhuni, mpuuuzi, asiye na malengo wala maono. Wasaidizi wake wanajaribu kufunika lkn wapi
 
Back
Top Bottom