Nini maana ya hiyo picha.

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,948
710
Fungua hiyo attachment hapo chini kisha toa maoni yako kulingana na hiyo picha.
 
Attachments

  • IMG_6835-755260.jpg
    IMG_6835-755260.jpg
    121.6 KB · Views: 577
Last edited by a moderator:
Kama ni ya siku za karibuni naweza kusema siku hizi watu wazima hawatoki tena kumlaki Jk ameshapoteza mvuto kwa kila mtanzania mwenye akili timamu. I hope huo mvuto utakuwa haupo pale 2010 hata baada ya kula pilau na kupata vit-shirt
 
Fungua hiyo attachment hapo chini kisha toa maoni yako kulingana na hiyo picha.

Mi naona kama watoto walikuwa wakimsogelea JK ili wapigwe picha lakini si kwa nia ya kumshabikia yeye kwani walio wengi hawamtazami yeye badala yake yamegeukia upande mwingine japo sina hakika kama ndo kwa mpiga picha!
 
...Kwa maoni yangu ni mshangao tu kwa hao watoto kumuona huyo bwana mkubwa anang'aa akiwA ameweka vitu kwenye uso wake....nahisi hilo eneo hakuna mtu mwenye mwili unaong'aa kama huyo mtu aliyembele yao it tells from sura za watoto unaowaona sielewi kama weusi wao ni kutokana na ukosefu wa maji au vipi???? But pia yawezekana hata huyo mtu mng'aavuna amevaa vitu usoni anashangaa kama katika dunia hii kuna mahali kwenye watoto wenye afya na mtazamo uliofifia kama wale akifananisha na watoto wake nyumbani (angalia sura ya mtoto wa pili toka kushoto mbele).....Ni jukumu la nani kuwafanya watoto hawa warudishe matumaini tena????? HUYU MTU MNG'AAVU MWENYE VITU USONI ANATAKIWA KUTOA MAJIBU....
 
Duh!! jamaa kawiva lakini watoto choka mbaya sana. Sijui anajisikiaje akiona watu choka mbaya namna hii huku yeye akitalii dunia kwenye G-5.....
 
Kwa wanaojua body language wataweza kuona kwamba JK anawazuga tu watoto lakini mawazo yake hayako nao, hata aliyempa mkono amempa kizugaji tu, amempa mkono lakini hata hamwangalii, anaweza kuwa analia lakini JK hawezi kujua, moreover inaonekana anaangalia past vichwa vya watotot kama vile anasema "Sijui tutamaliza saa nhapi suluba hii nijiondokee".

Unfortunately this is poignantly depicting his entire presidency, he does not have empathy or a care for his people and at this point he cannot wait to be an ex president.
 
Wamepauka hao watoto kwa kweli kama kuna mmoja yaani nywele ni vipilipili uso umepauka kweli.Huyu jamaa naona hata shavu limetoka na amekuwa mweupe kweli!
 
Wamepauka hao watoto kwa kweli kama kuna mmoja yaani nywele ni vipilipili uso umepauka kweli.Huyu jamaa naona hata shavu limetoka na amekuwa mweupe kweli!

Huyo mwenye kipilipili anahitaji wave.....Lol
 
Wamepauka hao watoto kwa kweli kama kuna mmoja yaani nywele ni vipilipili uso umepauka kweli.Huyu jamaa naona hata shavu limetoka na amekuwa mweupe kweli!

Hii ni sura halisi ya watanzania tulio wengi, halafu viongozi wetu wanaimba maisha bora kwa kila mtu. Angalia tofauti iliyopo kati ya kiongozi wa nchi na hao anaowaongoza.

We have a long way to go.

Njimba
 
Huyo mwenye kipilipili anahitaji wave.....Lol

Kwikwikwikwikwikwiiiiiiii!Sasa hicho kipilipili chenyewe kichana hakipiti do you expect wave itashika?Huyu anahitaji chakula bora nadhani Kikwete angevalia njuga suala la chakula bora mashuleni hawa wanafunzi wangekuwa hata na sura za kuvutia.
 
Yaani hata huyo amayeshikana naye mkono haonekani kumjali anayesalimiana naye, huyu mwingine wa kwanza yeye amemuona mpiga picha tu!
 
Nawaona watoto waliopauka,nyuso ziso matumaini
Videvu vimewashuka,we watazame kwa makini
Mashati yasiyofulika,wenye macho buriani
kipilipili kisochanika,hii ni nchi gani

Alie nao kanenepa.ana kijasho shavuni
Tabasamu kawapa,litawatoa gizani?
Wanunulie malapa,labda watathamini
Papa mkubwa papa,mdogo samaki gani?
 
Hata watoto hawana hakika (confused) nini reaction sahihi na kukutana na kiongozi wao.
 
Hilo tabasamu la JK hakupaswa kulitoa kabisa
Kwa sababu hali ya hao wanafunzi ni mbaya kupindukia
He suppose to feel sad about them.
 
Kwikwikwikwikwikwiiiiiiii!Sasa hicho kipilipili chenyewe kichana hakipiti do you expect wave itashika?Huyu anahitaji chakula bora nadhani Kikwete angevalia njuga suala la chakula bora mashuleni hawa wanafunzi wangekuwa hata na sura za kuvutia.

Kevo, wave ita-solve hilo tatizo la kipilipili. Ningemshauri atumie ile aina ya duke. Akishapiga wave, halafu apate lishe nzuri...apende asipende atakwiva tu!!!
 
Kwa wanaojua body language wataweza kuona kwamba JK anawazuga tu watoto lakini mawazo yake hayako nao, hata aliyempa mkono amempa kizugaji tu, amempa mkono lakini hata hamwangalii, anaweza kuwa analia lakini JK hawezi kujua, moreover inaonekana anaangalia past vichwa vya watotot kama vile anasema "Sijui tutamaliza saa nhapi suluba hii nijiondokee".

Unfortunately this is poignantly depicting his entire presidency, he does not have empathy or a care for his people and at this point he cannot wait to be an ex president.

Pundit,

Umekosea bwana,anamtazama yule binti mrembo aliyemrefu na karibia umri wa kuolewa ambaya hayuko kwenye picha!
 
Back
Top Bottom